Nyimbo wanazo sijabisha hilo, maana kila kabila dunia hii lina nyimbo zake za asili kama ilivyo kwamba wana lugha zao za asili, lakini ninachosema ni kwamba walishazitelekeza. Kupata nyimbo za asili sio issue, mbona kazi ya dakika chache tu, lakini cha msingi ni kwamba unakuta watu wa pale wengi hata hawana shughuli nazo na hawaziimbi wala kuongea lugha zao.
Hapa naweza nikakupa nyimbo za kizaramo, lakini kuwakuta wazaramo kitaa wakiziimba au wakiongea ongea lugha yao ya asili ni vigumu, wengi hawajui hata salamu na ndio taswira maeneo mengi Tanzania, watu wanaishi kama watumwa, hawajui asili yao na hawafundishi watoto wao mila na desturi zao. Mtoto anakua kama wale Wamarekani weusi wasiokua na asili wala kujua walitokea wapi. Wao hujua kwao ni Afrika, lakini hawajui chochote zaidi ya hapo na hutukanwa sana.