Je, wapinzani ni wakombozi?

TATIZO SIO WAPINZANI

  • TANZANIA TUNAHITAJI BUNGE BORA ILI TUWE NA GOOD GOVERNMENT BILA BUNGE ZURI HAMNA CHOCHOTE TUTAKACHOACHIEVE HATA WAPINZANI WASHINDE.

    PILI TATIZO LA TANZANIA SIO CHAMA ILA NI MITAZAMO YETU, TUNAPENDA SHORT CART NA HATUANGALII MBALI, SULUHISHO LA HILI SWALA NI KUWA NA VIJANA WENGINE MACHACHARI 15 TU BUNGENI AMBAO WAKO TAYARI KUIONA NCHI INAKWENDA MBELE

    MWISHO NYERERE ALIACHIEVE UHURU NA SISI TUTAWWAAMBIA WAJUKUU WETU TUMEIFANYIA NINI TANZANIA?
 
Pengine swali lingekuwa "Hivi kuendelea kuiweka CCM madarakani tunatazamia kupata Maendeleo au tunajihakikishia kufisadiwa (kuliwa)"
 

Leokweli,
Umeweka masuala mazuri ambayo yanaweza kupanua mjadala. Lakini kama ungeyatumia mawazo yako katika kuchakatua chama gani kitatufaa kwa kutilia maanani hayo uliyoshauri ingekuwa vema sana.




______________________
 
Leokweli,
Umeweka masuala mazuri ambayo yanaweza kupanua mjadala. Lakini kama ungeyatumia mawazo yako katika kuchakatua chama gani kitatufaa kwa kutilia maanani hayo uliyoshauri ingekuwa vema sana.




______________________

Are you in the process of building trust after you and your collegue Chinga aka Mtalii aka Mzee Kifimbo aka Mswahili lost it big time? Lakini kumbuka, hata ujipendekeze vipi- maandishi yako ya awali ya kuchochea ukabila na ubaguzi pamoja na kuchonganisha upinzani yamo humu. Tutakuwa tunakukumbusha tu nukuu zako. Kwenye msafara wa mamba na kenge wapo wallah!

Asha
 

Asha kupindisha mambo. Do you think you are 100% perfect? Discuss the topic, if you think you are off, go and start another thread period! Kweli nyani hajioni mkiani, wewe je ni mamba au kenge kwenye hili?
 
M/Kijiji safi sana kwa uchambuzi wako. Ni vizuri watu wakajifunza kutojadili swali amabao majibu wanayo tayari .
Tunamaribisha atupe hizo za Mwandosya.
 
Maendeleo Bora yanaletwa na siasa safi na viongozi Bora,Kama wapinzania,nazungumzia Chama kitakuwa na Sera Bora,siasa safi na viongozi bora basi nchi itaongozwa kwa kuleta maendeleo na tija kwa ufanisi wa khali ya juu.

ila kwa kusema Upinzani,kwa maana ya kupinga kinachofanywa na Mpinzani wako,huko hakuleti maendeleo.
 
TATIZO SIO WAPINZANI

  • TANZANIA TUNAHITAJI BUNGE BORA ILI TUWE NA GOOD GOVERNMENT BILA BUNGE ZURI HAMNA CHOCHOTE TUTAKACHOACHIEVE HATA WAPINZANI WASHINDE.

Bunge bora haliwezi kupatikana kama watanzania hawajui kiwango cha ubora kinachohitajika. Elimu ya umuhimu wa kupiga kura na kumpigia kura nani na kwa nini bado inahitajika.

Kikachokosekana sasa ni uchungu wa umaskini ambao sisiemu wao wamejikita kwa umaskini wa mtu mmoja mmoja (chukua chako mapema) ndio maana ufisadi umejikita hadi kwa mtendaji kata na balozi wa nyumba kumi.


Vyama vya upinzani vijitahidi vipate wabunge wengi ili waweze kuleta changamoto zaidi kwenye bunge e.g kubadilisha katiba, kuiwajibisha serikali na mambo kama hayo ambayo yanakosekana na kurudisha nyuma maendeleo.
Inashangaza sana kuona wananchi wana hali duni lkn bado hawajaamka toka usingizini kuhoji kwa nini waishi katika maisha hayo na ni nani anayesababisha waishi kwenye dimbwi la umaskini. kisa labda hakuna aliyewaamsha.


Maendeleo ya nchi hii hayategemei ni chama, bali ni nafsi safi y/za k/viongozi watakao kuwa madarakani. Hao wapinzani nao hatuna uhakika nao, inaweza ikawa yale yale wakipata madaraka wanatugeuka. Wapi Mzindakaya na G55?

Nadhani somo civics, GS na DS hayapewi umuhimu au mtaala wake haujitoshelezi ndio maana hatupati viongozi accountable.
 
Karibu sana Ndibalema,

Haya hebu tuwekee huo "ukibaraka" wa Dr. Slaa "hazarani" na tuhuma zako dhidi ya Prof. Mwandosya la sivyo tutakuwa na kila haki ya kukuita "Mpika Majungu".
 
