Je, Watanzania mlio nje ni vibarua na wabeba maboksi?

Je, Watanzania mlio nje ni vibarua na wabeba maboksi?



Watanzania wanaoishi nje wanapeleka wapi pesa zao


WaKenya ambao waaishi huku Tanzania na kwingineko duniani, mwaka uliopita walirudisha nyumbani kwao zaidi ya dola za Marekani $640 million. Wauganda nao walirudisha kwao $850 million mwaka jana. Pesa hizi zinatumika kununua nyumba, kulipa ada za shule, matibabu, nk na zinachangia sana kwenye pato la kigeni la nchi hizi jirani zetu.

Huko Kenya, pesa zinazotumwa na raia walio nje ndiyo chanzo kikubwa cha nne cha mapato ya kigeni baada ya mauzo ya nje ya chai, mauwa na utalii.

Benki Kuu ya Tanzania wala haijishuhulishi na pesa zinazotumwa nje na Watanzania na wala haitoi takwimu zake. Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, Watanzania wanaoishi nje (diaspora) wengi wenu mkiwa wachangaji wakubwa wa mada humu JF, mwaka jana walitarajiwa kurudisha nchini kwao $17 milion tu?!

Hii ina maana mbili. Watanzania walio nje ni wachache sana au ni wengi lakini siyo skilled workers wanaoweza kupata kipato kizuri kutokana na taaluma zao. Pengine wengi wenu mnafanya kazi za kibarua, hourly shifts kubeba maboksi and flipping burgers MacDonalds na KFC hivyo hamna pesa za kutuma kwenu nyumbani kwa ajili ya maendeleo na kusaidia ndugu zenu. Si mrudi basi Bongo?

Au maana nyingine ni kuwa pesa hizo zinatumwa kwa wingi lakini Benki Kuu haifanyi utaratibu wowote wa kuzirekodi. Au zinatumwa kienyeji kwa kufichwa kwenye barua na mizigo mingine. Ama Watanzania mnaendekeza anasa tu huko majuu wakati Wakenya na Waganda wanajenga nchi zao? Nawaza sipati jibu.

Soma hii study ambayo inapatikana katika journal ya World Bank WBER Vol. 25 (1)

[h=1]Remittances and the Brain Drain Revisited: The Microdata Show That More Educated Migrants Remit More[/h]
[h=2]Abstract[/h]Two of the most salient trends in migration and development over the last two decades are the large rise in remittances and in the flow of skilled migrants. However, recent literature based on cross-country regressions has claimed that more educated migrants remit less, leading to concerns that further increases in skilled migration will impede remittance growth. Microdata from surveys of immigrants in 11 major destination countries are used to revisit the relationship between education and remitting behavior. The data show a mixed pattern between education and the likelihood of remitting, and a strong positive relationship between education and amount remitted (intensive margin), conditional on remitting at all (extensive margin). Combining these intensive and extensive margins yields an overall positive effect of education on the amount remitted for the pooled sample, with heterogeneous results across destinations. The microdata allow investigation of why the more educated remit more, showing that the higher income earned by migrants, rather than family characteristics, explains much of the higher remittances.
 
Nafikiri tungeomba data toka BOT maana hii hesabu sidhani kama iko sahihi. Pia ningependa kujua how they arrived to $17mill in remitts across all of the Tanzanian diaspora.

Zaidi nasikitishwa na attitude ya baadhi ya wa Ughaibuni maana ni jazba na kutaka kila mtu ajijue kivyake! Lakini ukweli ni kwamba; unapopeleka pesa nyumbani sio unatuma tu kuwalisha ndugu na jamaa bila kufuatilia au kuwa-challange waizungushe ili nao wajitegemee. Hivi kama wewe ukikwama ndio wafe njaa? Inabidi uwashauri na kuwakomalia ili wafanye yale mnayokubaliana. Sio haki kusema bongo ukituma hela unanunuliwa kiwanja hewa na kujengewa tumboni street. Personally nimefanikiwa kuwekeza japo senti kidogo sehemu nyingi kupitia partnerships na ndugu, jamaa na hata schoolmates.

Nafikiri kama unaishi nje na unajihesabu kama mTz, basi tafuta jinsi uwekeze kwenu. However, kama umehamia nje na ndio kwenu kupya, nayo kheri. Mwisho wa siku Tz itajengwa au kuvunjwa na waTz. Unapokazana kulaumu jiulize kama umefanya all that is in your means kuelimisha, kuboresha, kuwezesha etc etc. Mara nyingi utajikuta you can take an extra step... so please do. Nawasilisha.
 
Acha mentality za kijinga wewe mtoa mada. Wenzetu Ulaya hawachagui kazi, mtu na PhD yake unamkuta anapangua snow kama kawaida, ili mradi mkono unaenda kinywani . Blue colar workers wa Ulaya huwezi kumlinganisha na Professor wa Tanzania kimapato. Hivyo issue hapa siyo aina ya kazi bali ni kipato. Hivyo nakushauri achana na inferiority complex yako, nikuhakikishie pia kuwa mawazo kama ya kwako yameshapitwa na wakati.

mkuu nakuunga mkono
mimi nchi ninayoishi ninapata mshahara mkubwa kuliko wabunge wenu hapo bongo na sina elimu kubwa
 
mkuu nakuunga mkono
mimi nchi ninayoishi ninapata mshahara mkubwa kuliko wabunge wenu hapo bongo na sina elimu kubwa
Sina tatizo na mbeba box yeyote, ila wewe huwezi kuwa na mshahara wa kumzidi mbunge wa Tanzania, labda mbunge wa hiyo nchi unayoishi.
 
Kuna nchi zingine huku ulaya, watu ambao hawajasoma wanalipwa pesa nyingi kuliko hata watu wa ofisini, kwahiyo hiyo sio sababu. Kazini kwetu mshahara wa chini kabisa baada ya taxes kwa watu ambao hawaja soma ni around 4000 usd. Kuna Watanzania wengi ambao tumesoma na tuna kazi nzuri tu. Lakini siwezi hata siku moja ku invest pesa yangu TZ kama mimi mwenyewe sipo, kila siku watu wanalizwa. At the end of the day, who wants that bullshit ya kukimbizana na watu. So there are some of us who have chosen to invest in Europe na tunaendelea vizuri tu zaidi ya ningejifanya ku invest in TZ.
 
Back
Top Bottom