Ibrahim alikuwa mcha Mungu kwa namna ambavyo Mungu alimueleze. Alafu unapaswa kutofautishwa sana ukristo na uislamu. H akuna dini ya ukristo iliyeshushwa kutoka mbinguni, ukristo ni namna ya. kumwabudu Mungu iliyotokana na Torati na mafundisho ya Yesu ,mwenyewe. Sisi wakristo neno dini huwa tnallisikia kwa waislamu pekee,, kifupi dini ni uislamu pekee. Sisi tuna taratibu zetu za kuabudu tumezitoa kwenye Torati na mwalimu mkuu wetu Yesu kristo, sisi ni wafasi wa Yesu kristo blaza, mambo ya dini ni yenu tu
Subhanallah nimesoma jibu lako nikabaki nafurahi why? Fitra yako inajitahidi kukuonesha kitu ila wewe bado umejiziba macho na hautaki kuona hebu tuangalie kile namaanisha .
1. tukianza na hapo uliposema "ibrahim alikuwa mcha mungu kwa namna ambayo Mungu alimuelezea " sasa unajua Mungu amemuelezea vipi ? Tuangalie aya hii hapa kwenye surat imran
Aal-e-Imran 3:67
مَا كَانَ إِبْرَٰهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.
Kumbe ili uwe mchamungu sharti uwe muislamu maana ndiyo dini ya kweli na je ? Wapi tunathibitisha hili? Kutokana na kauli yako hii hapa
"....kifupi dini ni uislamu pekee...." 😄😄
2. sasa tuthibitishe kauli yako kwa aya hii hapa
Kwenye sura hiyo hiyo al imran
Aal-e-Imran 3:19
إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلْإِسْلَٰمُۗ وَمَا ٱخْتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْۗ وَمَن يَكْفُرْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
HItimisho .
Ushauri wangu ni msome kwa hakika mkisoma mtaujua ukweli msiwe mnapelekwa pelekwa kaeni chini someni dini anzeni na dini yenu soma pia uislamu soma na dini nyengine kwa ajili ya kuutafuta ukweli fungueni akili mwisho mtakuja kugundua wapi ukweli upo.