Mtafiti77
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 1,877
- 2,314
Changamoto ipo kwenye kufahamu ni yupi amekugonga, mwenye kuua au la. Pia, kutokana na sababu za kiikolojia, unaweza kukuta eneo fulani likawa na sehemu kubwa ya hao wenye kuua kuliko sehemu nyingine au kinyume chake. Kwahiyo, bado hofu dhidi ya nyoka itaendelea kuwepo kutokana na changamoto hizi.Duniani kuna zaidi ya aina 3,000 zilizogundulika hadi sasa. Katika aina hizo ni 600 tu ndio wenye sumu.
Katika nyoka wenye sumu, ni aina 200 sawa na 7% ndio wana sumu ya kuweza kumuua binadamu.
Nyoka wengi huonekana nchi kavu, lakini 70% katika aina za nyoka waliopo wanapatikana kwenye maji, hasa Bahari ya Hindi na Pacific.
Kuna aina tano za nyoka ambao wanaweza kupaa. Kwa mujibu wa ICUN Red list, kuna aina mia za nyoka ambao wako hatarini kutoweka katika uso wa dunia.
View attachment 1724402