Je, wakosoaji wa Serikali ya Tanzania ni Demagogues ama Reformers?

Je, wakosoaji wa Serikali ya Tanzania ni Demagogues ama Reformers?

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,651
Reaction score
1,129
Je, wakosoaji wa Serikali ya Tanzania ni Demagogues au Reformers?

Wakosoaji aina ya Demagogues huwa wanazungumza mabaya ya Serikali kadiri wawezavyo lakini dhamira yao kubwa ni kupata Umaarufu na nafasi za Madaraka na sio kutoa suluhisho la matatizo baada ya kupata nafasi za Madaraka

Reformers wao dhamira ya kukosoa Serikali ni kutaka kuboresha na kutoa suluhisho la matatizo

Demagogues wanaishi maisha ya kitapeli na katika maisha yao huwa hakuna maendeleo yeyote wanafanya hata katika uongozi wa ngazi yeyote waliwahi kuwa nao kuanzia Viranja wa Shule za Msingi

Jamii wanazoishi hakuna maendeleo ya aina yeyote wanayokuwa wamefanya tangu kuzaliwa kwao
Hawana maendeleo ya aina yeyote waliyowahi kufanya ili yawape credibility ya kupewa nafasi ya Uraisi wa nchi

Hawana tofauti na Matapeli au Fataki

Reformers katika maisha yao wamekuwa nuru tangu kuzaliwa kwao
Walipopewa nafasi za uongozi wa chini kuanzia Viranja wa Shule za Msingi walileta maendeleo makubwa katika Shule zao
Kila wanapoishi wanaacha alama ya maendeleo
Hawa wakiulizwa na Taifa waorodheshe maendeleo waliyoletea Wananchi katika maisha yao kabla ya kupewa nafasi ya Uraisi basi hakuna vitabu vitakavyotosha kuorodhesha maendeleo waliyofanya

Je, tukiwa kama Wananchi, tunashabikia Wapinzani Demagogues au Reformers?
Tuwe makini tusijekutapeliwa
 
Back
Top Bottom