Je Wizara ya Elimu imekosa Meno kuhusu Kasumba ya Madarasa ya Mitihani?

abura90

Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
12
Reaction score
1
Kwa zaidi ya Miaka 10 sasa ukipitia Majukwaa mbalimbali humu utakutana na Malalamiko ya Wazazi na Walezi kuhusu Maamuzi kadha wa kadha yanayotolewa na Shule Binafsi nchini ambayo yaaathiri Malezi na Makuzi ya Wanafunzi lakini Wizara ya Elimu ambayo inabeba dhamana ya kusimamia utoaji wa elimu nchini imeshindwa kuchukua hatua .

Kabla sijaenda moja kwa moja nitoe pongezi zangu kwa Wizara ya Elimu na Wadau wote kwa kuja na Sera Mpya ya Elimu ambayo kama itatekelezwa vizuri basi tunatatajia vijana wetu watakuwa na maarifa yanayohitajika katika Ulimwengu wa Karne ya 21 ya Sayansi na Teknolojia. Kipekee niwapongeze kwa hatua iliyochukua ya kuondoa utaratibu wa TOP TEN schools ambao kimsingi haukuwa na tija yoyote bali kuzipa Shule za Binafsi mwanya wa ukandamizaji wa Haki za Msingi za Watoto pamoja na Kuiba Mitihani ili kupata nafasi ya kuingia katika TOP TEN ili kuwavutia wazazi kuwaandikisha wanafunzi wengi.

Pamoja na jitihada hizo ni wazi kuwa Serikali na dhamira yake ya kila mwanafunzi kupata elimu ya Msingi (yaani kufikia kidato cha 4 kwa mujibu wa Sera Mpya ya Elimu) bado imeshindwa kudhibiti kasumba ya Madarasa ya Mitihani hususani Shule za Private kuja na mipango ambayo kImsingi inakinzana na Makuzi na Malezi ya Watoto.

Kwa miaka mingi ukipitia threads mbalimbali humu jukwaani utagundua kumekuwa na lawama kutoka kwa Wazazi kuhusu Suala la Muda wa Ziada kwa Watoto wa Madarasa ya Mitihani ambalo hupelekea watoto kushindwa kupata muda wa mapumziko au kujishughulisha na shughuli nyingine za kijamii.

Ifuatayo ni Barua kutoka katika Shule Moja jijini Dar Es Salaam kwa Wazazi na Walezi ambayo imetumwa mwezi Agosti 2026;

MPITO WA DARASA LA TANO KWENDA DARASA LA SITA – 2026/2027

Mzazi/Mlezi Mpendwa,

Kufuatia maboresho ya Mtaala wa Tanzania, wanafunzi wetu wa sasa wa Darasa la Tano wataingia Darasa la Sita na watachukuliwa kama darasa la watahiniwa , kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wao wa Kitaifa wa Darasa la Sita.

Kwa hiyo, kuanzia Septemba 2026, wanafunzi wa Darasa la Tano watafuata programu ya masomo iliyoboreshwa, inayofanana na programu itakayotumika kwa wanafunzi wa Darasa la Sita wanaohamia hatua inayofuata. Programu hii inalenga kuwapa wanafunzi maandalizi na msaada wa kutosha kwa ajili ya mitihani yao ya kitaifa ijayo.

Ili kuwezesha wanafunzi kushiriki kikamilifu katika programu hii iliyoongezwa, shule itatoa huduma ya bweni kwa wanafunzi ambao wanaweza kupata changamoto kuhudhuria programu hiyo wakiwa wanafunzi wa kutwa.

