Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Katika ulimwengu kila mtu analo jukumu na nafasi yake.Kutambua nafasi yako kunaweza kukuwezesha kufikia mafanikio kwa muda sahihi na kufurahia maisha.Katika biashara na maendeleo huwa kuna aina mbalimbali za watu ambao hushiriki katika kupeleka gurudumu la maendeleo mbele.
Kuna kundi la Wafanyakazi(Labour Force)Kuna kundi la Wajasiriamali(ENtrepreneurs)na kundi la Wawekezaji(Investors.)
Kila kundi linayo majukumu na mahitaji yake.Mfanyakazi anataka Mshahara,Muwekezaji na Mjasiriamali wanahitaji Faida.Pamoja na hayo yote vyanzo vya faida vya hawa waiwili(Mwekezaji na Mjasiriamali ni tofauti)Mjasiriamali anataka faida anayopata kutokna na utendaji wakati Mwekezaji anataka faida kutokana na kiwango cha uwekezaji wake.
Mara nyingi watu hushindwa kutambua iwapo wao ni wafanyakazi tu au ni wajasiriamali ama ni wawekezaji.Leo tunajadili jinsi ya kutambua iwapo wewe ni Mfanyakazi/Mjasiriamali/Muwekezaji kwa kutumia vigezo kadhaa kama ifuatavyo:
Niwatakie tafakari njema

- Je wewe unaona Fursa wakati gani?Je unaona fursa wakati ukiwa na uwezo wa kuitumia au wakati ukiwa huna uwezo wa kuitumia?
- Je unaona RISKS(Hatari) wakati gani?Je ni wakati una uwezo wa kuzishinda au wakati ambao huna uwezo wa kuzishinda
- Je matumizi yako ya Fedha yakoje?Una kiwango maalum cha matumizi au unatumia mpaka iishe?
- Je kiwango kikubwa cha Pesa ambacho umewahi shika ni kiasi gani?Je ulizitumiaje?
- Je kipi rahisi kwako wewe kukifanya?Kumuelekeza mtu cha kufanya au kufuata maelekezo?
- Je unapofanya jambo gumu matarajio yako huwa nini?Kushindwa au kufanikiwa?
- Unapokuwa na matarajio ya kushindwa kiwango chako cha bidii kinaongezeka au kinapungua
- Je umewahi fikiria kuanzisha biashara?Ulihitaji ni kwanza ili uanzishe biashara?
- Je umewahi kuandika mchanganuo wa biashara?
- Je aina ya marafiki ulio nao ni wa namna gani?
- Je aina ya maeneo uanyotembelea ni ya aina gani?
- Je ukiona duka la mtu limejaa wateja huwa unawaza nini?Je ukiona haina wateja?
Niwatakie tafakari njema