LGE2024 Je Wananchi wamegoma kujiandikisha Daftari uchaguzi serikali za mitaa? Na hii ni hali ilivyo baadhi ya vituo Wilaya ya Bariadi na Maswa

LGE2024 Je Wananchi wamegoma kujiandikisha Daftari uchaguzi serikali za mitaa? Na hii ni hali ilivyo baadhi ya vituo Wilaya ya Bariadi na Maswa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
www.jpg
Ni kama wananchi wamesusia hili zoezi linaloendelea kwa sasa, la kujiandikisa katika daftari la mkazi kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Swali hapa la kujiuliza Je? Wananchi wamesusia? Wananchi hawajui umuhimu wa hili zoezi? Je Wananchi wamekata tamaa kutokana na kauli mbalimbali za wanasiasa? Au Nini kimetokea.

Kwa nini nimekuja na hayo maswali? Leo ni siku ya sita tangu zoezi hili limeanza kutekelezwa, ambapo serikali ilitangaza siku 10 za uandikishwaji wa wananchi kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi huu.

Mimi nipo katika Mkoa wa Simiyu, Leo hii nimetembelea baadhi ya vituo katika Wilaya ya Bariadi na Wilaya ya Maswa.

Kwa Wilaya zote mbili, nilitembelea takribani vituo 8, kati ya vituo vyote hivyo, vinne vipo mjini na vingine vinne vipo vijijini.

Soma Pia: Uzi Maalum wa Kasoro na Rafu kwenye zoezi zima la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Hiki ndicho ambacho nimekikuta katika vituo vyote hivyo, na hapa nitazungumzia angalau vituo viwili.

Katika kituo kimoja ndani ya Wilaya moja kwenye hizo Wilaya, Makisio ya hicho kituo ambacho kipo mjini, ni kuandikisha wapiga kura 2,000 lakini mpaka leo Asubuhi walikuwa wamendikisha watu 316.

Yaani kwenye hicho kituo hata robo ya makisio walikuwa hawajafikisha, na zimebaki siku nne zoezi lifungwe. Nilipowauliza wasimamizi na mawakala wa vyama juu ya hii hali wanasema “ Hatujui kama hata wapiga kura 400 watafika kwa hali ilivyo hivi”

Kituo cha Pili, hiki sasa kipo kijijini kabisaaaaa, Nilifika kwenye hicho kituo nikakuta wameandikisha wapiga kura 120 kati ya wapiga kura 1,500 ambao wanatakiwa kuandikishwa.

Hapa nimekuta msimamizi akiwa amelala zake kwenye mti yuko usingizi chaliiiii, ilikuwa majira ya saa saba mchana, kwa siku ya leo alikuwa ameandikisha watu 5 tu toka Asubuhi.

Mawakala nilipowauliza wanasema hawajui na wao kama watafikisha watu 200. Hata wao hawajui kwa nini wananchi hawajitokezi licha ya kuwatembelea kwenye familia zao na kuwahamasisha.

Nilivyouliza kwa nini kwenye uboreshaji wa Daftari la INEC watu walijitokeza kwa wingi, Majibu ya hao mawakala ni kuwa wananchi walijitokeza kwa wingi ili kujipatia kadi ya mpiga kura, kwani kadi hiyo inafanya kazi zaidi ya kupiga kura.

Baadhi ya Mawakala wanasema kuwa inawezekana wananchi wamekata tamaa, kutokana na maneno ya viongozi wa kisiasa ambayo yamekuwa yanatoa tafsiri ya kuwa kuna njama huwa zinafanyika kwenye uchaguzi.

Unakuta wananchi wanamchagua kiongozi fulani, wanaposikia zile kauli za wanasiasa, kauli za kufanya rafu kwenye uchaguzi, wanakata tamaa, wanarejea kiongozi waliomtaka hakushinda, inaonekana alishindwa kwa hizo rafu, hivyo wanaona hakuna haja ya kujiandikisha na kwenda kupiga kura,” wakala huyo anasimulia..

Jambo jingine ambalo Mawakala hao wanasema, uhamasishaji bado hajafanyika ipasavyo hasa katika maeneo ya vijijini, kwani kuna familia ambazo hazina taarifa juu ya uwepo wa zoezi hili.

Wanasema serikali iongeze nguvu kwenye hizi siku zilizobaki katika kufikisha matangazo kwa wananchi, magari ya matangazo yafike vijijini kabisa na siyo kupita barabara kuu pekee.
 
Nimeuliza Raia wawili leo mtaani ..wanasema maisha magumu.
Wanasema Wakajiandikishe ili iwe nini.!?
 
Hivi utaratibu wa kupata kitambulisho cha upiga kura ipoje mi nimejiandikisha lakini sina kitambulisho.
 
Binafsi nimefuatwa leo na mjumbe akiwa na bodaboda.
Sijui nani kamwambia leo sikutoka.
 
"Wajiandikishe wasijiandikishe, wapige kura wasipige, ushindi uko palepale" sauti kutoka kusini.
 
Nimeuliza Raia wawili leo mtaani ..wanasema maisha magumu.
Wanasema Wakajiandikishe ili iwe nini.!?
Na kweli ukimuuliza mtu kama kajiandikisha, jibu ni "ili iwe nini!!"

Kuna muandikishaji alidai mtu alienda kujiandikisha akijua atapata kitambulisho. Sasa akaanza kujielezea kuwa kitambulisho kilipotea hivyo anataka kipya, akaambiwa huu uandikishaji hauhusiani na vitambulisho. Akainuka na kuondoka. Anaambiwa arudi ajiandikishe, akawajibu yeye shida yake kitambulisho tu, kama hawatoi basi!
 
kuna mahali mkoa fulani hadi huruma, makarani yamekaa kama mazezeta yapo yenyewe tu yanalala kwenye madawati mengine yanachati na simu zao za mikopo......sasa watu wajigambe kwamba muda wote walikuwa wanaiba kura na wataendelea kuiba kura...alafu unataka ukanipangishe foleni kujiandikisha...unataka nikagundue nini tena?.....sina cha kukifanyia utafiti, tuvumiliane tu...watakaopiga kura na kujiandisha ndio haohao waendelee kuiba mali za nchi na waendelee kutukamua tu...dawa yao inakaribia😕🙁
 
Back
Top Bottom