Je, WEWE umesoma RASIMU YOTE (siyo sehemu) ya katiba ya JMT ya 2013?

Je, WEWE umesoma RASIMU YOTE (siyo sehemu) ya katiba ya JMT ya 2013?

Soki

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
1,303
Reaction score
279
Kwanza, ikiwa umeisoma rasimu YOTE (na siyo sehemu, wala kurukaruka), naomba uanze kwa kusema (andika) NDIYO. Baada ya hapo jaribu kueleza unaionaje.

Tatizo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba tutakuwa tunajadili RASIMU hii na watu ambao hawajaisoma YOTE kwa utulivu na matokeo yake tunayafahamu.

Nimegundua watu wengi wanapenda kuongea sana lakini hawapendi KUSOMA na kufanya japo research ndogo, ili mchango wao utokane na utafiti japo mdogo.

Mbaya zaidi ni kwamba wengi hawaisomi kwa UVIVU TU, na siyo kwamba hawana muda!

MIMI NIMEISOMA RASIMU YOTE KWA UTULIVU NA NIMEJIFUNZA MAMBO MENGI MNO - na mojawapo ni kwamba jambo la kwanza la muhimu liwe ni KUISOMA RASIMU YOTE na siyo nusunusu!

Karibuni!
 
Na maswali mengi watu wanayouliza majibu yamo humohumo. Kwa mfano mtu mmoja humu alikuwa anauliza nchi washirika zinazotajwa katika rasimu ni zipi jambo ambalo limeelezwa ndani ya rasimu
 
una soft copy utupiemo tuisome wote coz mie hata sijui inauzwa wapi. Haijafichwa kama mikataba?!
 
Ni kweli,watu wanajadili pasipo kuisoma yote! kwa mfano walikuwa wanasema kuwa kutakuwa na rais wa Tanzania bara na Rais wa Zanzibar kumbe kutakuwa na Magavana wa pande mbili na Rais wa Shirikisho.Pia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekufa rasmi na badala yake limezaliwa shirikisho la Tanzania.
 
una soft copy utupiemo tuisome wote coz mie hata sijui inauzwa wapi. Haijafichwa kama mikataba?!

Ipo mkuu. Niliikuta humuhumu jamvini. Hebu itafutetafute
 
una soft copy utupiemo tuisome wote coz mie hata sijui inauzwa wapi. Haijafichwa kama mikataba?!

Mkuu Said hiyo ndio rasimu ya katiba mpya!

Nimesikia watu wakishabikia suala la limit ya cabinet kuwa sio zaidi ya 15 na kwamba imepunguza mzigo, ukweli ni kwamba huenda mzigo ukawa umeongezeka zaidi kwa kuwa imependekeza serikali 3 na hiyo ya cabinet isiyozidi 15 ni kwa JMT, sio SMZ wala Tanzania bara (Tanganyika). Binafsi naona kama haiwezekani kuwa na serikali moja ni bora tungebaki na serikali mbili tu kama zamani.

Otherwise, kwa kiasi kikubwa naona ni nzuri ukiondoa kasoro ndogo kama kuta Tanzania bara badala ya Tanganyika nk. Nimependa kuingizwa kwa maadili na miiko ya uongozi wa umma. Ikiwa ni pamoja na kuzuia mtumishi wa umma kufungua na kuendesha akaunti katika benki nje ya nchi, ibara 15-(2)(a) uk 9, sifa za speaker wa bunge na naibu wake, kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi nk.

Kwa kiasi kikubwa imejaribu kugusa vilio vya watanzania wengi.
 
Soki ulichobaini ni ukweli mtupu. Mambo yale yale ya mikataba ya madini na gesi! Wabongo tumejenga utamaduni wa kuwa wavivu kusoma documents hata na vitabu vya kawaida. Tunataka mtu mwingine asome kasha atueleze kwa muhtasari - ambamo katika mchakato huo tunapotoshwa na kuuziwa mbuzi kwenye gunia!! Huu ni mfano hai - masuala na maswali mengi yanayoulizwa humu jamvini yanaoenesha the so called Great Thinkers do not want to read the document by themselves. Je, tunaweza kubadilisha utamaduni huu kwa kusisitiza mabadiliko ya mitaala katika ile wizara ya Mhe Mulugo kusudi kizazi kijacho kisiwe na uvuvi wa kusoma kama sisi???
 
MPIGA ZEZE umenena! Tatizo la kusoma ni kama donda ndugu!
Nimejaribu kuongea na baadhi ya watu ambao wamesoma kiasi fulani na kugundua hata hamasa ya kuisoma rasimu hii hawana. Lakini eti bado wanapenda kutoa maoni! Yaani ni kichekesho!!
 
Last edited by a moderator:
mkuu usiogopeshe wadau,acha watu waseme walichokiona. Kama umesoma rasimu yote umefanya vema zaidi,after all watz hatupendi kusoma kurasa nyingi,labda abstract. Sijaisoma yote lkn,kwa vipengele vichache nilivyopitia neno Tanganyika sijaliona.
 
Mkuu babajnr unasema naogopesha wadau?! Hapana! Naelezea jambo la muhimu sana - kuisoma rasimu yote, na nimedokeza ukweli kwamba tuna tatizo kubwa - KUSOMA!

Lengo langu ni kuhamasisha kuisoma!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom