#COVID19 Je, watu wa mtaani kwako wanachukua tahadhari dhidi ya #CoronaVirus?

#COVID19 Je, watu wa mtaani kwako wanachukua tahadhari dhidi ya #CoronaVirus?

Status
Not open for further replies.
Wapo tu wanaendelea na maisha kama kawaida...

Hakuna cha barakoa wala kuna maji... na hakuna waginjwa...
 
Kiukweli Mwendazake alijua kutuffuruga mana hizi kauli zote za kwamba tuko kwenye wimbi la tatu la huu ugonjwa zinapita huku na kutokea sikio la kule hamna ambaye anachukua tahadhari yeyote aisee.

Kuhusu kuelimisha inakuwa ngumu sababu hamna ambaye utamwambia akubali huku hamna mgonjwa maeneo hayo ambaye imefahamika hasa ana hiyo kirusi.
 
View attachment 1727209

Ni kawaida kwa watanzania walio wengi kuona suala la kawaida kama halijamgusa moja kwa moja. Hali hii iko hivyo kwa baadhi ya maeneo hapa nchini

Je, hali ikoje kwenye mtaa wako?

Watu wanachukua tahadhari au wanapuuzia ugonjwa?

Je, unachukua hatua yoyote kuwaelimisha zaidi?

Wale chawa wa mwendazake wako busy kuwashauri wasichukue tahadhari, hivi wako wanahesabu mafanikio.
 
Corona ya Tanzania ni fake kama bidhaa za kariakoo ukitaka OG nenda ulaya.
 
Upotoshaji mkubwa uliofanyika awali umewafanya wengi kuamini covid-19 haipo nchini ilishakimbia na wanaoipata ni wale walioenda nje ya nchi na kuchanjwa!

Aidha wengine wanadhani ni ugonjwa unaowapata viongozi wa juu na matajiri si makapuku na wanyonge walioko mitaani kwetu... zile ndoo na vitakasa mikono vilishakuwa historia
Nakubaliana nawe Mkuu na kazi ipo hasa kwetu watu wa hali ya chini katika kubadilisha bongo zetu ambazo zilishaishi kwa kuamini hamna hii kitu na hata kama ipo basi ipo kwa ajili ya watu fulani.
 
Mtaani kwangu hakuna tahadhari kabisa.

Shughuli zote za mikusanyiko kama vile kugombea magari,mikusanyiko ya mazishi,mikusanyiko ya sala na kadhalika inaendelea kama kawaida.Mtu mweusi ni Kima aliechangamka!
 
jana nimevaa barakoa mtaa mzma wana ningong'a live kabisa kila napopita nkaona isiwe kesi ngoja niiweke mfkoni tu
 
Hivi Mkuu hayo maombi yanafanyikia wapi? 😀

Mana kipindi kile cha mwanzo kulikuwaga na siku za maombi rasmi au sasa ndo kila mtu anafanyia kwake na nafsi yake?
Bwana anatenda miujiza...... Bi mkubwa mwenyewe anajua korona hamna hapa tz
 
Bwana anatenda miujiza...... Bi mkubwa mwenyewe anajua korona hamna hapa tz
Alitenda kipindi ile ambacho watu walipukutika kwa wingi tena kimya kimya Mkuu.

Angekuwa anajua haipo asingewataka wale sijui walinzi watoke haraka mule ndani pale Mwananyamala Hospital.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom