Je wewe unasemaje khs maoni haya?

MIUNDOMBINU

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2010
Posts
465
Reaction score
96
Kuna baadhi ya watanzania wanatamani bora tupigane vita ya wenyewe kwa wenyewe ili tuweze kuondokana na hili wimbi la viongozi warafi(mafisadi) ambao kila kukicha wanazidi kuongezeka.pia kuna kundi jingine wao wanatamani utawala wa wakoloni urudi tena, hawa nao wanasabau zao wanalalamikia ugumu wa maisha, wanasema bora enzi za mkoloni kuliko jinsi mambo yalivyo kwa sasa.pia kuna baadhi wanasema kuwa tz haina uhuru (haijawahi kupata uhuru) bali uhuru uliopo ni wa watu wachache tu, hao ndo wanaofaidi matunda ya uhuru.je wewe unasemaje khs maoni haya ya baadhi ya ndugu zetu?.
 
Kwa oni la kwanza, napingana nalo moja kwa moja, best vita ya cc kwa cc ni balaa wala haifai, labda kama wanamaanisha kuwa JWTZ liwapindue hawa mafisadi na liongoze kwa muda wa miezi sita tu halafu liitishe uchaguzi huru lakini baada ya kukipiga marufuku chama cha matumbo. Naafiki na niko tayari kuchangia damu kwa wapiganaji wa jeshi letu.

Lile la pili bado nalo napingana nalo labda kama wakoloni watatoka nchi ambazo hazikuwahi kuwa wakoloni kama Cuba na Japani nakubali lakini waje kama raia wa nchi hii ili tuwatambue safi tu. Lakini kimsingi hakuna mfumo wowote wa kikoloni wenye huruma kwa wanaokuwa colonized so for this A BIG NO.
Kwa la tatu, ni kuwa Tanzania imewahi kuwa huru na tulipata uhuru mwaka 1961 na baadae tukawa jamhuri. Kwa kipindi cha mzee kifimbo tulikuwa nchi huru. Badae wawili walomfuata wakatuingiza katika uhuru wa bendera. Na Hii awamu ya nne ndo imeshindilia msumari kwenye kidonda kwa kutufanya tuanze kuuzana kama enzi za waarabu ambapo waliwarubuni machifu ili wawauze watu wao. So hawa mnaowaita viongozi wa awamu ya NNE ndo hata wametuondoa kwenye uhuru wa bendera na kutuachia mlingoti tu bila identity yoyoye. BEST VITA BALAA USIOMBE!
 
Kuna haja gani ya kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kutiana ziki ya roho bure, na hata tuseme watu wamekubali kupigana hivyo vita fikra zako atakaeumia ni nani,ukichukuli mfano hizo nchi zinazipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hao "war lords" na famili zao vinawagusa?
Vita pigana na akili yako, ww ndo unaekubali kuwa chama cha Mapinduzi kidumu milele, ni wewe hutaki kuamini kuwa CCM imeshachoka na haina haja tena kuambiwa sababu unaziona mwenyewe kwa macho. Ni wewe unaetakiwa kupigana "civil war" na akili yako kuwa kuichagua CCM miaka mitano iliyopita hujapata chochote na njaa,ujinga na maradhi vimemuandama babu yako kabla ya uhuru, baba yako badala ya uhuru na ww mwenyewe mpaka leo bado unataka uletewe nabii aje akwambie "...umasikini unaufuga akilini mwako...", time has come for...kieleweke kuwa kuwepo na kutokuwapi CCM hakuna tofauti yoyote,labda kitakapokuwa hakipo inaweza kuwa afueni.
 
Lakini Itachukua mda mrefu mpaka watu kuweza kubaini kuwa wananyonywa na CCM, Make walio wengi hawajui kuwa wananyonywa.
 
Mimi nasema Nchi iendeshwe Kijeshe Tu na Tutaendelea, Pia mi nasapoti kabisa kukitokea Vita Watu watafahamu na viongozi walafi wote watang'oka,

Ila Bora Kijeshi tu kwa maana vita Duh
Mi nasema Kijeshi tu wakuu.
 
Ndugu yangu wewe unayesema hivyo naomba unionyeshe kitu kimoja ulichokifanya kwa maendeleo yako wewe binafsi kabla ya kwenda kwa wengine unaweza kukuta hata vikao vya maendeleo ya familia yako hufanyi kazi kwenda bar kupiga soga , hata vikao vya mitaani maendeleo kwa ajili ya mitaa yenu kuendi leo hii unaota uhuru uhuru utoke wapi kama wewe mwenyewe hujaamua kuwa huru na kusimamia uhuru huo kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kuanzia kwenye jamii zako mitaani , shuleni , makazini au popote unapoenda ?
 
Mimi nasema Nchi iendeshwe Kijeshe Tu na Tutaendelea, Pia mi nasapoti kabisa kukitokea Vita Watu watafahamu na viongozi walafi wote watang'oka,

Ila Bora Kijeshi tu kwa maana vita Duh
Mi nasema Kijeshi tu wakuu.

Jeshi gani unalosema .majeshi ya nchi nyingi za afrika yako politicised zaidi kuliko hata wanasiasa wenyewe. Umeshasikia walimu manesi wangapi wanastaafu wanapewa ukuu wa wilaya.?

Kama Jeshi letu lenyewe halina NIDHAMU. Mfano mdogo tu ni finacial disclipine ya Fedha na utunzaji na maitanance ya resurces nyingine kama magari. sasa wakipewa rungu la kuntrol hazina si itakuwa kichekesho. Lifespan ya basi la jeshi la dar na lifespan ya basi na mtu wa kawaida ikoje?

Unashangaa with Scarcity of reoucres tulizonazo priority zetu haziendani nayo. Hata wakija WAKOLONI labda watakachofanya ni kubadilisha SYSTEM(MFUMO) amabo hata sisi wanachi tukiamua tunaweza.

Vita sio solution pia bcs at the end ya hivyo vita utahitaji si tu UTAWALA BORA bali MFUMO wa huo utawala kufanya kazi .kwa hiyo tatizo halisi letu ni MFUMO. mengine yote ya UFISADI, NK ni EFFECT za TRUE PROBLEM


TRUE problem sio Utawala hata akija obama na kikosi chake cha kazi katika MFUMO uliopo atajikuta naye ni corrupt . TRUE problem ni SYSTEM.
 
Kama nilivyokuwa nikisema katika thread nyingi zilizopita tatizo la Tanzania ni kuwa na watawala wasiopenda kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na hii tumeathiriwa sana na watawala hawa kuwa karibu na wahindi. India kwa miaka kama 20 iliyopita hawakujali sheria na ndo maana pamoja na ukubwa wa nchi lao bado ni maskini. Alipoingia waziri mkuu Manimohan Singh kidogo amejaribu kuhamasisha watendaji kufuata sheria na kujaribu kupunguza rushwa ndo kidoogo unaona india nayo inajikongoja kuifuata uchina lakini wanahitaji miaka 30 zaidi ili waifikie china.

Tanzania tumejaliwa raslimali za kutosha kututajirisha lakini tatizo ni kutokuwa na watawala/viongozi wenye maono ya kuendeleza nchi. Tumekumbatia nadhalia ambazo hazitekelezeki kwa hiyo hata tukianza kupigana wenyewe bado jibu la matatizo yetu halitapatikana hivi karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…