Lonestriker
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 640
- 241
si kweli kwamba watanzania hawatumi pesa...na hata hao wakenya na waganda si kwamba hawabebi maboksi au kufanya vibarua..naomba nikueleze kuwa unapokuwa mfanyakazi na kibarua tofauti ya mshahara ni ndogo sana tofauti na kwetu..tena unaweza kushangaa kuona kibarua ni mkorofi kuliko hata boss kwa sababu haofii kupoteza kazi ,kwa sababu anajua kesho atapata kazi sehemu nyingine na utaweza kuona kibarua hanaishi maisha mazuri tu tofauti na unavyofikiri..
Ngoja nikwambie kitu kimoja unaweza kuwa umesoma una PhD au Masters bado ukaendelea kuwa kibarua kwa sababu si rahisi kupata kazi za oficin kwa sababu hii si nchi yako kwani kuna wazawa bado Prof.lakini hana kazi..Swala la kumkuta mtu ana miaka 25 ana Ph D si swala la ajabu...
Jaribu kufuatilia hizo takwimu zako BOT huwe na uhakika ujue Watanzania wameweza kutuma kiasi gani..
Pia kumbuka watanzania wengi wanapojaribu kutuma pesa bongo basi jamaa zao zile pesa huwa wanazituma tofauti na malengo yanayotumwa kwa ajili ya matumizi ya hizo pesa..basi wengi wao huwa wanakata tamaa ya kutuma pesa nje..
Watanzania si wengi walioko nje kulinganisha na Wakenya kutokana na Watanzia wengi wanabaniana nafasi za kutoka nje...wenzetu wanasaidiana sana na kunyanyuana...
Unafahamu tafsiri ya hilo neno mabulungutu ya dollar? unaijuwa dollar wewe?[/QUOTE]
Ndio, ndio na ninazo pia.
Idadi ya WaTZ ni ndogo sana huku ughaibuni ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.
Hebu fikiria nchi kama Gambia yenye idadi ya watu 1M ndani ya Gambia lakini ina watu zaidi ya 1M nje ya Gambia??
Wakenya walianza kuzamia hapa nchi za Ulaya na Amerika toka 60 wakati sisi tumeanza 90.
Wenzetu watu wanao zamia ni aina zote wakati sisi wazamiaji wengi ni watoto wa viongozi wa serikali ya CCM ambao kamwe hawaoni haja ya kutuma fedha kwa wazee wao walionona fedha za wizi.
Pengine ingewekwa Takwimu ya Madingi wa Kitanzania wanao tuma fedha kwa watoto wao Huku ghaibuni Tanzania ingeongoza.
Hata hivyo si kweli kwamba vipato vya watanzania ni vidogo huku ughibuni. Tuko wachache.
Wagambia waishio Marekani kwa mfano ni zaidi ya 150,000 wakati waTanzania waishio marekani wako chini ya 25,000 kwa Takwimu za miaka3 iliyopita, wengi wao wakiwa wamelelewa kwenye mazingira ya joto la THERMOS kule Oysterbay.
Wakenya sijui idadi yao lakini nadhani wako zaidi ya 200,000, wao wanakuja huku wakiwa tayari wamejeruhiwa na maisha ya kubanwa kule Kenya wajanja kweli kweli, wakati sisi Watanzania tunakuja huku tukitarajia tumeukata tunakuja kutesa, zaidi tunawaz kununua magari furniture na kuopoa mademu wa kizungu. Siwezi kuwasemea dada zetu.
Bado tunaipenda nchi yetu, madai yetu ya uraia wa nchi mbili ni madai ya msingi. Hebu fikiria watoto wangu wote wamezaliwa hapa wana Passport za USA.Kisheria ni Wamarekani kwa sababu wamezaliwa hapa Je nchi yangu Tanzania ipo tayari kuwakubali wawe raia wa Tanzania pia?? Je kuzaliwa kwao nje ya Tanzania ndiyo sababu ya kuwafanya wasiwe raia wa Tanzania?? Kosa lao ni nini kutokua raia wa Tanzania??
Waganda na Wakenya wote wanaruhusiwa kuwa raia wa nchi zote mbili ya ughaibuni na ya kwao. Sisi kwa sababu bado tunatekeleza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hilo linaonekana ni uasi kwa nchi.
Maoni mengi yanatoka vijiweni zaidi kuliko kureflect ukweli.
Maisha hapa ughaibuni ni magumu sana hata ukilipwa fedha nyingi bado maisha si marahisi kwa sababu ya setup ya system nzima.
Dar ukilipwa $4000.00 umeukata kweli kweli hapa USA inategemeana uko state gani hawa wenzetu wana Tax za kuua mtu pili system imejengwa ili kuhakikisha unarudisha fedha yote kwao mabepari.
Wewe unaweza ishi kwa kula Bamia na ugali kila siku watoto wako waliozaliwa hapa watakugomea na mwisho wataishia kula shuleni wakirudi nyumbani hawali. Hivi unadhani kila uchao utamwekea Lunch Box ya wali na nyama au maharage mtoto wa Kitanzania aliyezaliwa Marekani??
