Je, wapinzani ni wakombozi?



Huyu ndiyo Mzee Mwanakijiji ninayemjua mimi. Mwingine anakuwaga photocopy. Good points. Of course you need to be careful in the presentation, lest they easily backfire!
 
Mwanasiasa, naanza kuwaogopa humu... Wapinzani hawasemwi wala hawakosolewi!
 
Makwaia akana uteuzi CHAUSTA
 
Nianze na kumpongeza Mzee wa Je, tutafika? kwa uwazi wake. Utadhani Mzee Makwaia na Mzee Mwanakijiji ni pacha!


Mzee MKJJ, hoja karibu zote ulizoziainisha hapo juu/nyuma kuhusu nini wapinzani wafanye, si mpya, si hapa tu Tanzania, bali pia katika nchi jirani zetu kama Kenya, Malawi na Zambia. Nakumbuka wewe binafsi uliwahi kudadisi humu ndani kuwa wapinzani katika nchi hizo tajwa walipochukua madaraka kutoka kwenye vyama tawala wameleta mabadiliko gani ya kujivunia?

NARC waliahidi Katiba mpya ndani ya siku 100; tena kwa Kenya mchakato wa kuandika katiba mpya ulikuwa ushaanza wakati ule wa kina Prof Ghai; kwa hiyo kilichotakiwa ni kumalizia tu. Leo Kenya wako wapi na katiba yao mpya?

Bila shaka unamkumbuka Bw Githongo na wadhifa wake wa kupambana na ufisadi na kujenga utawala bora baada ya NARC kutwaa madaraka! Hatimaye aliamua kukimbia nchi. Ripoti yake imeishia wapi?

Chiluba alifanya nini kwa Mzee Kaunda? Kisha Mwanawasa alifanya nini kwa Chiluba? Leo Zambia wana nini cha kujivunia?

Bingu wa Mutharika na sarakasi zake kwa Muluzi? Sana sana akamwachisha kazi Mkuu wa "TAKURU ya Malawi" kwa kutaka kumkamata Muluzi!

Tuje kwa hao CCM uliowasema. Hao walianza siku nyingi na misemo kama "Fagio la chuma" (Mzee Ruksa); "Ukweli na Uwazi" (Bilionea wa Lupaso) na sasa "Ari Mpya..." Tumeona nini mpaka sasa cha kujivunia? Hiyo mikataba ya madini alisema watapitia. Wengine wakasema hataweza kwa sababu ya sheria za biashara ya kimataifa zinazolindwa na asasi kama WTO, ICSD, MIGA etc.

Je, hata kurekebisha suala la uuzwaji nyumba za serikali wameshindwa na wala hamna sheria ya kimataifa inayowabana? Labda wanasubiri wawekezaji wa nje au kampuni kama vile Netgroup waje wawasaidie kusimamia zoezi hilo!

Haya, tuna Tume ya Maadili ya Viongozi na TAKURU. Mbona wameshindwa kuwashughulikia hao viongozi wanaotuhumiwa kujilimbikizia mali? Wabunge wa bunge hili tunaambiwa baadhi wamechenga kutaja mali; mbona "sheria haijafuata mkondo wake?"
 
Kwa hiyo ndugu Mwanagenzi, hitimisho lako ni nini?

Kuhusu nchi ulizozitaja kuna mafanikio yaliyopatikana. La wazi kabisa ni kuwa wananchi katika nchi hizo sasa wana uwezo wa kubadilisha serikali zao. Angalau wameweza kuthubutu. Hatukutarajia kuwa mafanikio ya serikali zilizotokana na wapinzani yangepatikana mara moja, lakini angalau wapo katika babarabara ya mafanikio. Tatizo letu na CCM ni kuwa tumeacha njia. Yaani tunataka kwenda Dodoma lakini tumepanda gari linaloenda Mtwara. kamwe hatutafika Dodoma! Wapinzani tukiingia tutahakikisha tunapanda gari husika ili tuelekee Dodoma. Tatizo la wenzetu ukiwaambia hili gari silo, hawakubali!
 
mwanasiasa nafikiri kwa maneno mengine ni kuwa tunajua tunahcokitaka (kwenda Dodoma) lakini hatutaki kupanda gari la kwenda Dodoma, na badala yake tunajitahidi kujipa matumaini kuwa gari la Mtwara linaweza kutufikisha Dodoma! Ni kweli tunaweza kufika Dodoma kwa kupitia Mtwara (inategemea tunatoka wapi) Ukweli wa mambo ni kuwa Dodoma itaendelea kuwa katikati ya nchi, na kama unatoka Dar kwenda Dodoma basi njia nyepesi bila ya shaka ni kupitia Morogoro!

