Je, wajua Wakristo huwasindikiza Waislamu Kufunga Ramadhan? Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tutafunga siku 40, vipi Waislamu Mtatusindikiza?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi

Hili ni bandiko la swali kuwa

Je, wajua kuwa sisi Wakristo huwa tunanawasindikizaga ndugu zetu Waislamu kufunga swaumu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan? Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tunaanza safari ya kufunga kwa siku 40, vipi nyie wenzetu Waislamu, je mtatusindikiza kama ambavyo sisi tunavyo wasindikizaga?​


Leo ni siku ya Jumatano ya Majivu, Ash Wednesday ambayo ni kisheria cha mwanzo wa kufunga siku 40 kwa Wakristu kote duniani kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyofunga siku 40 Jangwani kabla ya kusulubiwa kwa mateso, na kufa msalabani siku ya Ijumaa Kuu ambapo Jumapili Alfajiri alifufuka katika wafu, akakaa na sisi duniani kwa siku 40 nyingine kisha akapaa mbinguni. Toka huko atarudi tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu na ufalme wake hautakuwa na mwisho.

Naomba kulianza bandiko hili lina sehemu 3.
  1. Sehemu ya kwanza ni sala ya Kanuni ya Imani
  2. Sehemu ya Pili ni Maana ya Jumatano ya Majivu
  3. Sehemu ya Tatu ni Mastori ya Pasco na Umuhimu wa kufunga.

Sehemu ya Kwanza​

Sala ya Kanuni ya Imani​

Amina.

Sehemu ya Pili

Maana ya Jumatano ya Majivu, hii ni C&P
Kutoka IFAHAMU JUMATANO YA MAJIVU
UTANGULIZI
Sehemu ya Tatu: Mastori ya Pasco
Dini mbili Kuu duniani ni Wakristo na Waislamu, hakuna sensa yoyote iliyowahi kufanyika duniani kuestablish Wakristu ni wangapi na Waislamu ni wangapi hivyo hakuna data nani ni wengi zaidi ya wengine. Kwa Tanzania enzi za sensa za mkoloni waliwahesabu hadi makabila na dini, kuna wakati Waislamu wslikuwa wengi Tanganyika baadaye Wakristu wakawa wengi, tulipuungana na Zanzibar na kwa Tanzania, sensa ya mwisho yenye swali la dini Waislamu wakawa wengi.

Baada ya hapo Mwalimu Nyerere akafuta maswali ya udini, sensa zote zilizofuatia hakuna tena kujua idadi nani ni wengi, ila baada ya Awamu ya kwanza zikaanza kelele za marginalisation ya dini fulani mara, mara ... kwa vile hili sii jukwaa la siasa hayo tuyaache ila sio wengi wanaofahamu kuwa Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba Mmoja, Ibrahim na Sheria ya Mungu kwa hizi dini zote mbili Wakristo na Waislamu ni sheria moja ile ile ya Musa amiliyoshushwa kwenye Kitabu cha Kumbukumbu la Torati ndani ya Biblia Takatifu na Tourat ndani ya Quran Tukufu, na si wengi wanafahamu kuwa Yesu Kristo wa kwenye Biblia aliyezaliwa na Bikira Maria kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ndiye yule yule Nabii Issa Bin Maryam wa kwenye Quran Tukufu.

Hili la Wakristu na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja, Jielimishe zaidi hapa "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!

Ndipo nikagundua kufunga kuna faida nyingi, achilia kufunga kwa ibada, kufunga hata bila ibada ni very beneficial to the body. Mwili unapumzika kufanya metabolism wakati wote hivyo kurelax na kufanya detoxification kuondoa sumu mwilini.

Tofauti ya Kufunga Kikistu na Kiislamu.
Kama nilivyo eleza mwanzo Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, na sheria ya Mungu ni sheria moja ile ile ya Musa, Waislamu wanaendelea kuifuata kama ilivyo, Kiislamu kufunga ni nguzo ya Kiislamu ni lazima.

Yesu alipokuja, hakuja kuitengua Tourat ya Musa, amekuja kuikamilisha, hivyo kufunga Kikistu sio lazima ni unapojisikia.

Kufunga kwa Waislamu ni hakuna kula chochote unakaa na njaa kuruhusiwi hata kunywa maji, ila rukhsa kumeza mate, kufunga kwa Wakristo ni ukozidiwa njaa, unaweza kula kidogo, ukizidiwa kiu unaweza kunywa kidogo.