Kuna tatizo la kutuma fedha Tanzania ksiha ndugu zako kukugeuza mjinga , wenyewe wanaita ATM.
Unatuma fedha ya kujenga nyumba yako au kurekebisha nyumba ya mdingi kijijini nduguzo ikiwa ni pamoja na mdingi wako wanaishia kujengea Tumboni Street na wengine kupata maradhi kwa sababu ya fedha yako.Mwisho unalaumiwa kwa kutuma fedha na kusababisha songombingo.
"Tangu uanze kumtumia fedha baba yako hapa nyumbani halali!!"
Wazazi au ndugu kuwa na matumaini makubwa kuopita kiasi hadi kufikia kuuliza mbona wewe hutumi fedha wakati so and so wanatuma fedha kila siku??
Yaani kila anyezamia Ughaibuni baada ya miaka 2 ni lazima awe ameukata??
Ukiwa abused namna hiyo na purukushani zote za First World si ndiyo hapo unaamua kula jiwe mpaka kielewke??
Wengi wamekuja ulaya kwa Package ya Scholarship, japo wamekaa miaka 3-4 system hawaijui hata kidogo wakirudi Bongo wanapaint picha tofauti kabisa na kufanya kila mtu huku aonekane si mzalendo huku ughaibuni.
Niliporudi Tz rafiki yangu mmoja aliniambia nirudi Bongho kwani najicheleweshea maendeleo yangu.
Katika kunipa stori ya namna alivyopata fedha niliishia kujua kwamba kila kitu kuanzia nyumba hadi utitiri wa magari ni matokeo ya Rushwa wizi na unyang'anyi wa kutumia nafasi yake, madaraka yake na loophole ndani ya system. Sikumwonea wivu hata kidogo kwa sababu;
Wizi niliukataa zamani nikiwa mtumishi Tanzania naukataa leo na kesho.
Katika miaka 10 ya utumishi wangu Tanzania nilifanikiwa kubana matumizi na kujenga nyumba 2 kisha kununu gari na kuoa. Vitu hivyo vinne vilinigharimu kila kitu nilichokua nacho na hata kunipachika jina la ugumu katika pesa,Roho ya korosho. Bado najivunia nyumba zangu mbili nilizo zijenga kwa taabu kwa pesa ya mshahara kwa kipindi cha miaka 10.(Enzi hizo mfuko wa cementi Tshs 2000 Mshahara kwa mwezi Tshs 12,500.00)japo kwa kiwango cha sasa nyumba inaonekana hafifu na ndogo.
Wengi hapa tunaishi kama ambavyo tungeishi Tanzania.
Wengi waishio Tanzania wanakunywa Bia kila siku, wanatembea na kila mtu wamtakaye, lakini wazazi wao hawawakumbuki. Lawama za kuto tuma fedha kwa wazazi tunajaziwa sisi tulioko ughaibuni.
Watanzania wengi,walio nje na walio ndani ni wavivu wa kufikiria kuhusu kesho.Hizo takwimu ni sahihi kabisa.Nashangaa mtua anaposema eti watanzania wanatuma pesa kwa njia ya mabulungutu,hivi kwani wakenya na waganda hawatumii hio njia?Au sisi ndio wajanja pekee tunaojua kutumia njia hizo za mabulunguti?Ok,hata kama ni mabulunguti mbona hatuoni kazi zake katika miji yetu?Binafsi natoka Mwanza lakini bado sijaona private estate hata moja ambayo unaweza kusema mwenye nayo anapiga kazi nje.watanzania hatutumii hela ipasavyo,tukubali udhaifu ili tuweze kupambana na hivyo virusi vya uzembe.
Cha msingi ndugu zangu mi naomba tusaidiane tu, regardless ya changamoto zilizopo kwenye hizo nchi za dunia ya kwanza( western countries) lakini bado kuna fursa ya kufanya kazi haijalishi ni casual au formal. Kuna Dr. Mmoja wa kike amenifundisha udsm alikuwa anasoma marekani, mwenyewe alisema alikuwa anafanya vibarua kwa masaa hata kufagia barabara, baada ya masomo yake kama miaka mitatu aliporudi bongo kapandisha majumba ya maana akaja na magari pia(NOT A STORY BUT A REALITY) .nawashukuru sana wachangiaji wengi ambao mmetupa uzoefu wenu huko ughaibuni, natambua mchango wako The Kop. Nimeumizwa mno na taarifa kwamba wengi wa wa-TZ wenzetu wanaonda ng'ambo badala ya ku-hustle ili wao ndio watume hela bongo eti wao ndio wanatumiwa.! Na hii inatokana na kwamba wengi wa wanaoenda huko ni watoto wa wenye nazo hasa wanasiasa ambao wengi wao ni legelege na wanajihurumia..tofauti na wenzetu wakenya ambao ni watafutaji matata, halafu wao kamwe hawaachani ingawa ni kwa makabila, hapa Tanzania graduates tunahaha ajira ngumu hadi uwe una mjuwa fulani, wanabana hata ku-volunteer, wanashobokea wakenya ambao sasa hv ni wengi na baadhi yao ndio mameneja waajiri.! Tanzania sasa hivi inaboa, MLIO UGHAIBUNI MTUSAIDIE NA SISI TUTOKE Tz .![/QUOTE]
Mkuu pole sana manake nimeisoma comment yako na napata picha rumba limekuwa kali sana na umepigika na msoto wa bongo kinoma.