RATIBA YA KILA SIKU YA DARASA LA SITA
- Jumatatu – Alhamisi : Saa 12:00 asubuhi – Saa 2:30 usiku
Ijumaa : Saa 5:00 asubuhi – Saa 10:00 jioni
Jumamosi : Saa 2:00 asubuhi – Saa 2:30 usiku
Jumapili: Saa 5:00 asubuhi – Saa 10:15 jioni

Swali ni lini Wizara itaota MENO na kuanza kuchukua hatua dhidi ya tasisi hizi ambazo zinaenda kinyume na Malengo mbalimbali ya Serikali? Inashindwa nini kuchukua hatua kwa Taasisi hizi au Lisemwalo ni kweli kwamba Wamiliki wa Shule hizi ndio Viongozi wa Umma hivyo wanahusika nao kuharibu mifumo kwa kukusudia?
 
Kwani lazima mwanao asome shule yenye utaratibu huo? Au unazuiliwa kumuhamisha.

Wazazi wengi wanapenda huo utaratibu. Wasioridhika huwahamisha watoto wao.
 
Sorry ndugu, una mtoto anayesoma? Shughuli gani za kijamii unazompa?

Watoto wengi hasa wa familia zenye vipato vikubwa na vya kati watoto wao ndio wako private.

Familia hizi wazazi wako busy. Mtoto akifika nyumbani ni michezo na tv siku nzima. Wengine wanashinda na smartphone 24/7.

Wazazi wako busy na utafutaji na watoto ama wanaleana wenyewe au wanapata uangalizi mdogo sana

Kipi bora wabaki shule wajiandae na mitihani au wabaki nyumbani? Ni wazi mifumo yetu inatambua ufaulu wa darasani kama kigezo kikuu cha sorting. Kama nataka mwanangu atambulike kitaaluma lazima nihakikishe anafaulu.

Kuhusu elimu ya jamii, elimu ya vitendo, serikali itakuwa na mda mrefu sana kufanikisha hili. Miaka ya mitihani ni miaka 4 kati ya miaka 11 ya elimu ya msingi, tumia miaka iliyobakia kumfundisha mtoto elimu ya maisha kama unaweza.

Au mtafute mtu maalum wa kumfundisha elimu hiyo kama watu wa kale walivyofanya.

Ziko shule za public zinavoenda na ratiba bila ziada. Je watoto wao wamefanikiwa kuliko wa private? Asilimia ya watoto wa private wanaojua kupambania malengo yao na asilimia ya watoto wa public zinafanana?

Mafanikio huleta mafanikio, kufeli huleta kufeli ( mwenye nacho huongezewa). Mtoto aliyezoea kupata sifuri darasani anajifunza unyonge na uduni, mtoto anaefaulu anajifunza kuwa na viwango vikubwa.

Ndiyo maana asilimia ndogo sana wanaopata sifuri kukuta wametoboa kihalali na wanajiamini.

Hitimisho, Serikali isizuie muda wa ziada iwe private au public. Kuna watoto, walimu na wazazi wanauhitaji mno kwa faida ya mtoto kulingana na mazingira yao. WASIMAMIE SHULE ZISITOE AMRI KIHOLELA KUWA LAZIMA KILA MTOTO AHUDHURIE NA KUCHANGIA MUDA WA ZIADA.
 
Vumilia mkuu.

Kwa sasa ni ngumu hilo kuzuilika. Walimu, wanafunzi na wazazi wamekuwa programmed kuwa Kuna madarasa yanapaswa kukazaniwa zaidi na mengine kuachwa.

Si shule binafsi, si shule teule, si shule za kata, kote mtindo ni mmoja.

Wanafunzi wakiwa kwa mfano form 1, form 3 hawajishughulishi na masomo kihivyo, sababu si darasa la mtihani.

Shule za kata nyingi zimeanzisha utaratibu wa kambi, lakini kambi hizo ni kwa madarasa ya mtihani (hasa la Saba na form four).

Hivyo, kuisha kwa hii mentality labda mfumo wa elimu uondoke kwenye mitihani.
 
Sehemu kubwa ktk elimu imekuwa ni kufundisha namna ya kujibu mitihani. Ndio maana programs nyingi za kufanikisha hili zoezi limewekwa Kwa darasa ya mitihani. Hakuna dhati ya kufundishana maarifa Kwa ajili ya changamoto za Kila siku.
 
