Chulumeshy
Member
- Jul 27, 2022
- 17
- 11
Tembea upande wa kulia wa barabara,
ili uweze kuyaona vizuri na kupishana na magari yanayotoka unakoelekea na iwe pembeni sana iwezekanavyo.
Upande utakaotembea itakusaidia wewe kuliona gari vizuri au vyombo vingine vya usafirikama vile pikipiki, bajaji na kuweza kukuepushia na madhara yanayoweza kusababishwa na vyombo vya moto mfano ajali kutokana na matatizo ya ghafla kama vile kukatika kwa breki, kupoteza mwelekeo, pancha na mengine yanayoweza kuleta madhara kwa kufanya hivyo inasaidia kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Usidhani kamwe madereva wanakuona
Wanaweza kuwa na mawazo au matatizo mbalimbali yawezekana kutokana na mambo mbalimbali yanayoendelea katika maish ya kila siku ya dereva huyo. Ni bora kuwasiliana macho na madereva ili kuhakikisha kuwa unaonekana. Dereva anaweza kukuona kwa urahisi kwa kuvaa mavazi ya rangi angavu wakati wa mchana. Usiku, vaa vifaa vya kuakisi, au tumia tochi.
Ajali zinaweza kuepukika kama watumiaji wa barabara watazingatia sheria za barabarani.