Tunataka kujenga Taifa la kisasa, la kidemokrasia na lenye maendeleo lakini hatutaki kufanya vile vitakavyotufikisha huko!
 
Mwanasiasa,
Ni kweli sikuweka hitimisho.

Kwa maneno machache, na bila kujiumauma, "TUNAHITAJI DIKTETA MWENYE UZALENDO NA VISHENI".

Tutaendelea kujadiliana kwa hili!
 
Maneneno mazito haya jamani nahitaji kuyarudia maana yame niingia . Mungu inusuru Tanzania yangu .
 
Mzee Mwanakijiji,
Mbona mzee wazidi hizo hekima?.. shule ipi hiyo nami nijiunge?..

Ebu niongeze yangu machache toka madrasa Jamiati...heee heee!
Kweli kabisa wananchi wanachotaka ni kufika Dodoma na njia rahisi inayofahamika kwao ni kupitia Morogoro!..
Maswala ya Mtikila atatupeleka kwa ndege watu walimshtukia!.. huo uwezo wa kununua ama kukodisha ndege hana! - CCM wao ndio kwanza tunaambiwa gari liko geraji kesho, mambo swafi dereva kijana... sijui kijana ndio huongeza kasi ya gari bovu? tutajiju!.. Sasa Chadema.. Mwanakijiji ndio kesha wapeni urahisi wa kushika hilo barabara la morogoro road bado mnataka kutupelekeka Kivukoni kwanza!... Jamani hizo meli tumeisha ziona tuanze safari!
 

Mwanakijiji, nimekuwa nasoma maandishi yako siku za hivi karibuni. Ume-improve sana. Unakuwa wa kisasa. Una hoja. Keep it up!
 

Mtu yeyote anayeishi Bongo akaona jinsi jamaa hawa wanavyokanyaga kila kitu, wasivyoogopa, wanavyokula kwa mikono miwili bila kunawa...rejea suala la rada, ndege ya rais na twin towers...hawezi kusema wapinzani hawakubaliki. Mfumo ndio unaowakataa, kwa sababu wao wako nje. Lakini Tanzania inawahitaji sana, inawakubali, na watanzania wanawapenda wapinzani, ila CCM wanahamasishana kipropaganda kuwadhulumu wapinzani kwa kutumia pia tume ya uchaguzi iliyoundwa na rais kwa maslahi ya CCM. Bado tuko mbali. Wapinzani wanakubalika sana ila tunaongozwa na mifumo inayosimamiwa na mashabiki wa CCM na dola; wanaoomba kazi; wanaoganga njaa!
 
Kichwamaji upo sawa

Tatizo ni mfumo mbaya na jamii laini, tunao wapinzani makini na wanaokubalika.
 
Eric.. na wanaweza kupewa nchi? kusimamia taasisi zote? haya nipe line up ya serikali ya Wapinzani. Kama chama ni Chadema nani anaweza kuwa Rais, Waziri Mkuu, Makamu, Wakuu wa Mikoa, ma DCs, n.k.. just fill 100 positions..!
 
Mwkjj,
Kuna Watanzania wengi tu wenye uwezo. Ndani ya CCM na ndani ya upinzani. Si lazima utajiwe majina hivi sasa. Mwaka 1995 ulimjua Asha-Rose Migiro ni nani?
 
Mwanakijiji wanaweza,

Kwa nini unaamini viongozi wote ni wana CCM?wengine ni wataalaam wanaotumikia tu sera mbaya za CCM. Si sahihi kuaamini watalaam wote wa Tanzania wamehodhiwa na CCM! makatibu wakuu na viongozi wa taasisi za serekali ni waajiriwa wa serekali si mali ya CCM, wanaweza kutumikia serekali ya CCM, CHADEMA,TLP na kadhalika, Hawa wanajiriwa kutokana na ujuzi wao na sio itikadi pamoja na kuwa Wapo wasomi wanaolamba miguu viongozi.

