Na hili ndo Tatizo Kuu. Siku zote Tanzania tumekuwa na Tatizo la kutunga sheria kwa mihemko hadi tunakuja kupata hasara. Ni shida sana kutumia nguvu ya kuua Tembo kuua sisimizi. Kama Tatizo lilikuwa matumizi mabaya ya fedha hizo wangekuja na utaratibu mzuri wa kudhubiti hayo matumizi mabaya sio kufanya maamuzi ya kuhatarisha kabisa sekta nzima ya uhifadhi na utalii.