Kufunga kwa Kiislamu ni kufunga kula tuu kunywa na kutokufanya dhambi ikiwemo kumega 'tunda!' kwa wenye ndoa zao baada ya kufuturu, unashushia chakula cha usiku ikiwemo kumega tunda!. Kufunga kwa Wakristo unaweza kufunga kitu chochote lakini starehe zote haziruhusiwi ikiwemo kumega 'tunda', hakuna cha wenye ndoa zao wala cha nini!, ndio maana wakati wa kipindi cha kwaresma hakuna sherehe yoyote wala ndoa yoyote ya Katoliki maana haiwezi kuwa consummated!

Kufunga kwa Kiislamu ni kufunga tuu chakula, lakini kufunga kwa Wakristo kuna room ya selectivity unachagua kufunga tuu kunywa pombe, au kuvuta sigara au starehe yoyote, mfano kwenda out, kufunga muziki, kufunga kuagalia TV, kufunga mitandao ya kijamii etc.

Kufunga kwa Waislamu kufungulia kunaitwa kufuturu na kunaendana na kuchomoza kwa jua ndio mwanzo wa kufunga na kuzama kwa jua ndio time ya kufuturu, kufunga kwa Wakristo hawana muda maalum wa kuanza wala muda maalumu wa kufungua na kufuangua kwetu hakuitwi kufuturu.

Kufunga kwa Waislamu kuna muda wa kula daku lakini kufunga kwa Wakristo hakuna daku, hivyo kuna baadhi ya Waislamu kwao mwezi mtukufu ni kubadili tuu masaa ya chakula cha milo mitatu, badala ya kula breakfast asubuhi lunch mchana na dinner usiku, ni breakfast anakula saa 12:30 jioni, wakati wa kufuturu, lunch anakula saa 5:00 usiku baada ya tarawea na dinner anakula saa 10:00 alfajir hivyo mchana wake ndio unakuwa usiku na usiku ni mchana.

Kufunga Kiislamu ni hadharani watu wote lazima wajue umefunga na ukikaribishwa chakula popote unasema uko kwenye swaumu, kufunga Kikistu ni siri, huruhusiwi kumwambia mtu yoyote kuwa umefunga na ukikaribishwa chakula popote unasema tuu asante, uko ok bila kusema umefunga.

Kufunga Kiislamu mdomo lazima ubaki mkavu usipake mafuta ili uonekane umefunga, uso unatakiwa kuonyesha huzuni or being serious all the time. Kufunga Kikistu unatakiwa kupaka mafuta mdomoni ili watu wasijue, kuwa umefunga, unatakiwa ku smile wakati wote na kuonyesha furaha na sio huzuni au kukunja uso.

Kufunga kwa Kiislamu ukifika muda wa kufururu ni lazima ufungulie na kufuturu na hakuna kufunga siku ya Idi, kufunga kwa Wakristo ni sio lazima kufungulia ukiweza kufunga two days, three days, 7 days, 40 days kama Yesu, unafunga. Unaweza kufunga foods only ukawa unakunywa maji tuu, hii inaitwa water fast, unaweza kufunga vyakula vyote ukawa ùnakunywa fresh juice only, inaitwa juice fast, unaweza kufunga vyakula vya nyama na starch ukawa unakula mboga mboga only, na kwa wale wanaofunga na ku meditate kuna wanaofunga kila kitu na kula hewa tuu, yaani breath, hawa wanaitwa, breathpeteriann wanafunga na kula hewa tuu!. Hawa ni ma master with full body control hakuna kuingiza kitu mwilini na hawatoi kitu mwilini wanakuwa wame stop all bodily metabolism processes hata chooni hawaendi wala perisperision process inakuwa stopped!

Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Radhani Waristo Tunawasindikiza Waislamu, Vipi Wenzetu Kwaresma, mtatusindikiza?

Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan baa na clubs hazijai, hata sisi Wakristo kwa kutambua wenzetu Waislamu wamefunga, sisi nasi tunapunguza starehe, baadhi ya bendi za muziki wa dansi zinakuwa likizo hazi perform.

Hata sisi Wakristo walaji wa kitimoto, wakati wa mwezi mtukufu tunapunguza kula mauzo yanashuka.

Hata sisi Wakristo tunatumia zile bidhaa za wale wadada zetu wa ile biashara ya usiku, tunapunguza kununua, hivyo bidhaa zinawadodea, hivyo hata wadada Kikristu hawapeleki bidhaa sokoni!