Usikonde. Kaza roho na iko siku utaibukia huko unakotaka kwenda. Kila la heri
Watanzania kwa kuomba jamani heee! haya usipotuma ndio hivyo unabeba box, Ukituma mjinga wewe ATM.. Basi ili mradi haijulikani ufanye nini.. Hakika Kwa mtanzania kila siku ni drama tu, na ajabu anayewahoji watu wa Ulaya yeye mwenyewe kibarua kesho kinaweza kuota...
Watanzania wanaoishi nje wanapeleka wapi pesa zao
WaKenya ambao waaishi huku Tanzania na kwingineko duniani, mwaka uliopita walirudisha nyumbani kwao zaidi ya dola za Marekani $640 million. Wauganda nao walirudisha kwao $850 million mwaka jana. Pesa hizi zinatumika kununua nyumba, kulipa ada za shule, matibabu, nk na zinachangia sana kwenye pato la kigeni la nchi hizi jirani zetu.
Huko Kenya, pesa zinazotumwa na raia walio nje ndiyo chanzo kikubwa cha nne cha mapato ya kigeni baada ya mauzo ya nje ya chai, mauwa na utalii.
Benki Kuu ya Tanzania wala haijishuhulishi na pesa zinazotumwa nje na Watanzania na wala haitoi takwimu zake. Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, Watanzania wanaoishi nje (diaspora) wengi wenu mkiwa wachangaji wakubwa wa mada humu JF, mwaka jana walitarajiwa kurudisha nchini kwao $17 milion tu?!
Hii ina maana mbili. Watanzania walio nje ni wachache sana au ni wengi lakini siyo skilled workers wanaoweza kupata kipato kizuri kutokana na taaluma zao. Pengine wengi wenu mnafanya kazi za kibarua, hourly shifts kubeba maboksi and flipping burgers MacDonalds na KFC hivyo hamna pesa za kutuma kwenu nyumbani kwa ajili ya maendeleo na kusaidia ndugu zenu. Si mrudi basi Bongo?
Au maana nyingine ni kuwa pesa hizo zinatumwa kwa wingi lakini Benki Kuu haifanyi utaratibu wowote wa kuzirekodi. Au zinatumwa kienyeji kwa kufichwa kwenye barua na mizigo mingine. Ama Watanzania mnaendekeza anasa tu huko majuu wakati Wakenya na Waganda wanajenga nchi zao? Nawaza sipati jibu.
Mkuu ukweli ni kwamba most of them, kwanza hawajaenda shule hivyo kazi za profession huwezi kupata na wengi wao wanaishi kwa kubahatisha hizo hela za kutuma huko watapata wapi?? Wale professional wachache wanajifanya kama sio watanzania tena na hawataki kusikia kitu chochote kuhusu bongo!! Sio kwamba hawawakumbuki ndugu zao bali hawana cha kutuma:twitch:!!
Watanzania wanaoishi nje wanapeleka wapi pesa zao
WaKenya ambao waaishi huku Tanzania na kwingineko duniani, mwaka uliopita walirudisha nyumbani kwao zaidi ya dola za Marekani $640 million. Wauganda nao walirudisha kwao $850 million mwaka jana. Pesa hizi zinatumika kununua nyumba, kulipa ada za shule, matibabu, nk na zinachangia sana kwenye pato la kigeni la nchi hizi jirani zetu.
Huko Kenya, pesa zinazotumwa na raia walio nje ndiyo chanzo kikubwa cha nne cha mapato ya kigeni baada ya mauzo ya nje ya chai, mauwa na utalii.
Benki Kuu ya Tanzania wala haijishuhulishi na pesa zinazotumwa nje na Watanzania na wala haitoi takwimu zake. Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, Watanzania wanaoishi nje (diaspora) wengi wenu mkiwa wachangaji wakubwa wa mada humu JF, mwaka jana walitarajiwa kurudisha nchini kwao $17 milion tu?!
Hii ina maana mbili. Watanzania walio nje ni wachache sana au ni wengi lakini siyo skilled workers wanaoweza kupata kipato kizuri kutokana na taaluma zao. Pengine wengi wenu mnafanya kazi za kibarua, hourly shifts kubeba maboksi and flipping burgers MacDonalds na KFC hivyo hamna pesa za kutuma kwenu nyumbani kwa ajili ya maendeleo na kusaidia ndugu zenu. Si mrudi basi Bongo?
Au maana nyingine ni kuwa pesa hizo zinatumwa kwa wingi lakini Benki Kuu haifanyi utaratibu wowote wa kuzirekodi. Au zinatumwa kienyeji kwa kufichwa kwenye barua na mizigo mingine. Ama Watanzania mnaendekeza anasa tu huko majuu wakati Wakenya na Waganda wanajenga nchi zao? Nawaza sipati jibu.