Interesting comments, but we must go to broader issues. When we talk about CCM, we will not be be fair to brand the whole party as a corrupt or evil institution, as some of members are trying to have us believe. So far pamoja na kuwa baadhi ya watu wanataka credit zote za vita dhidi ya ufisadi ziende kwa Dr Slaa(they may be right), sioni kama itakuwa haki kuwa dicredit watu walio ndani ya CCM wanaoipigania nchi kwa nguvu hata kuhatarisha maisha yao, kuna wengi tu wengine hata hawasemi kitu lakini vitendo vyao vinaonekana.
Nchi haiongozwi na mtu mmoja, inaongozwa na timu, pamoja na kuwa kiongozi wa juu ndio mhimili wa timu nzima, haina maana kuwa yeye as an individual ni "be end and end all". Babu JKN alisema kiti kile si lele mama, na wanao kitafuta kwa nguvu ujue kuna wanalotafuta.
Kama unavyojua CCM mtandao waliitafuta Ikulu kwa dirty games nyingi wameipata na tumeona walivyotutenda.
This is 2008, not 2010 ikifika katikati ya 2010 tutajua nani atagombea na nani hatagombea urais, au nani atafaa na nani hatafaa. Kuna watu walikuja hapa wakawa wanasema EL atakuwa rais 2015, lakini ona sasa EL aliko, itakuwa kichekesho sana kama ata bounce back kama Zuma. So let us wait and see in 2010.
 
Karibu sana Ndibalema,

Haya hebu tuwekee huo "ukibaraka" wa Dr. Slaa "hazarani" na tuhuma zako dhidi ya Prof. Mwandosya la sivyo tutakuwa na kila haki ya kukuita "Mpika Majungu".

Inaonekana Ndibalema hana data alikuwa anajaribu tu. Mafisadi wenyewe hakuweza kupata kitu kuhusu Dr. Slaa, tangiwa wakati huo, Je zitapatikana leo?

Hakuna nchi iliyoweza kupata maendeleo bila kuchukia mfumo walionao. Watanzania kwa mfumo tulionao, Sheria za 47 zilizomtoa mkoloni, Chama kinachoongoza karibia miaka 47, nk hatuwezi kupata maendeleo.Kwanza mifumo yenyewe imechoka, chama tawala kimechoka, watawala wamechoka, watanzania wanaotawaliwa ndo usiseme-nenda vijijini nk.

Maendeleo hatuwezi kuyapata bila kukaa chini kuangalia vikwazo vinavyosababisha tusiendelee na kuvitafutia ufumbuzi.

Leo hii kuna watu kibao ktk ofisi tunazozitegemea ziwe chachu ya maendeleo ukiwauliza wanafanya nini ofisini hata hawezi kukwambia kwa siku amefanya nini.

Tuna viongozi ambao hata hawajui kwa nini hatuendelei, tu masikini, sasa kama hata wanaotuongoza hawajajua kwa nini hatuendelei tunaweza kuendelea kweli?

Hili tupate maendeleo kwa mwendo tulio nao inatakiwa tubinafsishe kazi za serikali zetu na serikali kwa ujumla. Vinginevyo tubadili sheria na katiba zetu zielekee katika kutuletea maendeleo.

Leo hii ktk nchi zetu Kakindo nikipata madaraka kitu cha kwanza ni kuhakikisha ndugu zangu aka wapambe wote wawe wanaqualify wasiwewanaqualify ni kuwapa tunauita ulaji-kombolea.

Je kama kazi ni kupeana ulaji, huo ulaji unapatikana wapi? Ni sehemu mojawapo ya raslimali zinazotakiwa kuleta maendeleo au nini?


 

Mama
Hapo umemwaga pointi kubwa sana,nami nilikuwa na mawazo kama hayo.
Tunahitaji watu walio na uzalendo,waadilifu,wanaoweza kushirikisha nguvu zao na za wapiga kura na yakazaliwa maisha bora kwa kila M TZ.

Tindikali na nyongo zote lazima zichanganyike ndipo upate chumvi na maji na ukichanganya gesi ya oksijeni na ile ya haidrojeni ndipo unapata maji.Wakichanganyikana humo kwa asilimia kubwa ndani ya mjengo sisiem na wapinzani basi matokeo yake ni kasi kubwa ya kuleta haya maisha bora tuliyosubiri mda mrefu.

Nina maana kuna watu waadilifu sisiem na kuna watu waadilifu upinzani,sasa hapa tukija na mawazo ya chama kuna wengine ktk vyama vingine hatutawatendea haki ya kutumia talent zao ktk uongozi
 
Mdogo wangu Ndebalema,
Pole sana kwa yote yanayosononesha nafsi yako, ila kwa sasa naomba tuendelee kuweka matumaini yetu kwa JK, usisahau kuwa Kikwete bado analipenda Taifa letu, ni vijimambo tu vinavyotukela, kwelikweli,pia usisahau hawa jamaa walimsaidia kumueka hapo alipo,jk bado ni mzalendo na anaipenda Tanzania, asingekuwa yeye leo hii waandishi wasingekuwa na uhuru kama waliokuwa nao leo.

Tumpe muda mwingine.
 
Ndibalema
You have come up with a dead strategy.Kwani mkiwa mnatumwa kuja ku gauge upeopo huwa hawawapi na strategies makini ?Maana unaishia kuumbuka .Umesha test upepo nadhani umesha jua kwamba watu wako makini .Kawaambie kama hawajasoma kwamba hapa pagumu mjaribu Majira na Rai .
 

Mhh Kikwete analipenda taifa letu kwenye midst ya richmonduli na buzwagi? inaonekana kuna tafsiri mpya ya kupenda umeipata!
 

Kulipenda Taifa na kuwa na uwezo finyu kama Rais ni vitu viwili mbali mbali.
 
WAPINZANI WATAWEZA KWASABABU WANAJUA KUWA WASIPOFANYA HIVYO CCM ITARUDI MADARAKANI!TUNATAKA UPINZANI WACHUKUE NCHI ILI VYAMA VIANZE KUWA NA WIVU KATI YAO!WIVU WA KUWA NI NANI MWENYE KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO ZAIDI YA MWINGINE!THATS WHAT WE NEED NOW PEOPLE!
 

Ungejadili ishu na kuacha kumsahmbulia mtoa hoja, nafikiri ingesaidia zadi.


_________________________
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…