Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Habari zenu wadau.

Wote tunaamini kua kuna mambo mengi sana ya kisiasa, elimu, sayansi, geografia, na maarifa mengine mengi tu ambapo kwa namna moja au nyingine mtu unakua hujapata fursa ya kuyashuhudia au kuyasikia kwa muda muafaka. Hii inaweza kua kipindi kilichopita au hata kwa wakati huu ulipo.

Basi kupitia Thread hii ni vyema wadau tukafahamishana haya kwa lengo moja la kuelimishana.

Hivyo niwakaribishe wote wenye nia njema kuwekea wayajuayo, kwani ukijuacho wewe naweza nisikijue na akijuacho mwenzanko unaweza usikijue.

Karibuni.

Mende ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote.

Ni mdudu anayeweza kuishi wiki mbili bila ya kunywa maji.

Wakati moyo wa mwanadamu ni mmoja wenye chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu.

Baadhi ya mende wa kike hawaitaji wanaume kuweza kuzalisha mayai hupandana wao kwa wao na kutaga mayai katika kipindi chote cha maisha yao.

Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kupumua.

Mende ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki mbili akiwa amekatwa kichwa.

Ana uwezo wa zaidi ya mara 15 ya binadamu wa kuzuia miale mikali ya nuklia isimdhuru na kubaki hai

Mende ni mdudu asiye na mapafu.

Ana uwezo wa kuruka maili 3 kwa saa











Je, wajua? - Expire date kwenye chupa ya maji ni ya chupa sio ya maji

Je, wajua? - Sidney Etemesi ni mkenya mwenye Jinsia mbili

Je, wajua? - Ebola ni jina la mto
Ni kwasababu pia ndicho kitabu kinachochezewa zaidi kumtukana Mungu
 
Back
Top Bottom