Hata kama wote watakuwa wanachama wa CCM(si sahihi na si kwel), bado tunao watanzia wengi sana wanaweza kuchukua nafasi zao na kufanya kazi nzuri tu, wapo wengi tu ndani na nje ya nchi. CHADEMA yenyewe itapika sera mbadala(kazi halisi ya chama cha siasa).

Baraza la mawaziri mbona wengi tu, Raisi Mtu huru(The flying freeman) anao mawaziri kama zito kabwe, John Mnyika, wilboard slaa, Halima Mdee....

Na hawa ni wanaosikika tu,Kwa mfano ile timu ya kampeni ya Mnyka pale Ubungo ni serekali peke yake. Ile timu ilikuwa na wanafunzi wa UD,Mzumbe, SUA na IFM.Ni poropaganda isiyo na mantiki kusema vyama vya upinzani havina watu wa kuendesha serekali.

Inao watu wanaozidi maradufu,uwezo wa JK,lowassa, Makamba, Mudhihi mudhir na Ditopile. Tena ukitaka kujua tuna viongozi wenye uwezo mdogo fikiria hawa watu ndio wangekuwa wapinzani wangeweza kuwa na fikra mbadala?

Je leo CCM ikiwa chama cha upinzani kwa uongozi wake wa sasa itaweza kutoa fikra mbadala? Hawataweza, watapiga majungu tu basi sioni watu wa kutoa mawazo mazito katika safu ya juu ya CCM.
 
Eric,
Kama wasemavyo mahakamani: I rest my case. Chukua 5.
 
Eric.. na wanaweza kupewa nchi? kusimamia taasisi zote? haya nipe line up ya serikali ya Wapinzani. Kama chama ni Chadema nani anaweza kuwa Rais, Waziri Mkuu, Makamu, Wakuu wa Mikoa, ma DCs, n.k.. just fill 100 positions..!

Mwanakijiji,
Tatizo lako hapa unaamini kuongoza nchi ni jina maadamu wewe ni Kingunge, Lukuvi, Ditopile, Mashishanga basi ukipewa uongozi (soma utawala) unaweza. Hata kama ulikuwa upinzani kama Nswanzugwako ulikuwa huwezi hadi urejee CCM ndipo unapewa uwaziri na hapo akina mwanakijiji wataona kumbe ulikuwa na potential za kutawala.
Watanznaia wenye uwezo wa kuongoza wako wengi mno na wengi wao wako nje ya vyama vya siasa. Hivyo kutuambia nani atashika uongozi ni kuleta habari za CCM za kudhani watu wote lazima wawe wanachama wa vyama vya siasa.
Kinachokosekana Tanzania ni utawala wa kisheria na ndio maana tunaona hao wanaojidai ati wao tu ndio wenye uwezo wa kuongoza wakifanya mambo ya ajabu ajabu kwani hakuna kuwajibishwa. Penye utawala wa kisheria hata wewe Mwanakijiji, JJ, Mwanasiasa, Wacha, Wangwe, Halima Mdee na watu wengine lukuki ambao hawajihusishi moja kwa moja kwenye vyama wanaweza kuwa viongozi wazuri tu.
Hilo la kufill position mia hebu tuangalie maRC kama Abdul Aziz, Dito, Qaresi, Dr. Ishengoma na MaDC kama Betty Mkwasa, Uhahula na wengine wengi wana sifa gani ambazo ukipewa wewe huo UDC utashindwa? Hakuna zaidi ya ukada tu na kujipendekeza.
Ndio maana CHADEMA kinapendekeza nafasi nyingi za uongozi ziwe za kuchaguliwa badala ya kuteuliwa. Wanafahamu fika kuwa zaidi ya sifa watu watapeana ulaji kwa uana mtandao. Leo hii CHADEMA kikishika nchi utaona hao hao wanaojiita wafuasi wa CCm wataanza kusifia sera zake kumbe wanafuata ulaji. Kuepuka hilo wananchi wapewe nafasi ya kuchagua viongozi wao, wanatoka CCM, CUF, CHADEMA, CHAUSTA na wapi sijui hilo liachiwe wananchi. Nafasi zingine kama Ukurugenzi wa halmashauri za miji na manispaa hizo watu waombe na wapewe kulingana na sifa zao kama ambavyo ukurugenzi wa kampuni binafsi unavyoombwa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaainisha vema mtu gani anaweza kuwa kiongozi. Kwa mantiki hiyo si sahihi kudhani jina ambalo halijasikika tokea enzi za uhuru hadi leo hii halifaii kwa namna yeyote kuongoza na badala yake walewale wa tokea ninteen kweusi ndio wanaweza hata kama tumeona wanaharibu. Hatuna malaika ambao ni binadamu vilevile, iwe CCM, iwe CHADEMA, iwe CUF n.k ikiwa hakuna utawala wa kisheria hata kama chama kingeundwa na maprofesa waliobobea katika utawala na uzoefu wa miaka 45 bado mazingaombwe (kuazima maneno yako) tunayoonyeshwa sasa yataendelea milele.
 
