Girland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2016
- 2,489
- 4,253
Nimejaribu kuangalia hali ya upendo Kati ya madhehebu mbalimbali ya Kikristo, hali inasikitisha. Kila dhehebu linahubiri upendo kivyake ilhali wanawabagua wenzao wa dhehebu lingine.Hali hii inasababishwa na nini Je Kristo amegawanyika?
Binafsi familia niliyotoka nimefanikiwa kuona SDA (Wasabato) VS RC (Wakatoliki),huwezi kuamini kwamba wanatumia kitabu kimoja (BIBLE). Ushakutana na vita ya WALOKOLE (TAG, EAGT, EFATHA, MAKANISA YA MANABII) VS hao wengine?
Je, Mwili wa Kristo umejengwa kwa misingi ipi? Ni Nani aliye sahihi Kati yenu? Je mmeshindwa kabisa kupendana! Hakuna wanafiki Kama Hawa watu, ukitaka kujua hawapendani binti yake achumbiwe na dini nyingine! Utaona moto wake ilhali wote ni wakristo!
Mbona ndugu zetu waislamu pamoja na madhehebu yao wana umoja na upendo? Biblia inasema mpende jirani yako kama unavyojipenda je SDA anampenda RC Kama anavyojipenda? Je, RC anampenda mwamposa Kama anavyojipenda? Je, walokole wanawapenda wasabato Kama wanavyojipenda?
Tupendane ndugu zangu hii ni amri kubwa kuliko zote.