Je, wajua ni jinsi gani wakoloni wanatutawala kidigitali (Ukoloni Mamboleo)?

Je, wajua ni jinsi gani wakoloni wanatutawala kidigitali (Ukoloni Mamboleo)?

Basi usitumie simu ya mzungu leta bandiko kutokea chattle kwa kutumia kioo au upepo
Kweli leo hii upo Tanzania asubuhi unaenda ofsini ukifika mzungu anakwambia ufanye kazi flani na flani jiulize kama hamna faida kwanini wanang'ang'ania kuangalia kwenye seva zetu tena za muhimu sana kama hosipitali
 
Njia pekee ya kufanya hivyo ni kuwa na nidhamu ya matumizi ya pesa na rasilimali zetu kitu ambacho hakipo.

Leo unaona pesa zinavyotapanywa huko kwenye utengenezaji wa filamu ya utalii nani yuko accountable kwa shilingi inayohusika kuanzia mwanzo hadi mwisho?

Basi kama hatujaweza kuwa na nidhamu basi utegemezi hautokoma
Asante sana sijamaanisha uache kutumia simu nahitaji tuweze kutumia wataalamu wetu wa ndani kufanya mambo yetu na pale tunapotumiwa tusitumike tuwe wazalendo
Asante sana sijamaanisha uache kutumia simu nahitaji tuweze kutumia wataalamu wetu wa ndani kufanya mambo yetu na pale tunapotumiwa tusitumike tuwe wazalendo
 
Mkoloni ndio amekwambia hayo ni madini.....
asingekwambia ungeendelea kuchezea

Hizo ni myths to brother......mzungu katutangulia kweli.....hapa kwenyewe tunachati kwa kitu cha mzungu au vp?!
Kutumia cha mzungu kisikuondole Uzalendo wako mimi naamini tunaweza sisi kama waafrika kufanya mambo makubwa
 
Sababu misaada ya ulichokitaja ni vertical programs hizo

Leo hii nchi ikijitegemea hautakutana na hayo mambo ila kwa kuwa upigaji umejaa na wapigaji wako bega kwa bega na mzungu yataendelea tu
Kweli leo hii upo Tanzania asubuhi unaenda ofsini ukifika mzungu anakwambia ufanye kazi flani na flani jiulize kama hamna faida kwanini wanang'ang'ania kuangalia kwenye seva zetu tena za muhimu sana kama hosipitali
 
Njia pekee ya kufanya hivyo ni kuwa na nidhamu ya matumizi ya pesa na rasilimali zetu kitu ambacho hakipo.

Leo unaona pesa zinavyotapanywa huko kwenye utengenezaji wa filamu ya utalii nani yuko accountable kwa shilingi inayohusika kuanzia mwanzo hadi mwisho?

Basi kama hatujaweza kuwa na nidhamu basi utegemezi hautokoma
Nakubaliana na wewe asilimia mia moja ukiwa na nidhamu automatic utakuwa mzalendo
 
Sababu misaada ya ulichokitaja ni vertical programs hizo

Leo hii nchi ikijitegemea hautakutana na hayo mambo ila kwa kuwa upigaji umejaa na wapigaji wako bega kwa bega na mzungu yataendelea tu
Nachokiongea kipo siri nyingi za nchi zinavujaa je inamaana hamna wasomi Tanzania wanaoweza kukagua hii mifumo au mpaka tumsubiri mzungu aje kutukagulia mifumo yetu
 
Haaaaaahaaaaa Wazalendo wako wapi jamani Leo Mzungu kumtumia mwafrika kwenye nchi yake anavyotaka nisawa hadi wanasubutu kuwaweka viongozi wanaowataka bado inaonekana ni sawa ,,,,,Aise Mwenda Zake ulisema hadharani msidhani wanatupenda ila wengi wakapuuzia wakasema mbona anatuvalisha,anatusomesha ,anatupa usafiri tutafanyaje acha tu watuongoze sisi tu wadhaifu NASEMA HIVI KWA HERUFI KUBWA SISI TUNAWEZA KUFANYA JAMBO LOLOTE
 
JE WAJUA NI JINSI GANI WAKOLONI WANATUTAWALA KIDIGITALI(UKOLONI MAMBOLEO) NA WALIVYOMZUNGUKA MWENDAZAKE

Habari ndugu zangu wa JamiiForum ,

Ninaanza na kueleza nini maana ya Ukoloni mamboleo ni ile hali ya zile nchi tajiri duniani kuingilia masuala ya nchi zinazoendelea kijamii ,kiuchumi na kisiasa. Mara nyingi huwa wanaingia kwenye nchi hizo wakijaribu kuangalia fursa zilizopo mfano madini,mafuta na mali mbali mbali mfano nchi kama DRC kila kikicha ni vita kwasababu wana eneo kubwa lenye rasilimali nyingi

Kimsingi ukoloni mamboleo ni muendelezo wa sera za kikoloni baada ya uhuru, ambazo zinaendelea kumkandamiza Mwafrika na kumbadilisha afuate taratibu za Mzungu eti kisa wanampa msaada mfano hapa hapa nchini Tanzania kunabaadhi ya hosipitali watu wamekaa maofsini lakini wanaofanya kazi za kimitandao wapo nje kwa kuwa mitambo hiyo ya kidijitali iliwekwa na wazungu kipindi cha ukoloni na hata baada ya ukoloni wazungu humiliki maneno au nywira zote eti kisa wametupatia msaada ila ukifuatilia utakuta waajiriwa wote kwenye hizo taasisi kuanzia darasa la kwanza kasomeshwa na mzungu mpaka chuo kikuu ,huyo huyo mzungu anamtumia mpaka nguo za kuvaa na gari analotembelea ni la mzungu na Watoto wake wanasomeshwa na mzungu basi na ukurugenzi anapewa na mzungu.

