Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
- Thread starter
- #21
Tunajaribu kuukomesha udhalimu huu, tukikaa kimya, basi tujue kuwa kesho ni zamu yetu......Sina nia ovu wala sifurahii vitendo vya kidhalimu, lakini najaribu kuona hizi harakati manufaa yake ni nini?
kwa sababu Tito Magoti siku kadhaa nyuma alikuwa akishiriki hashtag freeIdrissaSultan leo ni yeye.
hakuna unafuu watu wanasombwa tu
Hebu tujikumbushe, alitekwa Saanane. Watu tukaamua kukaa kimya, hadi hivi Leo haijulikani kama Saanane bado nzima. Watekaji wake bado ni watu wasiojulikana...........
Akatekwa Azory Gwanda, watu tukaamua kukaa kimya, hatujui hadi hivi Leo kama Azory bado yu hai. Watekaji wake bado ni watu wasiojulikana.............
Ametekwa mwanamuziki Roma Mkatoliki, watu tukaamua kukaa kimya, baadaye Bashite "akatutabiria" kuwa Roma Mkatoliki ataachiwa na watekaji wake siku ya Jumapili na kweli ilipofika Jumapili tukaona Roma akiachiwa huru. Watekaji wake bado ni watu wasiojulikana..........
Ametekwa Mfanyibiashara maarufu Mo, tukaambiwa na Bashite kuwa ametekwa na wa-South Africa, hatimaye Mo akaachiwa. Bado watekaji wake ni watu wasiojulikana............
Hivi tutaendelea kukaa kimya hivi hadi nchi nzima tuwe tushatekwa?