Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!

Kwa katiba ya nchi hii ni vigumu sana kumpata spika bora. Spika bora ni yule ambaye atakua strong kuongoza kwa haki bila kujali tabaka la watawala au watawaliwa.
 
Tukutane kwenye kikao cha kamati ya maadili, nina bahasha yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana paschali
Kwa sasa hoja kuu ni namna gani tunampata speaker mpya wa bunge.
Mkuu uchumi2018, wewe uko karne ipi?, la Spika limeishapita, Spika ni Dr. Tulia Akson Mwamsasu, kinachosubiriwa sasa ni kukamilisha tuu taratibu!.
P
 
Kwa hiyo ulitaka akudanganye kuwa mihimili iko sawa
Kwa nini wabongo tunapendwa kudanganywa sana tukiambiwa ukweli mchungu tunanuna. JPM aliposema kuna mhimili uliojichimbia tukasema udikteta na ubabe kumbe ndio ukweli.

Kimsingi hio ndio ukweli.
Kikatiba bunge linasehemu 2
1 Bunge na
2 Rais
Yaani mbali ya Urais wake pia yeye ni nusu ya bunge sasa hapo watakuwaje sawa?
 
Tz ilipita kwenye janga kubwa sana ktk awamu ile, alipoingia mama watu tulipumua lakini kwa binti Ackson kuwa sabufa hili nalo ni janga jipya
 
Wewe KILA mtu anayetuliwa unamsifia na kumpamba! Unalenga kufanikisha nini?
Mkuu Yoda, jee ulifanikiwa kusoma pongezi zangu kwenye uteuzi huu?.
P
 
Ndio maana katiba mpya kutenganisha hii mihimili inahatajika sana.
 
Nchi hii kwa vituko haijambo

Pscal Mayala mleta mada ambaye alipata kura moja tu na kura za maoni za ubunge ndani ya CCM na kushika nafasi ya mwisho hicho kinyanganyiro akakosa kuteuliwa kugombea ubunge leo kajigeuza kuwa profesa wa kufundisha Spika wa bunge anatakiwa aweje!!!!!! Ubunge tu ngazi tu ya kura za maoni ulimshinda !!! Leo kajigeuza Profesa wa kueleza Tulia Spika wa bunge zima anatakiwa aweje aiseeeeee!!!

Nchi hii kuendelea safari ndefu
 

Sawa kaka, with age comes wisdom
 
Wanabodi,

Pili tuahidi kumpatia kila aina ya Ushirikiano Spika Mpya Dr. Tulia Akson ili aweze kuwa Spika Bora.
Hongera sana, Spika wetu mpya, Dr. Tulia Akson Mwansasu
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
 
Spika Dr Tulia Akson leo amethibitisha uwezo, she is the best!.
P.
 
Baada ya kumsikia Spika Tulia Bungeni Leo, kwa jinsi alivyo mdhibiti Mbunge wa Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka kwenye issue ya Ngorongoro,
I'm now convinced, Spika Tulia would made the second best Speaker baada ya Sitta.

Na kwa sababu both are lawyers nashauri kuanzia sasa, Spika wa Bunge la JMT lazima awe ni mbobezi wa sheria!.
P
 
Uongo wa kauli ya Spika uko wapi hapo?
 
Sendeka kabanwa kama mjusi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…