Mwisho wa siku kijana mlala hoi wa kimaskini anaajiriwa katika hiyo hospitali anakuta kazi zote zinafanywa na Mzungu remote kitaalamu inatakiwa kuwa na kiunganishi kimoja cha kupata data (IP Adress) lakini unakuta hospitali ina IP Address Zaidi ya saba ambazo hutumiwa kama njia za panya za kuingia kwenye mfumo zinazotumiwa na hao wazungu, inasikitisha sana kama unavojua dunia ya leo data ni kitu cha muhimu sana wazungu wanacho kifanya ni kukopi na kutumiana katika taasisi zao mbali mbali wanaangalia ni jinsi gani Tanzania immeathirika na magonjwa mbali mbali mfano UKIMWI,CORONA, KIFUA KIKUU, daah Mwenda zake akasema hawajui takwimu ila huwezi amini wanazijua, mtoto wa kizungu akitaka kufanya mazoezi anakuja Afrika anawachachana kwenye operation mbali mbali,anamuandikia andikia tuu dawa yeyote mgonjwa wa Kiafrika ,Daktari wa kiaafrika akimwambia unakosea, utasikia yule mwafrika mwenye uongozi aliyesomeshwa na mzungu kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu na anatembelea gari la mzungu anamwambia huna kazi na matusi juu eti kisa kamwelekeza daktari wa kizungu, huu ni ujinga kabisa nashangaa sana mtu anakosa uzalendo eti kisa kasomweshwa na Mzungu ,binafsi nikiwaona wanavyosema wanatupa misaada moja, mbili ,tatu nasita sana na sana ,Kwa ujumla ukoloni maomboleo ni zao la uongozi mbaya ambao huwa na matabaka wenye lengo la kuwafaa wachache ili hali wengi wanaumia haswa wale wasionacho

Namkumbuka sana Mwenda zake kwani alikuwa mzalendo Sanaa waliomtangulia walisaini mikataba ya hovyo hovyo lakini hakufuata hiyo misingi eti kisa aliyemtangulia alinunuliwa nguo na mzungu,kasomeshwa na mzungu,analishwa na mzungu na anatembelea gari mzungu akapambana na mabepari ila wao wakamwita mshamba, kisa hataki kuwa mwanafamilia wa kizungu kwa kukataa tabia zao za hovyo eti mwanaume uolewe inauma sana kwenye rasilimali kama madini eti nchi inapata faida asilimia tano katika miamoja alafu wao wanachukua asilimia 95% akasimama bila kujali waliomtangulia walilishwa na mzungu na kusimamia uzalendo na kuondoa maumivu kwaafrika wenzake,

Chondechonde kama unataka kuwa kiongozi usitumikishwe na ukoloni mamboleo simama uwe mzalendo naamini tutakukumbuka si kwa mabaya bali kwa mazuri mchana na usiku dua zetu kwako,maisha ni mafupi ilikuwa jana tu nilikuwa mchanga leo nimekuwa mzee kesho naondoka ni kheri nisimamie haki leo kesho nitapewa mshahara wangu na allah kule kwenye hazina yangu ya milele

Hitimisho
Naishauri kwanza Kwa viongozi msipende sana vya hao wazungu eti kisa mzungu kakusomesha,anakunulia nguo, amekupa dawa isisababishe uisaliti nchi yako tujifunze kuwa wazalendo kwa sababu wataalamu wapo lakini hawautumii ujuzi wao eti mpaka mzungu afanye inaumaa sana mtoto wa mlala hoi atafanyaje Zaidi ya kukaa kimya

Serikali inabidi itafute wataalamu wazuri wakufanyia ukaguzi wa mifumo yate ya kidijitali kama jinsi wanavyofanya kwenye taasisi zingine mfano ukaguzi wa matumizi ya fedha

Serikali ihakikishe mifumo yote iunganishwe kwenye data center ya taifa na kuhakikisha hakuna anayeweza kuingilia mifumo yote na kuwekeza kwenye technolojia zinazokuja zenye usalama Zaidi kama blockchain

kama kawaida topic imejaa ulalamishi. Tatizo ni ugunduzi nani katuzuia sisi kuwa wagunduzi. Hata kwenye chanjo tumeona sasa wabunifu wetu na wataalamu wako wapi. Wenzetu sio walalamishi . Tengeza whatapp yako nani kakuzuia na weka bila watu kulipa😂
 
kama kawaida topic imejaa ulalamishi. Tatizo ni ugunduzi nani katuzuia sisi kuwa wagunduzi. Hata kwenye chanjo tumeona sasa wabunifu wetu na wataalamu wako wapi. Wenzetu sio walalamishi . Tengeza whatapp yako nani kakuzuia na weka bila watu kulipa😂
backdoor zote lazima zifungiwe Haaaaaahaaaaa aise kipindi cha uchaguzi uliweza kukaa bila internet
 
Kama yepi!!?
Kwenye taasisi kubwa kama hosipitali haswa ambazo wazungu wametoa msaada wa kuweka mitambo ya kidijitali na baadae watanzania wakaajiriwa huwa wanabaki na backdoor nyingi ambazo mwafrika mlala hoi aliyeajiriwa akitaka kuizuiwa ghafla anafukuzwa kazi tena na mwafrika mwenzake ambaye amesomeshwa na huyo mzungu kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuuu fuatilia umuhimu wa data kwenye ulimwengu huu wa technolojia
 
Back
Top Bottom