Je, Kwaresma Ina Hadhi Sawa na Ramadan?
Je wajua kuwa ni mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadan tuu ndio unao fahamika rasmi kiserikali na kitaasisi mbalimbali utasikia viongozi wa kisiasa, kiserikali, taasisi na watu mbalimbali wakifuturisha, huku nyumba za matajiri zikifurika masikini kila Ijumaa ambapo matajiri hao hutoa sadaka kwa masikini, lakini kiukweli Kwaresma ni kama haitambuliki rasmi!, sijawahi kusikia ikizungumzwa popote hivyo Kwaresma ni ipo kama ipo ipo na funga yetu sisi Wakristo kuonekana kama funga zuga!, why funga ya Wakristo haipewi Umuhimu kama funga ya Waislamu?.

Ndugu Zetu Waislamu, Mtatusindikiza?
Vipi ndugu zetu Waislamu, sisi ndugu zenu wa baba mmoja Wakristo leo tumeanza mfungo wa Kwaresma ambapo tunafunga siku 40, vipi mtatusikiziza kama sisi tunavyowasindikizaga?

Nakutakia Kwaresma Njema.

Paskali.
 
Mkuu ndoa huwa inafungwa kipindi cha kwaresima ambacho hakiruhusiwi ni sherehe tu baada ya kutoka kufunga ndoa.
Rejea ndoa ya marehemu Mrema nakumbuka walifunga ndoa kipindi kama hiki hiki cha kwaresima.
Anyway hongera Kwa nondo zako.
 
Hii kwaresma zaidi inawahusu wakatoliki, huko kwingine kama FPCT, TAG na EAGT walikuwa na mifungo yao mwezi mzima kuombea mambo yao na taifa kwa Mungu. Sasa waunganishe na hii kwaresma hizo afya zao zitaharibika kwa njaa. Kwanza kwaresma kwa wapentekoste haipo.
 
Kwanza kuna vitu umeandika vya uongo, kama hujui, na ofcourse hujui swaumu ya kiislam usiiongelee mzee acha kuwalisha watu matango pori. Umesema unatakiw et uonekane upo serious huo ni uongo. Na mengine mengi.

Alaf unasema kwaresma kufunga wakristo sio lazima kama ya waislam ambao wao ni lazima kwa muislam balekh, na alaf hata akifunga kwaresma hatakiw mtu yyt kujua. Alaf unadai itambulike? Why? Kama ni siri kwann itambulike?? Ifanyeni isiwe siri ili itambulike.

Ya waislam ni mwez mahsus umewekw kwa ajili ya kufunga ndio maana unatambulika dunia nzima, na bila shaka ww mwenyew ni shahidi wapo ambao sio waislam wanaupa heshima kwa sababu ni mwez ambao upo dhahir je ungefanywa mwezi wa siri ungepewa iyo heshima unayopewa saizi ?

Mtu anatakiw ajue upo ktk ibada ya swaum ambayo huwez kula, ukimficha kutomwambia kama umefunga atakulazimisha ule. Why umfiche umefunga?
Mtu ukimwambia mara moja tu 'mm nmefunga' harudii tena kukukaribosha chakula na anaheshim lkn je umwambie tu asante?

Alaf Uislam na Ukristo ni dini Mbili tofaut, ni Imani tofaut, kwaio kamwe huwezi kulinganisha. Uislam sio dini ya mseto. Unatak mambo ya mseto kafanye ktk vyama vya siasa, au unganeni wakristo na wahindu na wengin ila ktk ibada za kiislam hakuna mambo ya mseto. Tunashirikiana ktk mambo mengin ya kijamii kisiasa kitamafun, mila desturi, ujirani, lkn kamwe sio katika ibada. Nyinyi mna dini yenu, na sisi tuna dini yetu.
 
Mkristo anafunga saa 12 jion/saa 1 usiku mpaka kesho saa 12/saa 1 usiku ndiyo anakula hapo hajanywa maji.
Muislamu anaacha kula kuanzia saa 10 usiku mpaka saa 1 usiku. Kuanzia saa 1 usiku mpk saa 10 anakula tu.
Ratiba ya kula mchana yeye anakula saa 9 usiku au saa 10. Ila mkristo akila saa 1 usiku mpk kesho hakuna kunywa maji wala kula kitu chochote.

Muislamu huwa hafungi ila anabadilisha ratiba ya kula.
 
