Mwanasiasa,
Nasubiri majibu ya hoja nyingine kabla sijazama zaidi ktk upimaji wangu.
hata hivyo, samahani mkuu nitapenda kufahamu hiyo KATIBA ambayo itawashirikisha wananchi inaundwa vipi? (process yake)..
Pili, hili swala la rais wa Zanzibar bado zito sana kwangu! nakuwa mzito kuamini kuwa Sharrif hamad akichukua urais wa Zanzibar chini ya CUF na bara iwe chini ya CCM, kutakuwepo na mfarakano mkubwa zaidi.
Hofu yangu kubwa ni kuwa vyama hivi vyote vinapigiwa kura sio kwa sababu ya sera zao (CCM) isipokuwa nani kasimamishwa. Na kibaya zaidi ni kwamba wananchi wepesi wa kusamehe chama makosa yake inapofikia kuwepo kwa utenganishi wa rangi.
Mwanasiasa, kumbuka tu sisi ni waafrika... tuna vijimila vibaya ambavyo haviwezi kuondoka kirahisi kwa hii demokrasia ya wazungu. Hata kama ndugu yako ni jambazi, siku akikamatwa mshikaji utamtetea kwa kila hali na pengine kuficha hata silaha zake!.. kwetu damu nzito sana na hakuna demokrasia inayoweza kuvunja mila hii kirahisi.. na ndio hapo by extension tunafika hadi kwenye makabila!..sielewi hayo marekebisho ya Katiba yamezingatia kwa kiasi gani mazingira yetu ama ndio sifa za Mzindakaya kuwa na ng'ombe wa kizungu 3,000!
Anyway, yote tisa, kumi hamuwezi kuwa na mabadiliko yoyote ktk katiba bila kuchukua kwanza ushindi bungeni!..
Nasubiri majibu ya hoja nyinginezo
Mkandara: niliahidi kukujibu swali lako kuhusu mchakato (process) wa kutunga katiba inayokubalika na kuheshimika kwa wananchi wote. Wataalamu wameanishwa michakato mbalimbali ya kutunga katiba. Mimi, na nafikiri CHADEMA kama chama pia, ninakubaliana na ule mchakato uliotolewa na Profesa Issa Shivji. Mchakato huu una hatua 4 zifuatazo:
1) Kutoa vikwazo vya kisheria vya kuruhusiwa mfumo wa vyama vingi kufanya kazi-hatua hii ilikwishatekelezwa
2) Kuruhusu uundwaji wa vyama na taasisi za kiraia-hatua hii nayo kwa kiasi fulani ilishatekelezwa
3)Mkutano wa Kitaifa: Hii ni hatua ya kisiasa katika kutafuta makubaliano kuhusu mambo muhimu ya kuingizwa katika katiba. Mkutano huu utajumuisha wa wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wananchi yakiwemo: vyama vya wakulima, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wavuvi, wafanyabishara, vyama vya siasa, taasisi za kidini, raia mashuhuri, wasomi, n.k. Kazi kubwa ya mkutano huu itakuwa kupata makubaliana juu ya mambo na misingi muhimu ya kuingiza katika katiba
4) Tume ya kuandika katiba: Baada ya kukubaliana misingi ya katiba, mkutano wa kitaifa utateua wajumbe kadhaa wenye fani mbalimbali watakaopitia yale yaliyokubaliwa katika mkutano wa kitaifa na kuyaandika katika lugha ya kikatiba. Hatua hii itatoa juzuu ya kwanza ya katiba
5) Juzu ya kwanza ya katiba itarudishwa kwa wananchi kwa njia ya kura ya maoni ili wananchi waikubali hiyo juzuu kuwa katiba. Kura ya maoni ikikamilika na kama wananchi wataikubali hiyo juzuu ya kwanza, basi hatua ya mwisho inafuta, ambayo ni:
6) Bunge kukaa kama bunge maalumu kwa ajili ya kupitisha katiba (Constituent Assembly). Hiyo juzuu ikitika hapa imepitishwa tunakuwa na katiba ya nchi.
Hizi ni hatua muhimu sana katika kupata katiba ambayo ni 'fair, just and respectable'.
Nitaendelea baada ya maoni yako na wengine.