Je wajua, ni 7% ya nyoka ndio wana sumu inayoweza kuua binadamu?

Je wajua, ni 7% ya nyoka ndio wana sumu inayoweza kuua binadamu?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Duniani kuna zaidi ya aina 3,000 zilizogundulika hadi sasa. Katika aina hizo ni 600 tu ndio wenye sumu.

Katika nyoka wenye sumu, ni aina 200 sawa na 7% ndio wana sumu ya kuweza kumuua binadamu.

Nyoka wengi huonekana nchi kavu, lakini 70% katika aina za nyoka waliopo wanapatikana kwenye maji, hasa Bahari ya Hindi na Pacific.

Kuna aina tano za nyoka ambao wanaweza kupaa. Kwa mujibu wa ICUN Red list, kuna aina mia za nyoka ambao wako hatarini kutoweka katika uso wa dunia.
1615630772058.png
 
Kuna mmoja huyo siombe narudia tena usiombe kukutana naye?

Hivi unadhani ni yupi huyu?
 
Basi hao %7 ni wengi kuliko hao 93 make huku kwetu kila nyoka ana uwezo wa kuua.
 
Siku akikugonga ukafa ndio utajua %100 ya nyoka wana sumu inayomuua binadamu.
 
Duh! huyo mdudu namuogopa ile mbaya nishawahi toka nae shamba hadi home akiwa ndani ya pickup kwenye gunia ya mkaa nilotoka nayo shamba. Dhuu hatari nilipofika home nataka nishushe kiloba cha mkaa naona kitu nyeusi inatoa kichwa na zile ndimi zake nilichofanya nilisukuma kiloba chini nikaagiza futa ya taa nikakipiga moto hapo nilimdhibiti. Then nikazima mkaa ulobaki[emoji91]
 
Hata wanaoumwa na nyuki huwa ni presha tu,nyuki hana sumu
Mkuu wamaanisha nyuki huyu huyu tumjuae ama ni aina mpya ya Nyuki mwaka juzi tu hapa nimezika ndugu yangu kisa Nyuki ma wewe hapa wasema nini nikuelewe.
 
Back
Top Bottom