Na hata hamfungi hivo hayo ni maneno tu ya kujimwambafai, mkristo gan afunge hivo (kwanza nyiny si mnatakiw mfunge siku 40 bila kula wala kunywa, wewe unaweza?) Mwenzako nchi jiran juz kati aliaga dunia. Na mkrsto akijitahd sana atafunga siku 2 au 3 na hivo akibanwa sana na kiu anakunywa maji na njaa ikimbana sana anakula kidoooogo (iyo ndo funga gani?), au utaskia mtu anasema anafunga aina flan t ya chakula, hiyo pia sio funga vile vile.

hilo moja, pili, kama waislam hawafungi wanabadilisha ratiba ya kula (kama vile kwako ni kitu simple) basi na ww jaribu sio mwez mzima, Laa, jaribu wiki 1 tu, ukae kuanzia saa 10 alfajir usile kitu uend na mishe zako kama kawaida uje ule saa 1 jion jarb hata kawiki kamoja tu siku 7.

Tatu, Uislam ni dini iliyokamilika, kama ambavyo na ww utasema ukristo ni dini iliyokamilika, uislam una mafundisho yake, na pia ukristo una mafundisho yake, (ambayo kiasilimia bas wakristo weng hawayafati, kwasbb haya make sense, mfano mzuri ni huo wa kufunga 40 days bila kula chcht wala kunyw chcht, ww mwnyw ni shahid wa nafs yako wakriat wangap unaowafaham wewe wanafunga hata robo tu ya izo siku 40 ambazo ni 10 days, wangapi?

Kwaio uislam umetoa mafunzo yake jins gan wafuasi wake wafunge, na ukiristo pia umetoa mafundisho yake jinsi vp watu wake wafunge.

Kwavile ni dini 2 tofaut hatutegemei mafundisho ya hiz dini mbili yatafanana kwa namna yyt.

Sasa ukisema waislam hawafungi unakosea, wao wanafunga kwa mujib wa mafundisho yao. Wewe unatak wafunge kwa mujib wa mafundisho yenu kitu ambach nyie wenyew mnashindwa haiwezekani hiyo mzee.

Wapo sahihi kwa mujib wa mafundish ya Kiislam.

Na ww funga vyvyt vile ulivofundishw kwa mujib wa mafundisho yenu.

Maelezo ni mengi ila nahis umenielewa na kamwe hutarudia kusema waislam hawafungi wanabadilish mda wa kula.

Lkn pia sitoshangaa hata ukirudia maana binadam ubishi ni maumbile yetu.

Karibu.
 
 
Yesu ni mwana wa Mungu aliweza kufunga siku 40 bila kula, aliweza kufa na kufufuka. Wewe mwenye damu na nyama huwezi.
Ukila saa 12 jioni mpaka kesho saa 12 hautakiwi kula chochote bila maji. Na wala huwezi kumjua mkristo amefunga. Ndiyo maana unasema tunajimwambafy.

Mathayo 6:16-18
Neno: Bibilia Takatifu
Mafundisho Kuhusu Kufunga
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao.
17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu
18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni
 
Sasa hayo ni mafundisho yenu mzee ya kanisani kwenu au ya dini yenu.

Sasa mbona unataka na waislam wafunge kwa kufuata sheria zenu ?? Au waislam ni wakirisito wenzenu ? Au mna shea biblia ?

Kua na akili basi we lijamaa.

Nyie fungeni mnavofunga, waacheni waislam wafunge wanavofunga unataka wafuate biblia yako ausio.

Alaf mnajidai waislam wanataka kila mtu awe kama wao ila nyinyi mnajisahau.
Acheni kujifanya wajuaji sana wazew.
 
Kila mtu anapaswa kufuata Biblia.Hiyo ni amri.
 
Kweli kuwa uyaone! yaani wewe unaefunga kwa kujichagulia tu unajifananisha na ufungaji wa muislamu ambae ana utaratibu kamili wa kufunga!

Mungekaa kimya ingekuwa bora kwenu!
 
Hivi mkuu na wewe pia una mtazamo finyu wa kidini? coz mengi uliyo andika hapo ni uongo na biasness ya imani yako!

Pili nikurahisishie tu, imani ya dini imefungamana na kweli na uongo kulingana na hiyo imani yenyewe. Kweli ya Uislamu ni uongo kwa Ukristo, vice versa is true. With all due respect, Waislamu hatuwezi kujumuika na nyinyi katika maswala yenu kwa kuwa yanakinzana na imani yetu. The same should have been with u guys kama kweli mngekuwa na imani na utaratibu kamili katika dini yenu.
 
Funga? Watu wanajitesa bure kuacha kula wakidhani mungu anawaona kumbe ni ibada ya sanamu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…