MIUNDOMBINU
JF-Expert Member
- Apr 14, 2010
- 465
- 96
Kuna baadhi ya watanzania wanatamani bora tupigane vita ya wenyewe kwa wenyewe ili tuweze kuondokana na hili wimbi la viongozi warafi(mafisadi) ambao kila kukicha wanazidi kuongezeka.pia kuna kundi jingine wao wanatamani utawala wa wakoloni urudi tena, hawa nao wanasabau zao wanalalamikia ugumu wa maisha, wanasema bora enzi za mkoloni kuliko jinsi mambo yalivyo kwa sasa.pia kuna baadhi wanasema kuwa tz haina uhuru (haijawahi kupata uhuru) bali uhuru uliopo ni wa watu wachache tu, hao ndo wanaofaidi matunda ya uhuru.je wewe unasemaje khs maoni haya ya baadhi ya ndugu zetu?.