anonymousafrica
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 611
- 640
Tarehe 05 mwezi Februari mwaka 1997 ilikuwa siku muhimu yenye matukio ya kufurahisha na kuhuzunisha. Kabla haujayapitia hayo matukio matatu, Kumbuka siku hii chama cha TANU na ASP viliungana na kuunda Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lakini 1. ASP ilikuwa inatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na siku hiyo ilikua inaagwa rasmi huko mjini Unguja. 2. Tuliadhimisha miaka 10 ya tangu kutangazwa kwa azimio la Arusha 3. Ndio siku ambayo umoja wa Afrika Mashariki ulivunjika.
Rais Kenyatta (Baba) akazishikilia ndege za shirika la ndege kwa kulimbikiza madeni ya matumizi ya uwanja wa Ekmbakasi. Ndege hizo zilibeba baadhi ya viongozi ambao walikuwa wanakuja nchini Tanzania kwa shughuli za kuundwa kwa CCM na MIAKA 10 YA AZIMIO LA ARUSHA