Je, wawafahamu kwa majina Mamajusi waliomsaliti Mfalme Herode na kumnusuru Yesu kuuawa na Mfalme huyo?

Je, wawafahamu kwa majina Mamajusi waliomsaliti Mfalme Herode na kumnusuru Yesu kuuawa na Mfalme huyo?

Hawakujiongeza Bali walionywa kupitia ndoto
Ok.sasa baada ya kuonywa si ndio wakajiongeza, wangapi wanaonywa na bado hawatii maonyo. Wanaendelea na mambo Yao/ maagizo ya mabosi wao ili wawafurahishe na kupata nafasi nzuri. Unadhani kwenda kinyume na mfalme ni kitu kirahisi tu
 
Baltazary, Merichioly na Gasper - Haya ndio majina ya MamaJusi watatu waliokuwa maarufu kwa kusoma nyota na walipoona Nyota mbali walimwambia mfalme Herode kuwa Hiyo ni ishara kuwa aliyezaliwa atakuwa mtu mkubwa - Mfame, Mtawala etc .

Hivyo Herode aliwaambia wakamuone mtoto wakirudi wampe taarifa Ili na yeye aende, jamaa wakajiongeza maana walishagundua nia ya Herode ilikuwa ni kumuua mtoto Yesu, walipofika walimsujudia wakampa zawadi wakasepa zao kurudi kwao kwa njia nyingine, wala hawakumfahamisha bwana Mkubwa Herode.

Story hii inatufundisha mambo mengi sana, hata katika maisha ya Sasa.
Baada ya kumsujudu kabla hawajaondoka roho mtakatifu akawajia kwenye maono na wakaelekezwa kuwa warudi kwa njia nyingne.

Shukran mkuu kwa story fupi na nzuri
 
Mimi zamani nilikuwa najuwa mamajusi ni Akina mama,ila nilikuwa sijui wanajishughilisha na nini akina mama hao
Hata mimi nilikuwa najua ni akina mama,sasa nashangaa kumbe walikuwa ni kina Gaspar[emoji3]
 
Mkuu Hayo Majina Umeyatoa Wapi Majina Ya Mama Jusi Ni Haya Mmoja Aliitwa Meru, Horu, Lunu
Inawezekana nimechanganya ila hao watatu niliowataja ndio waliomtembelea Yusuphu na Mariamu baada ya Mariamu kumzaa Yesu Kristo. Waliompelekea Manemane, Uvumba sijui na nini kingine

Ndio wanaitwa Magi.
 
Baada ya kumsujudu kabla hawajaondoka roho mtakatifu akawajia kwenye maono na wakaelekezwa kuwa warudi kwa njia nyingne.

Shukran mkuu kwa story fupi na nzuri
Kumbe Roho Mtakatifu alikuwepo kabla ya Kristo!?
Na huyu aliyekuja baada ya Yesu kupaa n Nani
 
Haya majina umeyapata wapi? Hayamo kwenye Bible
Acha uvivu Mkuu jisomee vitabu na nenda mitandaoni ukasome. Usishinde kwa wachungaji wanaogawa maji na mafuta hutaweza kujua mambo haya mkuu.
 
Acha uvivu Mkuu jisomee vitabu na nenda mitandaoni ukasome. Usishinde kwa wachungaji wanaogawa maji na mafuta hutaweza kujua mambo haya mkuu.
Niwekee hapa kitabu kimoja chenye hayo majina nisome meku
 
Kumbe Roho Mtakatifu alikuwepo kabla ya Kristo!?
Na huyu aliyekuja baada ya Yesu kupaa n Nani
"Hata mimba ya Yesu ilitungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu', yaani hapo mtani ndo utajua hujui
 
Siyo kweli mkuu.

Mamajusi kwa leo ni wanajimu.
Kuna biblia toleo moja la King James wamewaita "the magi" yaani kifupi ni wachawi.

NASA hakuna wasoma nyota.Kuna watafiti wa anga za mbali tu.
Hapana,mamajusi ni wataalamu wa mambo ya angani yaani nyota na vinginevyo kwa lugha ya sasa wangeitwa astrophisicians,kwa ulimwengu wa leo uanawapata NASA na mashirika mengine kama ESA (European Space Agency),hapa nchini kwetu sidhani kama tuna kitengo hicho.
 
Hawa ndio wenyewe Sasa, Kila mmoja alifariki na zaidi ya miaka 100. Kesho ntakuja na story fupi ya Kila mmoja
IMG-20220107-WA0020.jpg
 
Back
Top Bottom