Je, wajua? - Special Thread

je wajua jf ndo mtandao wa ambao watu wake wanamajina ya ajabu sana? Alafu majina yao yanafanana na tabia zao?
 
je wajua ukimchukua mdudu mende ukamkata kichwa atakufa baada ya siku 3 hadi 5 kutegemeana na mende mwenyewe..na sababu ya kufa kwake sio kwa kuwa umemkata kichwa la hasha ila ni kwa kuwa hataweza kula chakula hvo atakufa kwa njaa
 
je wajua china ina wazungumzaji wengi wa lugha ya kiingereza kuliko marekani.....??
 
je wajua ukichukua eneo la km za mraba za tanzania ukazidisha mara kumi ndo unapata ukubwa wa nchi ya marekani??
 
je wajua kuwa marekani nii nchi ya kumi kwa utajiri kiuchumi??hii ni kwa mujibu wa ripot ya karibuni iliyotolewa na world bank
 
Je wajua bibie OPRAH WINFREY jina lake halisi ni ORPAH na si OPRAH na hii yote imetokana na watu wa karibu yake kushindwa kutamka ORPAH na badale yake ikazoeleka OPRAH
 
Je wajua kicheche ndiye mnyama mdogo sana, lakini ana maajabu makubwa. Ana uwezo wa kumdaka kuku wa aina yoyote kwa kutumia mkia wake.

Lakini cha ajabu zaid hawezi kuishi bila kufanya mapenzi, ana uwezo wa kufanya mapenzi mara 26 kwa siku pia ni sawa na kukimbia umbali wa Km 360 kwa siku.

Na ndio maana mwanamke malaya sana huitwa kicheche najua hujui ila ndio nawajuza zaidi.
 
Mimi ndio najua sasa hivi(unanifahamisha)
 
Kicheche nani alimshududia, watafiti wengine wanatafuta sifa wakati wanajua si rahis kwenda kumchunga akifanya mapenzi.
 
Je wajua! .

Kicheche ndiye mnyama mdogo sana lakini ana maajabu makubwa.

Ana uwezo wa kumdaka kuku wa aina yoyote kwa kutumia mkia wake lakini cha ajabu zaid hawez kuish bila kufanya mapenzi, ana uwezo wa kufanya mapenzi mara 26 kwa siku pia ni sawa na kukimbia umbali wa Km 360 kwa siku.

Na ndio maana mwanamke & Wanaume malaya sana huitwa kicheche

najua wajua ila nakujuza zaidi.
 
hilo la kufanya mapenzi ndio kwanza wanijuza leo asante
 
wewe ni tour guide wa wapi, maana hizi details mh! ok, so a u kicheche too? maana kicheche lazima anamjua kicheche mwenzake?
 

Hahaa Nimeipenda hii ..
Nilikua Sijui Neno Kicheche liliibukia wapi .

Asanye kwa kutujuza .
 
Je wajua bibie OPRAH WINFREY jina lake halisi ni ORPAH na si OPRAH na hii yote imetokana na watu wa karibu yake kushindwa kutamka ORPAH na badale yake ikazoeleka OPRAH

Duuh . Nilikua sijui nimejua sasa .
 
Je wajua chuma kina kawaida ya kupanuka kinapopata joto kwahiyo mnara wa Paris(Eiffel tower) nao kipindi cha joto mnara huo huwa unaongezeka urefu kwa sentimita kadhaa
 
Je wajua Cleopatra aliyekuwa kiongozi Misri ndiye mwanamke mzuri/mrembo kuliko wote duniani pamoja na kuzaa watoto na hatatokea tena kama yeye? Source: soma Biblia takatifu.

Refference ya Source please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…