Waswahili wanasemaga
1. Mkuki mtamu kwa nguruwe ila kwa binaadamu mchungu
2. Mzigo wa mwenzio begani kwako ni kama kanda la sufi
3. Mtenda akitendewa hujihisi kaonewa
4. Malipo ni hapa hapa duniani
Kwa kifupi kutendewa si masihara hata kidogo, wengi tunawatendea wenzetu lakini sisi tukitendewa inakua ngumu sana, na inasemwa ukifanya dhambi huku unacheka utaingia motoni huku unalia.
Kikubwa ukitendwa utangalia na kosa liuzito gani, na hapa kikubwa kinachotuumiza zaidi ni AIBU kwa yale yaliyotendeka, je kupenda tena huku ni kwa yuleyule ama kwa mwengine.
Kama kwa yuleyule, utapenda japo utakua bado na majeraha moyoni. TUWE WAAMINIFU KWA WAPENZI WETU