Kwani lazima mwanao asome shule yenye utaratibu huo? Au unazuiliwa kumuhamisha.

Wazazi wengi wanapenda huo utaratibu. Wasioridhika huwahamisha watoto wao.
Unamuhamisha unampeleka wapi wakati Shule karibia zote zimeanzisha huu mfumo ikiwemo za Serikali?
 
Vumilia mkuu.

Kwa sasa ni ngumu hilo kuzuilika. Walimu, wanafunzi na wazazi wamekuwa programmed kuwa Kuna madarasa yanapaswa kukazaniwa zaidi na mengine kuachwa.

Si shule binafsi, si shule teule, si shule za kata, kote mtindo ni mmoja.

Wanafunzi wakiwa kwa mfano form 1, form 3 hawajishughulishi na masomo kihivyo, sababu si darasa la mtihani.

Shule za kata nyingi zimeanzisha utaratibu wa kambi, lakini kambi hizo ni kwa madarasa ya mtihani (hasa la Saba na form four).

Hivyo, kuisha kwa hii mentality labda mfumo wa elimu uondoke kwenye mitihani.
Kwa hiyo tumekuwa taifa la kuvumilia hata yale yasiyo sawa
 
Mbaya zaidi pamoja na mambo hayo yote lakini elimu ya Tanzania bado ni ya hovyo ulilinganisha elimu za nchi zingine.
 
Sorry ndugu, una mtoto anayesoma? Shughuli gani za kijamii unazompa?

Watoto wengi hasa wa familia zenye vipato vikubwa na vya kati watoto wao ndio wako private.

Familia hizi wazazi wako busy. Mtoto akifika nyumbani ni michezo na tv siku nzima. Wengine wanashinda na smartphone 24/7.

Wazazi wako busy na utafutaji na watoto ama wanaleana wenyewe au wanapata uangalizi mdogo sana

Kipi bora wabaki shule wajiandae na mitihani au wabaki nyumbani? Ni wazi mifumo yetu inatambua ufaulu wa darasani kama kigezo kikuu cha sorting. Kama nataka mwanangu atambulike kitaaluma lazima nihakikishe anafaulu.

Kuhusu elimu ya jamii, elimu ya vitendo, serikali itakuwa na mda mrefu sana kufanikisha hili. Miaka ya mitihani ni miaka 4 kati ya miaka 11 ya elimu ya msingi, tumia miaka iliyobakia kumfundisha mtoto elimu ya maisha kama unaweza.

Au mtafute mtu maalum wa kumfundisha elimu hiyo kama watu wa kale walivyofanya.

Ziko shule za public zinavoenda na ratiba bila ziada. Je watoto wao wamefanikiwa kuliko wa private? Asilimia ya watoto wa private wanaojua kupambania malengo yao na asilimia ya watoto wa public zinafanana?

Mafanikio huleta mafanikio, kufeli huleta kufeli ( mwenye nacho huongezewa). Mtoto aliyezoea kupata sifuri darasani anajifunza unyonge na uduni, mtoto anaefaulu anajifunza kuwa na viwango vikubwa.

Ndiyo maana asilimia ndogo sana wanaopata sifuri kukuta wametoboa kihalali na wanajiamini.

Hitimisho, Serikali isizuie muda wa ziada iwe private au public. Kuna watoto, walimu na wazazi wanauhitaji mno kwa faida ya mtoto kulingana na mazingira yao. WASIMAMIE SHULE ZISITOE AMRI KIHOLELA KUWA LAZIMA KILA MTOTO AHUDHURIE NA KUCHANGIA MUDA WA ( wazazi wako busy ................mimi ni mzazi mbona siko busy) angalia hoja yako nyingine (watoto wanapata uangalizi mdogo sana.............. Kwa hiyo wazazi hamko busy ila walimu wenye watoto wao ndio wawalelee watoto wenu?)

Sorry ndugu, una mtoto anayesoma? Shughuli gani za kijamii unazompa?

