Je, wale wanaosafiri na vilabu vya Simba na Yanga kwenda nje, hula na kulala wapi?

KASULI

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
599
Reaction score
677
Habari za jioni Watanzania wenzangu.

Kwa miaka ya hivi karibuni mpira wa Nchi yetu umechangamka sana. Vilabu vyetu Simba na Yanga si tu vinaogopeka baki pia vinacheza mpira wa kuvutia kwa viwango vyetu vya Afrika.

Suala hili limepelekea watanzania rika na jinsi tofauti kuonesha kusupport angalau kushangilia vilabu hivi viwapo nchini au nje ya nchi.

Kwa nyakati hizi Simba watakuwa ZAMBIA Yanga watakuwa RWANDA. Nimepitia Page za hizi klabu zote mbili kila upande umeandaa usafiri. Yes Usafiri wa kwenda Zambia (SIMBA) na KWENDA RWANDA (YANGA) usafiri husika ni nauli na ratiba ya safari vimewekwa.

AMBACHO BADO NATAMANI KUFAHAMU SASA.

JE, MASHABIKI AWA WATAKAO ENDA WATAKULA WAPI?
WATAKULA NINI?
WATALALA WAPI?
WATAFIKIA WAPI?

NINA IMANI HIZI SAFARI SIO MARA YA KWANZA ZINAFANYIKA WENYE UZOEFU NAOMBA MTUPE MWANGAZA. KUMBUKUMBU ZANGU ZINANIONESHA KUNA KIPINDO YANGA WALIENDA NA NDEGE YA SERIKALI AFRIKA KASIKAZINI MWAKA JANA.

NIKO INTERESTED KWENDA RWANDA BUT BEFORE NATAMANI KUPATA TARIFA KUHUSU MAMBO TAJWA HAPO JUU.
 
Mimi huwa najiulizaga


Kuna mashabiki kila inapoenda timu na wao wanaenda

Unakuta timu ipo Lindi wao wapo, baada ya siku 4 ipo Kigoma wao wapo baada ya siku tano ipo Dar wao wapo baada ya siku 6 timu ipo nje ya nchi na wao wapo


Muda mwingi huwa wanatumia kusafir na kuwa mikoani (mfano Safari ya Rwanda Hadi kurudi itachukua siku Karibu 7)

Hawa jamaa huwa hawafanyi kazi zao??? (za kiuchumi)

Hela za kusafiria kila mkoa/sehemu timu ilipo wanapata wapi??

Au ile ndio ajira yao??
 
Wafanyabiashara wale mkuu ,wengi wachuuzi wa jezi na wengine wana misheni zao si unajua mjini mipango?
 
Katika hiz Safari wapo wanaolipiwa na matajiri ambao n mashabik wa hiz timu hasa wale mashabik Lia Lia

Pili wapo ambao huwa wanafanya biashara ya jez hutembea na timu kila sehemu ambayo timu itacheza kwa hyo hawa n wafanyabiashara

Tatu wapo ambao hujipanga taratibu mdogomdogo had hufikia kiwango fulan Cha pesa na kukitumia Kama Safari mfano kwenda nje ya nchi n kama utalii fulan kwa hyo huitwa sport tourism unatumia fursa ya timu yako kwenda nje nawe kupata fursa

Kifupi kundi la pili na latatu wengi hula migahawan au hupika wenyewe na kulala kwenye basi kwa siku zote na wachache wao hulala nyumba za wagen na kula huko
 
🤣🤣🤣Wako kazini hao mkuu
 
Hapo ndio kazini kwao
 
Nakukumbusha tu Kigari ndio kule kwenye vitoto vizuri utadhani vimejiumba vyenyewe, kama wallet haisomi vizuri sikushauri utaenda kuitesa nafsi yako tu na kushindwa kufurahia ushindi wa Yanga.
 


Hotelin na kwenye migahawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…