Je, WCB wanahusika kumhujumu Ali Kiba you tube, views kuganda?

Yeah ni kweli na kwa taarifa yenu Harmonize ana Masters Degree ya IT sasa huyu jamaa ndio master wa figisu zote zinazohusu views za Kiba.
 
si tuliwauliza juzi mkasema analounge bidhaa kanunua airtime siku nzima walipokua wanampamba msitafute mchawi ni nani mziki wa saizi unataka bidii sio ukongwe wala maneno
 
Yeah ni kweli na kwa taarifa yenu Harmonize ana Masters Degree ya IT sasa huyu jamaa ndio master wa figisu zote zinazohusu views za Kiba.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Naskia huyu ame zi stall views kwenye fixed number hata ukienda kuangalia zinabaki pale pale zilipo
 
Diamond anahusika moja kwa moja.
 
Teh teh teh Diamond mtoto mbaya sana yule dooh
 
inayoonekana yale maswala ya kununua views yamemgharimu maana juzi katoa wimbo masaa 4 tu views laki tano nazaidi
 
Juzi nilisema wimbo huu ukifikisha views 1M ndani ya siku tatu najivua uteam WCB
 
Tunaomba Mange aingilie kati
 
Wimbo aliotoa Ali Kiba hauna ladha. Wengi walienda kuangalia ameimba nini. Nimeusikiliza kwa sekunde tano na sikupata mshawasha wa kuendelea kupoteza MB zangu kuusikiliza.
Ushauri tu, ni bora Ali Kiba atafute kazi nyingine ya kufanya astaafu mziki kwa heshima. Alishafika peak sasa ana drop kwa kasi ya mwanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…