Watoto wengi hasa wa familia zenye vipato vikubwa na vya kati watoto wao ndio wako private.

Familia hizi wazazi wako busy. Mtoto akifika nyumbani ni michezo na tv siku nzima. Wengine wanashinda na smartphone 24/7.

Wazazi wako busy na utafutaji na watoto ama wanaleana wenyewe au wanapata uangalizi mdogo sana

Kipi bora wabaki shule wajiandae na mitihani au wabaki nyumbani? Ni wazi mifumo yetu inatambua ufaulu wa darasani kama kigezo kikuu cha sorting. Kama nataka mwanangu atambulike kitaaluma lazima nihakikishe anafaulu.

Kuhusu elimu ya jamii, elimu ya vitendo, serikali itakuwa na mda mrefu sana kufanikisha hili. Miaka ya mitihani ni miaka 4 kati ya miaka 11 ya elimu ya msingi, tumia miaka iliyobakia kumfundisha mtoto elimu ya maisha kama unaweza.

Au mtafute mtu maalum wa kumfundisha elimu hiyo kama watu wa kale walivyofanya.

Ziko shule za public zinavoenda na ratiba bila ziada. Je watoto wao wamefanikiwa kuliko wa private? Asilimia ya watoto wa private wanaojua kupambania malengo yao na asilimia ya watoto wa public zinafanana?

Mafanikio huleta mafanikio, kufeli huleta kufeli ( mwenye nacho huongezewa). Mtoto aliyezoea kupata sifuri darasani anajifunza unyonge na uduni, mtoto anaefaulu anajifunza kuwa na viwango vikubwa.

Ndiyo maana asilimia ndogo sana wanaopata sifuri kukuta wametoboa kihalali na wanajiamini.

Hitimisho, Serikali isizuie muda wa ziada iwe private au public. Kuna watoto, walimu na wazazi wanauhitaji mno kwa faida ya mtoto kulingana na mazingira yao. WASIMAMIE SHULE ZISITOE AMRI KIHOLELA KUWA LAZIMA KILA MTOTO AHUDHURIE NA KUCHANGIA MUDA WA ZIADA.
Nafuatilia hoja zako na nitakujibu ( wazazi wako busy ................mimi ni mzazi mbona siko busy) angalia hoja yako nyingine (watoto wanapata uangalizi mdogo sana.............. Kwa hiyo wazazi hamko busy ila walimu wenye watoto wao ndio wawalelee watoto wenu?) Hitimisho, Serikali isizuie muda wa ziada iwe private au public ( Serikali inapotoa ratiba ya masomo ina maana haijafanya utafiti wa kina kuhusu muda anaotakiwa kukaa mtoto darasani kulingana na huu mtaala?)
 
Unamuhamisha unampeleka wapi wakati Shule karibia zote zimeanzisha huu mfumo ikiwemo za Serikali?
Umesema vizuri, karibu zote ila sio zote. Maana yake ziko ambazo hazina utaratibu huo.
 
Kupumzika muhimu ili akili iwe sharp, ona paka na simba wanapumzika wanalala sana ili wawe shapu kwenye uwindaji, lakini mbuzi na nyumbu kulala sio sana kila muda wanakimbiakimbia tu.

Kumbukumbu na kuziweka sawa akili inakuja muda ambao umeipumzisha
 
Kwa zaidi ya Miaka 10 sasa ukipitia Majukwaa mbalimbali humu utakutana na Malalamiko ya Wazazi na Walezi kuhusu Maamuzi kadha wa kadha yanayotolewa na Shule Binafsi nchini ambayo yaaathiri Malezi na Makuzi ya Wanafunzi lakini Wizara ya Elimu ambayo inabeba dhamana ya kusimamia utoaji wa elimu nchini imeshindwa kuchukua hatua .

