Je, wewe ni chanzo cha furaha kwa watu wengine?

Je, wewe ni chanzo cha furaha kwa watu wengine?

Itovanilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
2,314
Reaction score
5,150
Wasalaam wanajamvi, hope mu wazima

Leo nimeona nigusie jambo moja ambalo Kila kiumbe chini ya jua anapendelea kuwa nayo. FURAHA naam FURAHA ile hali unayoipata mara baada ya kufanyiwa au kupewa kitu kizuri

Ni vile unasaini wakati wa kupokea mshahara,au kukubaliwa maombi ya kazi ni wakati ambao mishipa na viungo vingi vya mwili hu relax

Vyote hutengeneza furaha

Ulishawahi kupewa dhamana iwe mahakamani/mahabusu na ikakubalika? Yaani mwenyewe unajiona kabisa hapa siponi,lakini mwenyezi MUNGU anajalia,vipi kuhusu furaha yake. Hata unapotongoza,halafu unaona kabisa mhusika anaelekea huwa unajisikiaje?

Ni machache kati ya mengi ambayo huleta amani ya moyo.lakini lengo la mada Ni kwamba.....@..si tu ufurahi wewe tu,ila unapaswa kuwa chanzo Cha FURAHA kwa wengine

Maamuzi ya kupiga muziki mkubwa hususan maeneo ya uswahilini Ni ushahidi tosha kwa muhusika anapata vibe la kutosha lakini vipi wagonjwa,na wenye shida mbali mbali ambao huenda ikawa Ni kero kwa wakati huo,tujitathmini

Pia Kuna ile hali ya kutoa msaada iwe kwa mtu mmoja mmoja au kundi la watu usipokuwa makini,unaweza kugawa bahasha za hela zenye thamani ya milion Mia tano.na ukasababisha huzuni kubwa kwa watu tofauti na malengo yako

Kwanini?

Ni kwa vile umeshindwa kutumia hekima na busara kwenye uwasilishaji wa msaada wako. Kumfurahisha mtu sio lazima,bali ni uwajibikaji ambao utakuletea Faida na furaha baadae e.g kumridhisha mpenzi wako.huenda ikamfanya asiwaze kuchepuka,basi Ni faida kwako

Kufanya kazi kwa bidii unaweza kuwafurahisha waajiri/mabosi wako,lakini pia waweza kupata faida ikiwemo kupandishwa daraja/cheo au mshahara. Tengeneza furaha Iwe ndoa, familia na hata uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzako maofisini/makazini kwenu.

Swali:Je umejitengenezea msimamo upi ili kuwa chanzo cha furaha kwenye jamii inayokuzunguka?

Tiririka kwa Faida ya wengi...

Pia muwe na wakati mwema wanajamvi.
 
Tenda haki, haijalishi kwa nafasi uliyopo na hakika utakuwa umeleta furaha kwa anayestahili.

Furaha ni matokeo ya haki. Lakini kumpokonya mtu haki yake na kumzawadia mwingine ni dhulma. Furaha imeenda kwa asiyestahili. Lakini ni furaha isiyo na amani ndani yake.
 
Tenda haki, haijalishi kwa nafasi uliyopo na hakika utakuwa umeleta furaha kwa anayestahili.

Furaha ni matokeo ya haki. Lakini kumpokonya mtu haki yake na kumzawadia mwingine ni dhulma. Furaha imeenda kwa asiyestahili. Lakini ni furaha isiyo na amani ndani yake.
Fact
 
Nimesoma kichwa cha habari tu.yes ni chanzo cha furaha tena iliyotukuka..lakini bange ikiingizwa katikati hapo..ni chanzo pia cha timbwili
 
Mimi naona wakati mwingine huzuni yako au matatizo yako pia inakuwa sababu ya wengine kufurahi

MÊmENtO HoMO
 
Back
Top Bottom