Je, watu wanavyokutizama ndivyo ulivyo? Au ndivyo utakavyokuwa?

Je, watu wanavyokutizama ndivyo ulivyo? Au ndivyo utakavyokuwa?

Helixir

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2022
Posts
461
Reaction score
1,214
Wakuu habari za mchana,

Heri ya pasaka kwa Wakristo. Kwa ndugu zangu waislamu poleni na swaumu.

Niende kwenye mada husika. Watu hunitizama kama beureucrat, usalama wa Taifa, askari wa PGO au mtu fulani mwenye wazfa mkubwa serikalini au kwenye taasisi Kubwa Kubwa.

Imefikia mpaka hatua vijana wa rika langu au juu yangu kuja kuniomba KAZI na USHAURI wa nini wafanye kwenye Maisha yao kufikia malengo, mtaani hapa pia nimekuwa nikipokea kesi za maafande kuwaonea baadhi ya raia wa hapa, au nikiulizwa unafahamiana na afande Fulani.

Mimi ni dhoofu la Hali kama raia wengine ila hii Hali imekuwa ulinipa Mawazo mda mwingi .. mda mwingine nikifikiria nabaki kucheka hihiii.

Kwasababu ukweli naujua mimi

Je, ni utabiri, ama kuna namna natakiwa nibadilike labda naweza kuwa na wadhifa mkubwa, au ni nini haswa?

Wajuvi mnisaidie kama sijaeleweka nakaribisha maswali Ili nieleweke na mimi nipate kujielewa.

NB: MFUKONI SINA HATA NDURURU
 
unaposema watu una maanisha nini labda
Raia Jamii inayonizunguka, siyo ninapoishi hivi sasa hata nilipotoka mambo ni hivyo hivyo , yaani nahusishwa Sana na habari za pesa nyingi, Heshima , Na nyadhfa Kubwa Kubwa.
 
Kuna namna hivi watu (wasiokufahamu) wanaweza kuku-judge kutokana na appearance yako hasa ya mavazi, personality na character pia.
Hivi vitu vinawafanya watu wengi kuchukuliwa ndivyo walivyo kumbe sivyo and vice versa hasa katika jamii inayokuzunguka na isiyojua background yako!

Mara nyingi kwenye jamii na hata hapa JF wananichukulia msomi, mwanachuo (hata mwenye degree) au mwinjilisti kutokana na namna nilivyo kwa wao, kumbe ni STD 7 leaver!

Hii ni kutokana na kwamba, watu wameshazoea kwamba, mavazi fulan huvaliwa na watu fulani etc...

Kwa wewe mtoa mada, pengine una vi-element zinazofanana na kundi la watu unaochukuliwa na jamii kuwa upo.

Kwa mantiki hiyo, hapo kuna mambo mawili. Either kama umechelewa basi hivyo ndivyo ulitakiwa uwe au hivyo ndivyo utakavyokuwa!
 
Lkn pia sauti yako ya ndani (the inner voice) inakuambiaje? Hiyo pia ina nafasi ya kukutabiria utakavyokuwa...
 
Watumishi wa Mungu wanasema usikatae namna watu wanavyokuona (namna nzuri) maana Kuna kitu kipo ndani yako ambacho wao hukiona hata kikiwa bado ww hujakiona.

Pia kuna namna kikawaida jamii hukuona ambayo ni tofauti sana na wewe ulivyo. Kwahiyo kama wanakuona hivyo basi in sh allah mapenzi ya Mungu yatimzwe juu yako.
 
Back
Top Bottom