The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Si nadra kusikia watendaji wa umma wakisema "rais amefanya, ametoa, anataka, hataki,' na mengine mengi. Je watendaji wetu wapo kwa ajili ya rais au taifa?
Je wanafanya wafanyayo kwa sababu ya hisani, mapenzi, au utashi wa rais au matakwa ya sheria za nchi? Je rais wetu ni sheria na yuko juu ya sheria? Je ni kwanini rais ameshindwa kuliona, kulikemea, na kuliepuka hili?
Je hili linamuonyesha kama mtawala au kingozi wa namna gani? Je inakuwaje rais wetu ni mkubwa kuliko serikali na nchi hata kuonekana kama yuko juu ya sheria?
Wakizindua au kufanikisha kukamilisha mradi, utawasiki wakisema 'haya ni matokeo, maono, au msaada toka kwa rais. Je rais anatumia fedha yake binafsi? Je hii siyo aina fulani ya udikteta, ufisadi, na matumizi mabaya ya madaraka ambayo ni dhamana toka kwa wananchi?
Je nini kifanyike kuwaelimisha watu wa namna hii ambao hawajui kuwa nchi ni zaidi ya rais? Je serikali ni rais tu au na taasisi nyingine za umma kama vile mihimili mitatu ya dola?
Naomba kuwasilisha.