Kabla sijaenda moja kwa moja nitoe pongezi zangu kwa Wizara ya Elimu na Wadau wote kwa kuja na Sera Mpya ya Elimu ambayo kama itatekelezwa vizuri basi tunatatajia vijana wetu watakuwa na maarifa yanayohitajika katika Ulimwengu wa Karne ya 21 ya Sayansi na Teknolojia. Kipekee niwapongeze kwa hatua iliyochukua ya kuondoa utaratibu wa TOP TEN schools ambao kimsingi haukuwa na tija yoyote bali kuzipa Shule za Binafsi mwanya wa ukandamizaji wa Haki za Msingi za Watoto pamoja na Kuiba Mitihani ili kupata nafasi ya kuingia katika TOP TEN ili kuwavutia wazazi kuwaandikisha wanafunzi wengi.

Pamoja na jitihada hizo ni wazi kuwa Serikali na dhamira yake ya kila mwanafunzi kupata elimu ya Msingi (yaani kufikia kidato cha 4 kwa mujibu wa Sera Mpya ya Elimu) bado imeshindwa kudhibiti kasumba ya Madarasa ya Mitihani hususani Shule za Private kuja na mipango ambayo kImsingi inakinzana na Makuzi na Malezi ya Watoto.

Kwa miaka mingi ukipitia threads mbalimbali humu jukwaani utagundua kumekuwa na lawama kutoka kwa Wazazi kuhusu Suala la Muda wa Ziada kwa Watoto wa Madarasa ya Mitihani ambalo hupelekea watoto kushindwa kupata muda wa mapumziko au kujishughulisha na shughuli nyingine za kijamii.

Ifuatayo ni Barua kutoka katika Shule Moja jijini Dar Es Salaam kwa Wazazi na Walezi ambayo imetumwa mwezi Agosti 2026;

MPITO WA DARASA LA TANO KWENDA DARASA LA SITA – 2026/2027

Mzazi/Mlezi Mpendwa,

Kufuatia maboresho ya Mtaala wa Tanzania, wanafunzi wetu wa sasa wa Darasa la Tano wataingia Darasa la Sita na watachukuliwa kama darasa la watahiniwa , kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wao wa Kitaifa wa Darasa la Sita.

Kwa hiyo, kuanzia Septemba 2026, wanafunzi wa Darasa la Tano watafuata programu ya masomo iliyoboreshwa, inayofanana na programu itakayotumika kwa wanafunzi wa Darasa la Sita wanaohamia hatua inayofuata. Programu hii inalenga kuwapa wanafunzi maandalizi na msaada wa kutosha kwa ajili ya mitihani yao ya kitaifa ijayo.

Ili kuwezesha wanafunzi kushiriki kikamilifu katika programu hii iliyoongezwa, shule itatoa huduma ya bweni kwa wanafunzi ambao wanaweza kupata changamoto kuhudhuria programu hiyo wakiwa wanafunzi wa kutwa.

RATIBA YA KILA SIKU YA DARASA LA SITA
- Jumatatu – Alhamisi : Saa 12:00 asubuhi – Saa 2:30 usiku
Ijumaa : Saa 5:00 asubuhi – Saa 10:00 jioni
Jumamosi : Saa 2:00 asubuhi – Saa 2:30 usiku
Jumapili: Saa 5:00 asubuhi – Saa 10:15 jioni

Swali ni lini Wizara itaota MENO na kuanza kuchukua hatua dhidi ya tasisi hizi ambazo zinaenda kinyume na Malengo mbalimbali ya Serikali? Inashindwa nini kuchukua hatua kwa Taasisi hizi au Lisemwalo ni kweli kwamba Wamiliki wa Shule hizi ndio Viongozi wa Umma hivyo wanahusika nao kuharibu mifumo kwa kukusudia?
Haya tunajadili kwenye vikao vya wazazi na tunakubaliana wazazi na shule. Sidhani kama shule zinaamua tu bila kuwashirikisha wazazi.ukihudhuria vikao vya haya maamuzi shuleni ndiko mahali sahihi pa kufikisha malalamiko yako.kama unakua hujaridhishwa siyo lazima umruhusu mtotot wako kujumuika na wengine kwenye mpango huu.
 
Back
Top Bottom