Je, wewe ni muhanga wa Gharama za spea za Hybrid Cars?

Je, wewe ni muhanga wa Gharama za spea za Hybrid Cars?

Sapre zote za hybrid ziko mimi niko Japan kama unataizo lolo la spare ya Gari lolote nicheki
 
Hello my good people, natumia gari ya hybrid (Toyota Prius) sasa juzi nilipatwa na changamoto moto ya kuharibikiwa na auxiliary electric water pump inayo zungusha maji ya kupoza inverter na gearbox.

Ee bwana ee kipampu kidogo sana but jamaa wakanipa quotation ya bei eti laki tano nikashangaa, nkauliza why that price wakasema wananunua kwa price ya juu huko vinako toka, wakesema used ni 450k bado nikashangaa, yaan bei ambayo unanunulia gear box ya Gari ndo unanua pump.

But just kwakua mie na DIY person (mtu ninae tengeneza vitu vyangu mwenyewe) ikabidi nitafute solution ya kupata hii pump kwa bei rahisi, kumbuka hii pump ni ya umeme yaan kazi yake ni kuzungusha maji tu nothing else, so meaning any electric pump ili mradi ni ya volts 12 itafanya same job. So nakenda mtandaoni (kikuu) nikaagiza pump ya dc 12 kwa shinlingi 17,000( elfu kumi na saba) ambayo ntaisubiri na ntakuja ku install, but wakati nasubiri hii pump, nimepata auxiliary electric pump nyingine pale tandale inaYofungwa kwenye vw, kwa 20,000 nimefunga na maisha yamekua safi. Kabisa.

Sasa nini maana ya huu uzi?
Ni hivi ukiwa ni mtu mdadisi na unafatilia vitu na you take your time kutafuta information basi costs nyingi za ku maintain hybrid car uzipunguza, yet hybrid car ina less maintenance costs kwakua ina less regular services ukilinganisha na Gari yakawaida.

But kwakua kibongo bongo wstu hutumia ignorance ya mteja kumpiga bei basi unaweza ichukia gari.
===
Haya mambo yanawork kwenye toyota tu. Na na baadhi ya wajapani labda.

Huwezi kufanya hivi kwenye gari yoyote ya mzungu.

Nililetewa Amarok imeua pump km hiyo, imeshajiset kwenye limp mode haivuki 80kph.

Aliagiza pump ya fake nje, kuja kufunga iligoma.
 
Back
Top Bottom