Eric Ongora,
Nilikuwa busy najaribu kuweka senti mbili kwenye hoja ya mwanakijiji ambayo ni dhaifu kabisa ndipo nikakuta mchango wako mwanana ajabu. Na kwa sababu hiyo naongeza jina lako kwenye list ya viongozi wetu. Bila shaka Mwanakijiji anaamini civil servants wote ni die hard-CCM.
 
Mnajua wakati mwingine ninakuwa mgumu kueleweka. What you have just done is exactly what I have been asking you to do.. make yourself relevant! Mlichonihakikishia mimi ndicho Watanzania wanatakiwa kuhakikishiwa (do not assume they understand you and your potential as leaders). You have to make a case, kwamba wapinzani wanaweza kuongoza nchi! You do not need CCM to lead the nation, and as you Eric, and Tabasamu have eloquently pointed out... wapo viongozi wengi na watu wengi wenye uwezo wa kuongoza nje ya CCM!

Ninapouliza maswali haya do not assume what I think or where I stand! Mimi ni mjenga hoja, and sometimes, I need to do some socratic method to make my points across. Je wapinzani ni wakombozi? Je wanaweza kuongoza Tanzania, je watamudu kuongoza Tanzania bora zaidi kuliko CCM? You have to make a case with plausible arguments that you in principle and in fact CAN lead the nation!

To assume that kwa vile Watanzania wanaichagua CCM haina maana Watanzania wameridhika na CCM, yaweza pia kuwa na maana hawajaona uongozi mbadala ya CCM. Nyinyi ndio muwahakikishie kuwa mpo na mnaweza!!!
 
Mwanakjj,
Si kweli kwamba tunapoikosoa CCM basi tumekuwa wapinzania.Ukweli ni kuwa CCM inaleta kinyaa,inatuudhi inatulazimisha tuichukie,haifanyi kazi kama Chama ila kama kundi la majambazi wenye dhumuni maalum la kujilimbikizia mali.Mie sioni kile wanachostahili kujisifia,ambacho is so exceptional. "Mama anapoomba mimba akizaaa anawajibu wa kumnyonyesha mtoto wake na ahitaji kujisifia kwa kufanya hivyo".Hivyo basi CCM wanapoomba madaraka na wakapewa hizo km chache wanazojenga ni wajibu wao,ni kazi walioiomba.Zaidi mie nawaona hawa CCM ni sawa na mama aliyezaa then anamwacha mtoto wake bila ya kumyonyesha ili matiti yake yendelee kusimama na kuvutia wanaume.
Pamoja na kutowapenda CCM naona pia upinzani haujajipanga ili kuniondolea wasiwasi wangu katika kuwapa kura.Ila ni bora mara mia niwapatie wao nione watanifikisha wapi kuliko basi la CCM ambalo ninauhakika haliendi kule ninakohitaji.
Katika hesabu 4+4 kama ulijaza 2 na ukakosa, tena zaidi ya mara kadhaa itakuwa ni ujinga usipojaribu namba ingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…