Je , Watanzania wenye elimu ya kuanzia diploma hadi profesa ni wangapi?

Je , Watanzania wenye elimu ya kuanzia diploma hadi profesa ni wangapi?

Tatizo ni uchache wa wasomi au uchache wa fursa za ajira ;
Kwahapa kwetu siasa inanguvu kuliko elimu, kwahyo usitegemee maajabu ya hili kundi dogo lililomezwa na kundi kubwa.

Chengne ubinafs kila mtu anajal tumbo lake na kizaz chake kuanzia mfanyakaz wa kiima Cha chini Hadi ju kwenye ngazi ya utumish wa umma, na mjumbe wa nyumba kumi Hadi juu kwenye ngazi ya kisiasa
 
Kwa mujibu wa makadirio ya sensa ya mwaka 2022, Tanzania ina takribani watanzania milioni 60. Kati ya hao, idadi ya waliopata elimu ya juu (yaani kuanzia Diploma, Degree, Masters hadi PhD/Profesa) ni ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa idadi hiyo.

Takwimu Muhimu (Elimu ya Juu kwa Watu Wenye Miaka 25 na Zaidi):

  • 2.6% ya Watanzania wana elimu ya baada ya sekondari (diploma na kuendelea).
  • Kwa idadi ya watu milioni 60, hii ni sawa na takribani 1,560,000 watu.
(Chanzo: Charting the Globe – Educational Attainment in Tanzania)

Tofauti kati ya Miji na Vijijini (Utafiti wa ResearchGate, 2024):

  • Vijijini: Wanawake wenye elimu ya diploma au chuo kikuu ni 0.5%
  • Miji mingine (nje ya Dar): Wanawake wenye elimu ya juu ni 3.6%
  • Dar es Salaam: Wanawake wenye elimu ya diploma au shahada ni 7.5%

(Chanzo: ResearchGate – “Growing Through Cities in Tanzania”, 2024)

Sekta Rasmi ya Ajira (Utafiti wa NBS 2022/23):

  • PhD holders: 0.7%
  • Master’s holders: 2.5%
  • Bachelor/Diploma ya Juu: 32.3%
  • Diploma ya Kawaida: 31.9%
(Idadi ilichukuliwa kati ya wafanyakazi 1,367 walioajiriwa rasmi)
(Chanzo: NBS Employment and Earnings Survey 2022/23)


Hitimisho:
Licha ya ongezeko la vyuo na nafasi za elimu ya juu, Watanzania wenye elimu kuanzia diploma hadi profesa bado ni wachache – wengi wakitokea mijini kama Dar es Salaam. Changamoto bado ipo vijijini, ambako upatikanaji wa elimu ya juu ni mdogo sana.
Tanzania, on the whole, hakuna wasomi, acha ujinga.

Usomi haupimwi kwa makaratasi, acha ulimbukeni.
 
Ukosaji wa Ajira inafanya vijana kuishia ngazi za chini na kujihusisha na kutafuta pesa wanaona muda unaenda na Ajira hamna
Na wengi wanaishia njiani kuridhika na kiwango cha elimu kumbe bado

Wengine wanakata tamaa
 
Profesa siyo elimu bali ni ngazi katika ufundishaji wa vyuo vikuu. Vyuo vingine vina ngazi hiyo kiwango cha chini sana wakati kuna vyozu vintoa ngazi hiyo kwa kiwangio cha juu sana. Ni kawaid kumtaja profesa kama vile "Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Oxford" ili kumtofautishba na maprofesa uchwala kama wa chuo kikuu cha Kuchuguuni.
 
Back
Top Bottom