Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kuna baadhi ya watu ambao wanataka tuamini kuwa siku Tanzania ikichukuliwa na wapinzani basi matatizo yote ya Tanzania yatatoweka kama ukungu! Baadhi ya watu hawa, hawaishi kuonesha udhaifu wa chama tawala na serikali yake iliyoko madarakani. Ni watu hawa ambao kwao hakuna jema lolote, na hakuna kitu chochote kizuri ambacho kimewahi kufanywa na serikali iliyoko madarakani. Kwa watu hawa, ili kuweza kuona angalau kitu kizuri basi inabidi utumie darubini!!
Baadhi ya watu hawa wameonesha uwezo mkubwa wa kuonesha matatizo na udhaifu wa chama tawala ambao hahuitaji darubini kuuona kwano ni dhahiri! Ni rahisi kwao kuonesha mapungufu ya masuala ya mikataba mbalimbali, tuhuma za rushwa n.k! Ni kwa sababu hiyo basi baadhi ya watu hawa pamoja na wapiga debe wengine wa upinzani wamefikia mahali pa kudai kwa ujasiri kuwa CCM na serikali yake havijafanya lolote la maana zaidi ya kutudidimiza kimaisha.
Ukweli wa mambo ni kuwa hoja zao nyingi ni za msingi na mambo mengine ambayo wanayaonesha ni ya wazi ambayo hata mtu asiye mpinzani anaweza kuyaona! Kwa mtu yeyote anayeipenda nchi yetu hatuna budi kuwashukuru watu hao kwa moyo wao wa kizalendo na kujituma kufichua maovu na ufisadi! Siyo jukumu la watu hao peke yao na vyama vyao kuonesha ubaya, upotofu, na ubovu wa serikali iliyoko madarakani! Si vibaya kabisa kwa wao kwa kutumia mwanga kama wa kurunzi kuangazia umma na kuonesha kuwa baadhi ya viongozi au wafanyakazi wa serikali ni wabadhirifu, wanatumia madaraka yao vibaya, na baadhi yao wamefanya vitendo ambavyo vinapakana kabisa na usaliti kama siyo uhaini dhidi ya jamhuri yetu.
Viongozi hawa walioko upinzani na wapambe wao wamejitahidi miaka nenda rudi tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi kuiamsha Tanzania ili wananchi waelewe kuwa kuna chaguo jingine na kuna chama mbadala wa CCM. Walijaribu kwa mafanikio makubwa kwenye uchaguzi wa 1995 na kutokana na mvuto wa mmoja wa wapinzani hao aliyewahi kuwa madarakani basi watu waliamua kuachana na CCM na kujiunga na upinzani wakitumaini kuwa hapo "wamefika nyumbani" kwani CCM imewachosha! Lakini katika chaguzi mbili zilizofuata baadaye (2000 na 2005) vyama hivi vimeendelea kufanya vibaya licha ya majina yao na itikadi zao kueleka zaidi!
Pamoja na kudidimia kwa vyama hivyo kwenye sanduku la kura, viongozi wao bado wanapita kunadi sera zao wakiangazia udhaifu na ubovu wa CCM kuwa ni sababu ya wananchi kuwaamini kuwa wapinzani ndio mbadala wa uhakika wa chama tawala, na hivyo wananchi waanze kuwaamini kwa kuwapa madaraka!
Swali kubwa na la msingi ambalo kila Mtanzania hana budi kujibu ni kuwa, je wapinzani wakipewa madaraka ya nchi leo hii (siyo kupewa kama hisani bali kutwaa kwa nguvu ya kura) matatizo ya Tanzania yatatoweka ghafla? Je wapinzain wakiwa Ikulu hospitali zetu zote zitakuwa za kisasa, wanafunzi wote watakwenda shule, mishahara italipwa kwa wakati n.k n.k? Je wapinzani wakitwaa madaraka ina maana umasikini wa Tanzania utatoweka ndani ya mwaka mmoja?
Kama mifano ya wapinzani kuchukua madaraka katika nchi jirani inaonesha lolote, basi mtu yeyote mwenye akili timamu ambaye anadhania kuwa endapo wapinzani watachukua madaraka basi maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa ahuei na yatabadilika kwa ghafla mtu huyo adhanie tena! Ni mabadiliko gani ya kimaisha wananchi wa Kenya wameyapata baada ya NARC kuingia madarakani? Vipi kule malawi baada ya chama cha MDC kuingia madarakani watu wa Bulawayo, Lilongwe, Blantyre, na Karonga maisha yao yamebadilika vipi? Je wapinzani walipochukua madakaraka huko Zambia, maisha ya watu wa Lusaka, Copper Belt, na Capri Mposhi yamebadilika vipi?
Wapinzani wameendelea kudai kuwa CCM imejaa watu wafisadi wasioipenda nchi yao, wenye kutumia madaraka yao vibaya, je wao wakiingia madarakani na kujaza nafasi zote za utawala kuanzia Rais hadi mwenyekiti wa kijiji watatuhakikishia vipi kuwa hakuna mtu kati mamia ya watumishi hao atakayekula rushwa au kutumia madaraka yake vibaya? Je tuna uhakika gani kuwa vyama vya upinzani vitaweza kumsimamia kila polisi, kila mwalimu, kila meneja, kila Mkurugenzi, kila mwenyekiti wa bodi n.k na kuhakikisha hakuna hata mmoja wao atakayemziba raia kibao hadharani au ambaye atafyatua bunduki yake na kumlipua mpiga debe?
Kama kweli wapinzani wataahidi kufanya haya yote na kutokosea kabisa, kutoharibu hata mara moja, na wakiahidi kuondoa kero zote na matatizo yote yanayoikabili Tanzania huku viongozi wake wote (Rais hadi mwenyekiti kata wa kijiji cha Mkata) wakiwa waadilifu wasiomezwa na ulafi, wasiolewa madaraka wakitumikia nchi yao kwa mapenzi makubwa, basi Tanzania lazima iwachague wapinzani!! Kwani kwenye vyama vya upinzani hakuna binadamu wote ni Malaika, na wote hawajali matumbo yao wala mifuko yao!! Ni katika vyama hivyo yule Musa Nabii yupo, na ni yeye ndiye atakayetutoa utumwani!! Kama kweli vyama vya upinzani vitafanya mambo hayo yote basi ndugu zangu Watanzania, inawezekana mkombozi yupo katikati yetu na hatujamgundua!!
Kwa kuelewa hulka za binadamu bila kujali itikadi zao na mitazamo yao kutegemea wapinzani kuwa wakombozi wa Tanzania kwa vile tu ni Watanzania wanaotoka Chadema, TLP, CUF, NCCR, au vyama vingine ni mategemeo ambayo yatapeperuka kama unyasi upeperushwavyo na upepo, ni kama umande unavyopukutika kwenye majani asubuhi inapofika! Manabii wa upinzani wako wapi watutabirie?