Je watanzania wanafahamu kuhusu miradi ya TACTIC kwa upana?

Je watanzania wanafahamu kuhusu miradi ya TACTIC kwa upana?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imeendelea kutoa mafunzo ya masuala ya kijamii na Mazingira kwa watumishi wa Halmashauri Tanzania, zinazotekeleza awamu ya mbalimbali za mradi wa TACTIC inayotekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya Dunia.​

1721649725485.png


Mafunzo yamefanyika huku lengo likiwa ni kuhakikisha miradi inayotekelezwa haileti athari za kimazingira na kijamii katika halimashauri hizo. Mratibu wa Mradi TACTIC kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Emmanuel Manyanga amewakumbusha wataalamu hao kuhakikisha wanasimamia na kuondoa athari za kijamii na kimazingira wakati wa kuelekea utekelezaji wa mradi huo.​

PICHA LINAANZA HAPA!​

Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa alisema hatua za awali za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zimekamilika katika miji 12 kati ya 45 ya awali itakayonufaika na miradi ya kuboresha miundombinu katika Miji, Manispaa na Majiji. Bashungwa alitoa maelekezo hayo Jumanne ya Septemba 20, 2022 Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa majibu ya maswali ya waheshimiwa wabunge kuhusu hatua za utekelezaji wa Miradi ya Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness (TACTIC).

1721648439229.png


“Usanifu katika miji 12 tayari umekamilika, kazi ya kutangaza tenda kwa ajili ya kupata wakandarasi itafanyika muda wowote ili kazi zianze Mwezi Machi 2023” alisema Bashungwa.

Bashungwa alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hii ya TACTIC umegawanyika katika Makundi matatu, ambapo kundi la kwanza ni Miji ya Arusha CC, Mwanza CC, Dodoma CC, llemela MC, Kigoma MC, Mbeya CC, Geita TC, Morogoro CC, Songea MC, Sumbawanga MC, Tabora MC na Kahama MC. Awali Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza kuwa baada ya Serikali kusaini Mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia, mradi huu utaratibiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI mwezi Juni 2022, alielekeza utekelezaji wa Miradi huo kuanza mara moja.

Aidha, Bashungwa amesema utekelezaji wa miradi hiyo katika kundi la kwanza utaenda sambamba na kundi la pili litakalohusisha miji 15 ambayo ni Mtwara Mikindani MC, Tanga CC, Babati TC, Bariadi TC, Bukoba MC, Iringa MC, Kibaha TC, Korogwe TC, Lindi MC, Moshi MC, Mpanda MC, Musoma MC, Njombe TC, Singida MC na Shinyanga MC.

1721648508159.png


Vile vile, alisema utekelezaji wa miradi ya TACTIC kundi la tatu ulitazamiwa kufanyika katika mwaka wa fedha wa 2022/ 2023 katika miji ya Bunda TC, Handeni TC, Ifakara TC, Kasulu TC, Kondoa TC, Mafinga TC, Makambako TC, Masasi TC, Mbinga TC, Mbulu DC, Nanyamba TC, Newala TC, Nzega TC, Tarime TC, Tunduma TC, Vwawa TC, Bagamovo DC, Chato DC.

Ila ukiingia kwenye tovuti ya TAMISEMI utakutana na kitu kinaitwa Safeguard Documents for TACTIC Project ambapo kina link za documents zinazohusu mradi huu, kuanzia, ESCP TACTIC Project, LMP for TACTIC Project, ESMF for TACTIC Project, RPF for TACTIC Project, pamoja na SEP For TACTIC Project. Sehemu ambayo nimepata kuipitia kwa umakini na kuona kuna vitu havipo sawa haswa kwa upande wa wananchi.
Kwanza kabsa kuna kauli ambayo wananchi hatujawahi kuikubali hata siku moja:​
"The United Republic of Tanzania through the President’s Office-Regional Administration and Local Government is planning to implement the Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness Project (TACTIC) through Tanzania Rural and Urban Roads Agency (TARURA) with various Local Government Authorities (LGAs) being the implementing Agencies."

