________________________________________
Ni ukweli uliowazi kabisa kuwa idadi ya wanojutia uamuzi wao wa kuipigia kura CCM katika chaguzi zilizopita hasa ule wa mwaka 2005 inaongezeka siku hadi siku.
Wanchi sasa wanazidi kupata mateso badala ya maisha bora waliyoahidiwa na viongozi wa CCM.
Mambo kama Ufisadi, Kulindana, Majigambo na nyodo za viongozi, Ahadi hewa, na 'uchafu' kibao ambao unaendelea kufanywa na viongozi wa serikali ya CCM ni miongoni mwa mambo yanayo wachefua Watanzania.
Ukibahatika kukaa kwenye vijiwe utawasikia hata wale ambao kipindi kile waliokuwa huwaelezi kitu mbele ya JK wakimlaani huyu mtu na CCM yake, bila shaka sasa kwa mbaali wanaanza 'kuipata picha'.
Imefikia mahali sasa watu wanajiuliza ' Hivi huyu jamaa kuna watu wanamwongoza au?' maana haiingii akilini kwa mfano 'Jitu' limefilisi nchi, raia wema wanakueleza eti unawajibu 'Mwacheni mzee apumzike' Huyu jamaa alipitia jeshi kweli??
Lakini mbali na yote hayo, Swali linalobaki vichwani mwa wengi ni kwamba, Je, 2010 Tukiamua kuwapitisha Wapinzani kwa kishindo watatuletea maendeleo na maisha bora ambayo serikali ya CCM ilishindwa?
Je, Hakutokuwa na mafisadi kama hawa tunaowaona leo?
Swali lingine ni je kuna mgombea yeyote kati ya hawa tunaowajua kutoka upinzani atakua 'strong' ambaye hatokubali kumlinda mtu kama afanyavyo JK?
Pengine watu wangependa kujua zaidi iwapo kama Hivi 'vijisenti' vya ruzuku tu tayari watu wa Makao makuu wanajipendelea na kusahau wa mikoani, je Wakipewa Wizara si patakua hapakaliki?
Ingawa katika kambi ya upinzani kuna 'hazina' ya uchumi ambaye si mwingine bali ni Profesa Ibrahim Lipumba lakini bado lazima tujiulize je, maamuzi yake mara baada ya kufika Ikulu hayatakua ya kibabe kama maprofesa wengine wa hapa nchini na Duniani kwa ujumla? inasemekana kuwa hakuna rais Profesa katika nchi zote duniani.
Mfano rahisi ni Maprofesa ambao ni wakuu wa vyuo na taasisi mbali mbali hapa nchini achilia mbali Prof. Mwandosya ambaye analazimisha raia wa kigeni kuchangie maendeleo ya jimbo lake vinginevyo anatengenezea 'skendo' ili watimuliwe nchini.
Hawa jamaa(Maprofesa) huwa wanajiona hawakosei kwa sababu Elimu yao ni kubwa kuliko elimu zote. Kuna rafiki yangu hivi karibuni alimtaja Dr. Slaa kuwa anafaa. Ningenda kumwahidi yeye na wengine wote kuwa hivi karibuni kwa kupitia humu humu JF nitaweka hazarani 'Ukibaraka' wa Dr.Slaa.
Pia yupo huyu Freeman Mbowe ambaye bila kificho huyu jamaa ni mfanyabiashara mkubwa tu hapa nchini, Je ataweza kujizuia kufanya biashara akiwa Ikulu?
Hata hivyo simaanishi kuwa
Tusiwape Wapinzani Kura bali pia sio mbaya tukajiuliza maswali ambayo ni muhimu kupata majibu yake kabla ya kufanya maamuzi mazito.
Mwisho ningependa kuwasalimu jamaa zangu wa PPT-MAENDELEO, TADEA, DP, JAHAZI na wengine ambao tunawasikia kipindi cha uchaguzi mkuu tu. Amkeni Jamani wakati ndo huu CCM wameshindwa kazi, I LOVE TAZANIA, I HATE MAFISADI.