Bikirembwe
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 250
- 7
Point noted... nadhani kuna watu kuchanganya elimu na mtu kuweza kuongoza. Siyo kila mwenye shahada ya Udaktari atakuwa kiongozi mzuri kwa sababu tu ya shahada yake. Hivi Rais Lula wa Brazili ana shahada ngapi za Udaktari na amesoma vyuo gani vikuu hadi akaupata urais wa moja ya nchi zinazoendelea kwa haraka?
Naamini kabisa wapinzani wana uwezo mkubwa tu wa kutawala na kuongoza kwa ufanisi mkubwa iwapo watanzania watawapa ridhaa ya kuiongoza nchi.
Si wapinzani wala CCM watakaoweza kuiendesha nchi vyema, ni mwamko wa wananchi wenyewe.
Viongozi wa kisiasa wa upinzani wakipewa nchi 2010 wanaweza kuanza na euphoria ya change, lakini wakajikuta na challenge nyingi sana hata kama waki u combat ufisadi, which itself is questionable, but due to the gross CCM record lets say they will be able to do better than CCM on that end, then what?
Kazi ya kuiendeleza nchi masikini kama Tanzania si lelemama andd before you know it people may deem the task insurmountable and become fatigued, and slip back into ufisadi.It happenned with Nyerere, Mwinyi hardly made an attempt, it happenned with Mkapa and now we are witnessing a Kikwete fiasco.
What we should focus on is institutions that will ensure checks and balances, good governance, civic education, freedom of the press and economic development for all.Once we have these institutions, the people will not wait for the rulers to hand good governance to them, the people will demand good government even before the rulers are sworn in.
If we focus on which party may do a better job but leave the presidency too powerful, the constitution parctically a one party charade and an uneducated mass, even a Gandhi will be tempted to take us for a ride.
Unless everybody in the opposition is a sage of the level of walii and nabii, they can only do so much without the stick to enforce some legal code.It has been said that the carrot of moral high ground and some Mohammed Ibrahim Award is too low compared to the temptations a ruling party "access granted" status can give.
Focus ya kwanza ni kukitoa madarakani chama kilichoshindwa kuongoza!
Wazambia walisema hivyo hivyo, na kumuweka Chiluba
Wakenya walisema hivyo hivyo, na kumuweka Kibaki
Tumeona matokeo.
Sheria zile zile za treason mkoloni alizotumia kuwashtaki kina Nyerere ndiyo hizo hizo kina Nyerere walizitumia kuwakandamiza wapinzani.
Ndiyo maana nasema inabidi tu focus kwenye institutions.
wazimbabwe na wanorth korea wamemwacha mugabe na kim madarakani na tumeona matokeo yake.
wazimbabwe na wanorth korea wamemwacha mugabe na kim madarakani na tumeona matokeo yake.
Tatizo ni kwamba una interpret ninachokisema in a rather simplistic way, kwamba nina advocate kuacha regimes madarakani.Hasha.
Ninachosema ni kuwa hata kama tukibadili chama tawala leo lakini kama hatuna deeper institutional changes basi tutajikuta tunarudi square one kirahisi tu.Tena mtu mwingine anaweza kuleta argument kuwa hivyo vyama vya upinzani kwa sababu havijaweza kujijenga sana vikawa rather easily manipulated na watu influential ndani ya vyama.
Vyama vijengwe zaidi, networks ziimarishwe, institutions ziwezeshwe, CCM iondolewe.Hapo vyama vitakuwa havina choice bali kuleta maendeleo.Lakini ukitoa mwanya wa longolongo ni human nature kuanza ku backslide na kuja na vi slogan vitakavyokuwa version mpya ya "kasi mpya..." or some bs like that.
They say a man is only as honest as his options, let us not give any options for abuse and have a guaranteed good government instead of playing Russian Roulette with our country.
Mkuu ninakuelewa vizuri sana na ninapata shule toka kwenye posting zako. Kinachogomba hapa ni kuongezea alichosema Ngabu hapo juu kuwa, ccm hawako tayari kubadili hizo institutions na wamesema hili on our faces.
Sasa je, tuwaache kwa kuwaangalia waliiofeli au tufanye our own way. Mimi ninapinga kumaintain status quo.
Nani atajenga hivyo vyama mkuu Pundit? CCM wanamiliki kila kitu hapo Tanzania na najua unaelewa hili. Wanapata mabilioni ya pesa za wizi toka bank kuu na institutions zingine. Hiyo ya kujenga vyama wakati sisiemu wanauza na kufilisi nchi ni excuse ambayo wengine tumeikataa!
True dat!
CCM needs to go...wanayoyafanya ni mabaya mno kiasi kwamba tukiwachagua tena tutakuwa wanafiki. Mpaka sasa imeshadhihirika kuwa hawako interested na kubadilika au kubadilisha chochote including hizo "institutions"....So why keep them? Makes no sense.
.....
