Je, wajua mkoa wako kilomita huwa zinaanza kuhesabiwa kutoka eneo lipi kuelekea kwingine?

Morogoro km 0 ni roundabout ya msamvu, Dodoma ni roundabout ya nyerere square.
Kwa Dodoma zamani ilikuwa inaanzia POSTA.Lakini Sasa huanzia Round about ya BAHIROAD ambapo Kuna makutano ya barabarani 4,yaani
DOM- MORO-DAR
DOM - IRINGA
DOM - ARUSHA
DOM - SINGIDA - MWANZA
 
Mnara wa Askari jina lingine panaitwa kilomita zero ndipo unapoanza kuhesabu kilomita kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mingine

Je, mkoani kwako huanzia wapi? Kilomita zero iko wapi?
Unao uhakika wa unachodai? Barabara ya Morogoro inaanzia eneo la bandari inapokutana na Barbara ya Sokoine ambapo ni makao makuu ya jiji, hapo ndipo kilomita sifuri. Mnara wa askari ni kilomita za kwenda wapi, maktaba? Usipotoshe watu.
 
Morogoro km 0 ni roundabout ya msamvu, Dodoma ni roundabout ya nyerere square.
Zamani katkati ya mji ndipo palipokua panajengwa posta. Ila kwa mabadiliko yaliyotokana na maendeleo, baadhi ya miji ofisi za posta zimejengwa mpya kwenye maeneo mengine.

Sasa bas, kwa zamani 0km ilikua inasoma posta.
Kwahyo ukiongelea Dodoma, 0km ni posta ya zamani ambayo sasahivi ni TAKUKURU
 
Hapana SIO POSTA YA TAKUKURU NI POSTA YA MKOA KULE RAILWAYS.Halafu pale round about ya POSTA hapakuwahi kuwa na POSTA bali lile jengo la TAKUKURU WANANCHI waliliita POSTA ndo kuzaliwa jina la POSTA
 
Posta ya Railway ni posta mpya.
Awali posta ilikua ilipo TAKUKURU sasa. Kwahyo center ya mji ilikua posta ya zamani. Soma sambamba na post yakwanza uliyoquote.
Mmh pale palikiwa pori mkuu ni mwaka gani palikuwa na POSTA pale Mkuu
 
kitaalamu kilometa sifuri lazima isome kutoka usawa wa maji,,, kwa hapa Dar inasomwa kuanzia kwenye bahari
 
Kwa anaye jua mkoa wa Pwani/mji wa Kibaha atusaidie.
 
Mkuu nimezaliwa na kukulia maeneo hayo hakukuw a na POSTA pale Bali palikuwa na kichaka na korongo stop koki kuu ya idara ya maji
Nimekwambia uliza kwa wakubwa wanaokuzungu.

Wewe umezaliwa wakati hilo jengo limetelekezwa na Posta kwa habari yakua linatitia. Hivyo vichaka viliota wakati jengo limetelekezwa. Jengo hilo lilikua na muonekano wa tofali zakuchoma. Unachokiona sasa sio kilivyokua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…