Je walio Serikalini hawafahamu umuhimu wa internet kwa dunia ya leo?

Maleven

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2019
Posts
689
Reaction score
3,373
Internet sio anasa, internet sio jambo la option, internet ni ulimwengu kama ulivyo ulimwengu wa kifizikia,
Watu waanasoma mtandaoni
Watu wanafanya biashara mtandaoni
Watu wanaburudika mtandaoni
Watu wanasoma mtandaoni
Watu wanapata taarifa mtandaoni
Watu wanajuliana hali na kuendeleza mambo ya kijamii
Kubwa zaidi, watu wanafanya kazi mtandaoni,
Kwa sasa ajira hakuna, wapo watu wamejiaajiri kupitia Internet, inakuaje internet inachukuliwa kama ni sehemu ya ziada au option ? Hata kama watu wanakua wanatumia internet kuangalia udaku, yes ni style ya maisha yake, kwa nini serikali isione fursa hii naa kufanya mazingira rafiki? Kama ulivyo umuhimu wa kujenge barabara vivyohivyo katika kufanya mazingira mazuri ya internet , hii ni kwa Bei ya vifurishi na pia upatikanaji wake ( affordability and accessibility)

Leo hii nikiwa nimeamua kusoma graphic design mtandaoni ili nije nijiajiri, ikiwa GB 2 ni elf 10, ntahitajika kua na bei gani? Je hii ni njia ya kuwawezesha wananchi? Je TCRA hawafahamu kundi kubwa la watanzania ni wenye uwezo gani hadi waruhusu bei kisha baada ya kelele ndo wasitishe? Hakika wanachakujibu na kama hawawezi kuwahudumia wananchi waseme wasaidiwe
 
Pia wafungue na Twitter, hatuwezi teseka watu milioni zaidi ya hamsini kisa kuna mtu anaitwa Kigogo anaongea habari za uzushi. Wengine tunamambo tofauti huko twitter, kigogo mumtafute ila msinyime watu uhuru wa kupata habari na mengineyo kwa kigezo cha kigogo, it is ridiculous to block citizens in search for Kigogo, we don't meant to use VPN
 
Watu wenye akili hawapendi siasa,wajinga ndio wamekimbilia kwenye siasa unategemea nini?

Kama watu wenye akili Africa wakiendelea kuiweka kando siasa na kuamini haiwahusu tutaongozwa na wajinga mpaka ujio wa pili wa wakoloni
 
Tatizo Tanzania na Africa kwa ujumla inaongozwa na wanasiasa wanao amani maendeleo ni kumnyanyasa
Mtu na kumpatia mzigo mkubwa wa kodi
 
Watu wenye akili hawapendi siasa,wajinga ndio wamekimbilia kwenye siasa unategemea nini?

Kama watu wenye akili Africa wakiendelea kuiweka kando siasa na kuamini haiwahusu tutaongozwa na wajinga mpaka ujio wa pili wa wakoloni
Ina maana hata hawa TCRA sio professional ni political position? Mwanzoni mwa mwaka watu walilalamika kuhusu vifurushi, kulitatua hili waziri akaahidi mabadiliko , watu wakawa wapole wakitegemea kua yajayo yanafurahisha, how comes mitandao ikawasilisha vifurushi ambavyo ni hivyo zaidi ya vile vilivyopigiwa kelele na wananchi then wakapitisha? Basi ni bora wangeacha soko hurua tu kila mtandao ujiamulie, huenda kungekua na ushindani katika bei za vifurushi, kuliko kutia pua zao harafu wanaharibu zaidi
 
Wamewaambia msiingie twiter mmekuwa viburi, fungueni Sasa, mbona fb ni bure!!!
 
Ajabu sasa hawa watu ni degree holders
Na ajabu wazir wetu ni MD na anajua siku izi ktk medical kuna matumizi ya internet pia ktk mafunzo
 
Internet sio anasa, internet sio jambo la option, internet ni ulimwengu kama ulivyo ulimwengu wa kifizikia,
Watu waanasoma mtandaoni
Watu wanafanya biashara mtandaoni
Watu wanaburudika mtandaoni
Watu wanasoma mtandaoni
Watu wanapata taarifa mtandaoni
Watu wanajuliana hali na kuendeleza mambo ya kijamii
Kubwa zaidi, watu wanafanya kazi mtandaoni,
Kwa sasa ajira hakuna, wapo watu wamejiaajiri kupitia Internet, inakuaje internet inachukuliwa kama ni sehemu ya ziada au option ? Hata kama watu wanakua wanatumia internet kuangalia udaku, yes ni style ya maisha yake, kwa nini serikali isione fursa hii naa kufanya mazingira rafiki? Kama ulivyo umuhimu wa kujenge barabara vivyohivyo katika kufanya mazingira mazuri ya internet , hii ni kwa Bei ya vifurishi na pia upatikanaji wake ( affordability and accessibility)

Leo hii nikiwa nimeamua kusoma graphic design mtandaoni ili nije nijiajiri, ikiwa GB 2 ni elf 10, ntahitajika kua na bei gani? Je hii ni njia ya kuwawezesha wananchi? Je TCRA hawafahamu kundi kubwa la watanzania ni wenye uwezo gani hadi waruhusu bei kisha baada ya kelele ndo wasitishe? Hakika wanachakujibu na kama hawawezi kuwahudumia wananchi waseme wasaidiwe
Masikini akipata matako hulia mbwata, ndiyo huyo waziri wa vifurushi
 
Back
Top Bottom