Idadi ya WaTZ ni ndogo sana huku ughaibuni ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.
Hebu fikiria nchi kama Gambia yenye idadi ya watu 1M ndani ya Gambia lakini ina watu zaidi ya 1M nje ya Gambia??
Wakenya walianza kuzamia hapa nchi za Ulaya na Amerika toka 60 wakati sisi tumeanza 90.
Wenzetu watu wanao zamia ni aina zote wakati sisi wazamiaji wengi ni watoto wa viongozi wa serikali ya CCM ambao kamwe hawaoni haja ya kutuma fedha kwa wazee wao walionona fedha za wizi.
Pengine ingewekwa Takwimu ya Madingi wa Kitanzania wanao tuma fedha kwa watoto wao Huku ghaibuni Tanzania ingeongoza.
Hata hivyo si kweli kwamba vipato vya watanzania ni vidogo huku ughibuni. Tuko wachache.
Wagambia waishio Marekani kwa mfano ni zaidi ya 150,000 wakati waTanzania waishio marekani wako chini ya 25,000 kwa Takwimu za miaka3 iliyopita, wengi wao wakiwa wamelelewa kwenye mazingira ya joto la THERMOS kule Oysterbay.
Wakenya sijui idadi yao lakini nadhani wako zaidi ya 200,000, wao wanakuja huku wakiwa tayari wamejeruhiwa na maisha ya kubanwa kule Kenya wajanja kweli kweli, wakati sisi Watanzania tunakuja huku tukitarajia tumeukata tunakuja kutesa, zaidi tunawaz kununua magari furniture na kuopoa mademu wa kizungu. Siwezi kuwasemea dada zetu.
Bado tunaipenda nchi yetu, madai yetu ya uraia wa nchi mbili ni madai ya msingi. Hebu fikiria watoto wangu wote wamezaliwa hapa wana Passport za USA.Kisheria ni Wamarekani kwa sababu wamezaliwa hapa Je nchi yangu Tanzania ipo tayari kuwakubali wawe raia wa Tanzania pia?? Je kuzaliwa kwao nje ya Tanzania ndiyo sababu ya kuwafanya wasiwe raia wa Tanzania?? Kosa lao ni nini kutokua raia wa Tanzania??
Waganda na Wakenya wote wanaruhusiwa kuwa raia wa nchi zote mbili ya ughaibuni na ya kwao. Sisi kwa sababu bado tunatekeleza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hilo linaonekana ni uasi kwa nchi.
Maoni mengi yanatoka vijiweni zaidi kuliko kureflect ukweli.
Maisha hapa ughaibuni ni magumu sana hata ukilipwa fedha nyingi bado maisha si marahisi kwa sababu ya setup ya system nzima.
Dar ukilipwa $4000.00 umeukata kweli kweli hapa USA inategemeana uko state gani hawa wenzetu wana Tax za kuua mtu pili system imejengwa ili kuhakikisha unarudisha fedha yote kwao mabepari.
Wewe unaweza ishi kwa kula Bamia na ugali kila siku watoto wako waliozaliwa hapa watakugomea na mwisho wataishia kula shuleni wakirudi nyumbani hawali. Hivi unadhani kila uchao utamwekea Lunch Box ya wali na nyama au maharage mtoto wa Kitanzania aliyezaliwa Marekani??
Kuna tatizo la kutuma fedha Tanzania ksiha ndugu zako kukugeuza mjinga , wenyewe wanaita ATM.
Unatuma fedha ya kujenga nyumba yako au kurekebisha nyumba ya mdingi kijijini nduguzo ikiwa ni pamoja na mdingi wako wanaishia kujengea Tumboni Street na wengine kupata maradhi kwa sababu ya fedha yako.Mwisho unalaumiwa kwa kutuma fedha na kusababisha songombingo.
"Tangu uanze kumtumia fedha baba yako hapa nyumbani halali!!"
Wazazi au ndugu kuwa na matumaini makubwa kuopita kiasi hadi kufikia kuuliza mbona wewe hutumi fedha wakati so and so wanatuma fedha kila siku??
Yaani kila anyezamia Ughaibuni baada ya miaka 2 ni lazima awe ameukata??
Ukiwa abused namna hiyo na purukushani zote za First World si ndiyo hapo unaamua kula jiwe mpaka kielewke??
Wengi wamekuja ulaya kwa Package ya Scholarship, japo wamekaa miaka 3-4 system hawaijui hata kidogo wakirudi Bongo wanapaint picha tofauti kabisa na kufanya kila mtu huku aonekane si mzalendo huku ughaibuni.
Niliporudi Tz rafiki yangu mmoja aliniambia nirudi Bongho kwani najicheleweshea maendeleo yangu.
Katika kunipa stori ya namna alivyopata fedha niliishia kujua kwamba kila kitu kuanzia nyumba hadi utitiri wa magari ni matokeo ya Rushwa wizi na unyang'anyi wa kutumia nafasi yake, madaraka yake na loophole ndani ya system. Sikumwonea wivu hata kidogo kwa sababu;
Wizi niliukataa zamani nikiwa mtumishi Tanzania naukataa leo na kesho.
Katika miaka 10 ya utumishi wangu Tanzania nilifanikiwa kubana matumizi na kujenga nyumba 2 kisha kununu gari na kuoa. Vitu hivyo vinne vilinigharimu kila kitu nilichokua nacho na hata kunipachika jina la ugumu katika pesa,Roho ya korosho. Bado najivunia nyumba zangu mbili nilizo zijenga kwa taabu kwa pesa ya mshahara kwa kipindi cha miaka 10.(Enzi hizo mfuko wa cementi Tshs 2000 Mshahara kwa mwezi Tshs 12,500.00)japo kwa kiwango cha sasa nyumba inaonekana hafifu na ndogo.
Wengi hapa tunaishi kama ambavyo tungeishi Tanzania.
Wengi waishio Tanzania wanakunywa Bia kila siku, wanatembea na kila mtu wamtakaye, lakini wazazi wao hawawakumbuki. Lawama za kuto tuma fedha kwa wazazi tunajaziwa sisi tulioko ughaibuni.