Je, wana Yanga SC Wenzangu huu Ushauri wangu hautakuwa na Tija kwa Ushindi wa Kipenati za Kupewa mara kwa mara tukicheza?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nataka niushauri Uongozi wangu wa Yanga SC kwamba tuwaombe CAF na hata TFF watuanzishe Ligi ' Maalum ' tu ambao Ushindi wake utakuwa ni wa Kupiga / Kupigiana tu Penati kwani naamini kwa Timu yetu ya Yanga SC tutafanya vyema kwakuwa tumesajili Wachezaji si wa Kucheza Soka bali ni wale tu wa Kupiga Penati za Kupewa na Waamuzi baada ya Sisi Kuwahonga au za Kiuchawi Uchawi tu.

Naamini wana Yanga SC wenzangu hapa JamiiForums mtanipa Ushirikiano wenu juu ya hili nililolishauri.
 
Hata sisi simba refa alivyoona tumebanwa sana akatusaidia kapenat kwa vile vijeba vya kimakondeni ila halikutosha kutusaidia
 

Ni ushauri na mawazo ya ''kipuuzi' kwa kuwa soka au mchezo wa mpira wa miguu una taratibu, sheria, kanuni na utamaduni wake kuhusu unavyochezwa...ukileta kejeli za ''kipuuzi' na 'utoto' kuwa CAF waanzishe ligi ya kupigiana penalti ni ushahidi mojawapo wa kwanini sisi Watanzania tuko nyuma kwenye mpira...Hatuwezi kusonga mbele ikiwa watu wataanza kujadili hoja za aina hii...Watu wazima na walio makini huwasilisha na kujadili hoja za maana na siyo kama hizi za kuomba eti ianzishwe ligi ya kupigiana penalti...
 
Wewe jamaa una ID ngapi humu?
 
Yanga haina utamaduni wa kwenda kulialia CAF au FIFA kama watani zetu. Yale mashitaka yaliyopekwa FIFA na Kaburu hadi leo hakuna jibu.
Lingine, Yanga haina kamchezo ka kupuliza sumu vyumba vya timu pinzani pale kwa Mkapa.
Hayo tuwachie jirani zetu..
 
Sasa nimegundua ni kwa nini serikali inajitahidi kuwazuia wananchi wake wasivute/wasitukie sigara aina ya bange/bangi aka Msuba aka ganja! Mtoa mada, kwa ufupi tu bangi haikupendi.
 
hahahahah... Gentamcyne tangu lini umekuwa yanga?
NB. Ushauri mzuri umeutoa na mhimu zaidi CAF waangalie namna nzuri ya kuzpiga faina timu zinazoingia kwenye mashindano kwa bonasi halafu zinaishia kutoshinda hata mechi moja kwa uwanja wa nyumbani.
 
hahahahah... Gentamcyne tangu lini umekuwa yanga?
NB. Ushauri mzuri umeutoa na mhimu zaidi CAF waangalie namna nzuri ya kuzpiga faina timu zinazoingia kwenye mashindano kwa bonasi halafu zinaishia kutoshinda hata mechi moja kwa uwanja wa nyumbani.
Mwandiko wake unamsaliti hats aje na ID 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…