#COVID19 Je, watu wa mtaani kwako wanachukua tahadhari dhidi ya #CoronaVirus?

#COVID19 Je, watu wa mtaani kwako wanachukua tahadhari dhidi ya #CoronaVirus?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
20210316_164025_0000.png


Ni kawaida kwa watanzania walio wengi kuona suala la kawaida kama halijamgusa moja kwa moja. Hali hii iko hivyo kwa baadhi ya maeneo hapa nchini

Je, hali ikoje kwenye mtaa wako?

Watu wanachukua tahadhari au wanapuuzia ugonjwa?

Je, unachukua hatua yoyote kuwaelimisha zaidi?
 
Mtaani kwangu kwanza hawaamini kabisa kama hii kitu ipo, achilia mbali kuchukua tahadhari, na huwaambii kitu 😄😄😄
 
Hakuna hatua inayochukuliwa watu wanaishi normal life.
 
Corona achieni mizungu sisi tupambane na hali zetu za kutafuta mkate wa kila siku.

Hela ya kununua mask na vitakasa mikono ni kubwa kuliko bei ya vitafunio vya chai.
 
Ni kudra za MUNGU tu kwa waTanzania ambao hatujaguswa na tatizo hili hasa tulio mbali na miji mikubwa.
 
Hatuwezi kupoteza Muda na vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku.
 
View attachment 1727209

Ni kawaida kwa watanzania walio wengi kuona suala la kawaida kama halijamgusa moja kwa moja. Hali hii iko hivyo kwa baadhi ya maeneo hapa nchini...
Upotoshaji mkubwa uliofanyika awali umewafanya wengi kuamini covid-19 haipo nchini ilishakimbia na wanaoipata ni wale walioenda nje ya nchi na kuchanjwa!

Aidha wengine wanadhani ni ugonjwa unaowapata viongozi wa juu na matajiri si makapuku na wanyonge walioko mitaani kwetu... zile ndoo na vitakasa mikono vilishakuwa historia
 
HUKU MTAA RAIA WANACHUKULIA POA SANA, WENGINE NDIO KWANZA HAWANA HATA HABARI NAO

WACHACHE UKIWAELEWESHA WANAELEWA
 
mtaani kwangu walimuelewa sana JIWE/CHUMA JPM mambo ya barakoa hawataki hata kusikia wanapiga nyungu
 
Mtaani kwangu mm ni kwenye Mwendokasi hamna lolote linalifanyika tunabanana kama kawaida
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom