AI BRAINFULL
JF-Expert Member
- Oct 31, 2019
- 2,122
- 5,319
Mm nahis kispanish+kitaliano+kireno na kifaransa ndio kimeunda kilatini
Ngoja pia nimpe shavu Mbaga Jr.secretarybird
Haya yanakuhusu kabisa, kula ugali wa kono moja kwa picha ya samaki
Ni sawa na kinyakyusa na kindali!Hapo ongezea na kiitaliano!....mm nahisi hizi lugha tatu kuna vitu vingi wanaelewana anaejua zaidi atujuze
Wakuu,
Kwa wale wanaozijua lugha hizo mbili naomba mnisaidie.
Mimi sio mzungumzaji wa lugha yeyote kati ya hizo ila naweza kusema kwamba naelewa baadhi ya maneno au sentesi sababu nimekuwa nikifuatilia sana nyimbo za zinazoimbwa Kihispania, katika harakati za kujua maana ya nyimbo hizo nikajikuta najua maneno mengi na hata matamshi na kuna kipindi nilianza kusoma mwenyewe online kuanzia spanish alphabet,salamu, namba, siku za wiki nk, kwahio ninaulewa kiasi.
Kadri nilivyoendelea nikaanza pia kupenda nyimbo za Kireno(Portuguese) ndio nikaanza kugundua pia naelewa baadhi ya maneno ya kireno kwa kuwa yanafanana na Kihispania
Mfano
Que tal? - how are you, whatsup
Como estas-how are you
De nada-you are welcome
Por favor(please)
Adios-Goodbye
Amor-Mpenzi
Amigo-rafiki
Spanish - Hola/portuguese-Ola'=Hello or Hi
Na mengine mengi ambayo yanakaribiana kama habari za asubuhi, mchana, jioni.
Je Wazungumzaji wa lugha hizi mbili wanasikilizana? maana hizi lugha zinazungumzwa nchi tofauti na mabara tofauti?
Asante.