Tujivunie nini kama nchi na sisi kama wananchi ?Je tujivunie hawa viongozi ambao wamejipachika madarakani bila kuchaguliwa na wanachi? Au tujivunie viongozi waliojaa viburi na wezi mafisadi wanaoendelea kutunga sheria kali kwa ajili ya wanachi wao waendelee kunufaika na rasilimali za nchi huku hizi sheria zikiwa kama waya makali kwa wananchi.
Tumeona watawala wakiandaa watoto wao kuja kichukua nafasi zao mbeleni. Je kama nchi tujivunie huu ufisadi unaofanywa na viongozi wetu? Ambao wameweka bondi kila rasilimali za nchi na kutoa elimu inaitwa elimu bure ambayo haina ubora kwa watoto wetu na wameshidwa kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya ajira za watoto watu hata BOT kuogea private bank kutoa mikopo nafuu kwa hawa vijana wanaoweza kuitimu na kufungua kampuni angalau wapate mikopo na tenda?
Tujivunie nini sisi kama wananchi au tujivunie viongozi mafisadi wanaozunguka kwa wananchi maskini wakijifanya wazalendo wakati wameshidwa kuwatoa wananchi kwenye lindi la umaskini? Tujivunie hawa viongozi walioingia madarakani kwa kumwaga damu October 29 na sasa wame mweka Tundu Lissu jela kwa kesi ya uongo na kubumba kwa kuogopa anaweza kuwasumbua wakati wa kula
Keki ya taifa au tujivunie hawa JWTZ ambao waliungana na watesi wetu kuua watoto wetu kisa kudai mabadiliko ya kikatiba Tujivunie nini au hii mikataba kama ya Dp world iliyojaaa sitofahamu? Tujivunie hawa viongozi 10% kwa kila mradi au tujivunie nini hawa ambao wameshidwa kulipa hata Wakandarasi nchi ambayo ina rasilimali lukuki bado wanachi wanaogelea kwenye umaskini wakati wachache wakinufaika na rasilimali za nchi na kuweka mihimili yote na vyombo vya dola mfukoni kweli kama nchi inaitaji tujitafakali