Yaani mradi ukisimamiwa na Halmashauri za Miji basi hapo pesa zitapigwa hatari na sio suala la kuuliza kwani inaeleweka wazi wazi, Ripoti za CAG zinaonesha na zinatupatia maumivu makubwa wananchi huku kwa upande wa viongozi ripoti zikiwa ni kama vile haziwahusu. Sasa mwanzoni kabsa inasema kuwa Halmashauri ndo zitakuwa zinafanya kazi pamoja na TAMISEMI pamoja na TARURA kwenye kufanikisha mradi wa TACTIC. Sio mbaya!

1721648618523.png


Nyaraka nyingi kuhusu mradi huu zipo kwenye lugha ya Kiingereza, na zina taarifa nyingi sana, nyaraka moja inaweza kuwa na kurasa hata zaidi ya 80 tena kwenye mfumo wa pdf. Kulikuwa na kila sababu ya kutengeneza nakala ya lugha ya kiswahili na kuzisambaza kwa wananchi kuelewa kile ambacho kitaendelea. Pia tukumbuke kuwa hizi pesa tutatakiwa kuzilipa kwa World Bank sio bure bali kwa riba, sasa hapo chini sentensi inasema:
"Where Project changes, unforeseen circumstances, or Project performance result in changes to the risks and impacts during Project implementation, The United Republic of Tanzania through PORALG/TARURA and respective Local Government Authorities (LGAs shall provide additional funds, if needed."

Ni kweli kabsa kuwa mradi ukipata tatizo sehemu basi World Bank hatotakiwa kutoa pesa ya ziada yoyote, hivyo TAMISEMI pamoja na TARURA wataingia mfukoni kwa ajili ya kujazia pesa ili miradi ikamilike. Swali langu la msingi ni “Je ili kuweka sawa mahesabu ya kifedha kwenye miradi hii, hawa TAMISEMi na TARURA watachukua pesa kwenye mifuko yao ya kawaida au wataongea tozo na ushuru katika huduma za umma? Je vyombo hivi vina vyanzo vya kujitegemea ambavyo haviwezi kuwaumiza wananchi?

Tusisahau kuwa wapigaji wapo wengi wa wameziona hizi 745,766,491.84 ni pesa za kujenga miradi yao binafsi na kupata ulaji, na amini usiamini kiasi hiki cha pesa kwa usimamizi wetu watanzania wenye njaa hakitoshi kumaliza miradi ya TACTIC. Kila halmashauri ina wapigaji wake wa pesa haswa hizi ambazo zinatoka kwa wahisani.

1721648755614.png


Tukumbuke nyuma kidogo Kipindi Waziri Jaffo alipouliza kuhusu pesa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale, fedha ambazo zimepotea katika miradi ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R). Sasa TACTIC upo salama kweli?

Serikali imefeli sana kuwaelezea watanzania kuhusu miradi hii ya TACTIC, nina uhakika kuwa serikali ikitaka jambo lake lifanikiwe hutumia TBC kusambaza jumbe na taarifa kwa wananchi. Mfano, chanjo ya UVIKO-19 TBC ilipiga kampeni kisawasawa kiasi kwamba baadhi ya wafanyakazi wake walitoka hadharani na kusema wamechanja chanjo. Kwanini TBC haijatupatia makala ya kusifia serikali kuhusu kutia saini kwenye hili.

1721648823755.png


Kweli wameshindwa kuwatangazia wananchi kuwa WB wametupatia mkopo wa pesa 745,766,491.84 kwa ajili ya miradi ya TACTIC? Au ndo kimya kimya ili pesa ziishe juu kwa juu halafu Mwigulu Nchemba aje kutuongezea tozo ili tuweze kulipa mkopo wa watu. Ikumbukwe kuwa pesa hizi zitalipwa kwa riba, pesa ya mzungu haiendi bure bure.

Pia tufuatilie mambo vizuri, sio kweli kuwa Rais Samia ndo aliyetoa pesa kwa ajili ya miradi ya TACTIC kama vile wachambuzi wanavyosema na kudai. Kuna chapisho moja humu ndani linaelezea kuwa Rais Samia Ametoa Shilingi Trilioni 1 Kuboresha Miji, taarifa hii sio ya ukweli, ni Benki ya Dunia ndio imeikopesha serikali ya Tanzania.

Tujiandae kulipa mkopo wa World Bank!
 
Back
Top Bottom