Inabidi tuwe honest with ourselves na tusitafute majibu rahisi kwa maswali magumu.Matatizo yetu ni deeper than regime change, we need institutional change and to me institutional change needs to happen either simultaneously with regime change or before regime change.Otherwise mtu akishashika power kwa mara ya kwanza pale inakuwa vigumu sana kumshawishi afanye mabadiliko.
Mambo ya kulazimisha watu wasiotaka mabadiliko yamepitwa na wakati. Walikuwa na muda mwingi sana wa kubadilika lakini hawakutaka. Sasa hapo mimi sioni alternative nyingine zaidi ya kuwaondoa hao watu na kuweka wengine. Hao wengine watakaowekwa na wenyewe wakileta za kuleta tunawaondoa. Nchi ni ya kwetu sisi wananchi and we get to decide who leads us. Hakuna waliozaliwa kututawala. Nawaambia sisi wananchi tukiwa wakali hata viongozi wetu nao watakuwa makini maana watajua hatuna mchezo wala uvumilivu wa mambo ya kijinga. Kama mtu huwezi kazi tuliyokupa basi katafute nyingine unayoiweza. Hili linawezekana kabisa.
________________________________________
Ni ukweli uliowazi kabisa kuwa idadi ya wanojutia uamuzi wao wa kuipigia kura CCM katika chaguzi zilizopita hasa ule wa mwaka 2005 inaongezeka siku hadi siku.
Wanchi sasa wanazidi kupata mateso badala ya maisha bora waliyoahidiwa na viongozi wa CCM.
Mambo kama Ufisadi, Kulindana, Majigambo na nyodo za viongozi, Ahadi hewa, na 'uchafu' kibao ambao unaendelea kufanywa na viongozi wa serikali ya CCM ni miongoni mwa mambo yanayo wachefua Watanzania.
Ukibahatika kukaa kwenye vijiwe utawasikia hata wale ambao kipindi kile waliokuwa huwaelezi kitu mbele ya JK wakimlaani huyu mtu na CCM yake, bila shaka sasa kwa mbaali wanaanza 'kuipata picha'.
Imefikia mahali sasa watu wanajiuliza ' Hivi huyu jamaa kuna watu wanamwongoza au?' maana haiingii akilini kwa mfano 'Jitu' limefilisi nchi, raia wema wanakueleza eti unawajibu 'Mwacheni mzee apumzike' Huyu jamaa alipitia jeshi kweli??
Lakini mbali na yote hayo, Swali linalobaki vichwani mwa wengi ni kwamba, Je, 2010 Tukiamua kuwapitisha Wapinzani kwa kishindo watatuletea maendeleo na maisha bora ambayo serikali ya CCM ilishindwa?
Je, Hakutokuwa na mafisadi kama hawa tunaowaona leo?
Swali lingine ni je kuna mgombea yeyote kati ya hawa tunaowajua kutoka upinzani atakua 'strong' ambaye hatokubali kumlinda mtu kama afanyavyo JK?
Pengine watu wangependa kujua zaidi iwapo kama Hivi 'vijisenti' vya ruzuku tu tayari watu wa Makao makuu wanajipendelea na kusahau wa mikoani, je Wakipewa Wizara si patakua hapakaliki?
Ingawa katika kambi ya upinzani kuna 'hazina' ya uchumi ambaye si mwingine bali ni Profesa Ibrahim Lipumba lakini bado lazima tujiulize je, maamuzi yake mara baada ya kufika Ikulu hayatakua ya kibabe kama maprofesa wengine wa hapa nchini na Duniani kwa ujumla? inasemekana kuwa hakuna rais Profesa katika nchi zote duniani.
Mfano rahisi ni Maprofesa ambao ni wakuu wa vyuo na taasisi mbali mbali hapa nchini achilia mbali Prof. Mwandosya ambaye analazimisha raia wa kigeni kuchangie maendeleo ya jimbo lake vinginevyo anatengenezea 'skendo' ili watimuliwe nchini.
Hawa jamaa(Maprofesa) huwa wanajiona hawakosei kwa sababu Elimu yao ni kubwa kuliko elimu zote. Kuna rafiki yangu hivi karibuni alimtaja Dr. Slaa kuwa anafaa. Ningenda kumwahidi yeye na wengine wote kuwa hivi karibuni kwa kupitia humu humu JF nitaweka hazarani 'Ukibaraka' wa Dr.Slaa.
Pia yupo huyu Freeman Mbowe ambaye bila kificho huyu jamaa ni mfanyabiashara mkubwa tu hapa nchini, Je ataweza kujizuia kufanya biashara akiwa Ikulu?
Hata hivyo simaanishi kuwa
Tusiwape Wapinzani Kura bali pia sio mbaya tukajiuliza maswali ambayo ni muhimu kupata majibu yake kabla ya kufanya maamuzi mazito.
Mwisho ningependa kuwasalimu jamaa zangu wa PPT-MAENDELEO, TADEA, DP, JAHAZI na wengine ambao tunawasikia kipindi cha uchaguzi mkuu tu. Amkeni Jamani wakati ndo huu CCM wameshindwa kazi, I LOVE TAZANIA, I HATE MAFISADI.