Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wataalam wa Sayansi ya mpira tujadiliane kidogo kuhusu hili linaloendelea mitandaoni
Tangu mechi ya kwanza ya Ligi Kuu, Yanga akiwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar licha ya kushinda bao 2-0 bado kulizuka mijadala kuhusu kiwango chao, hata mechi zilizofuata (na CEB 1-0, Ken Gold 1-0 zote ugenini).
Mjadala ulikufa baada ya ushindi wa bao 6 kwa mtungi kwenye mechi ya marudio na CBE pale Zanzibar kwani ilionekana kama wamerudi kwenye utaratibu wao wa msimu uliopita 2023/24 wa kutembeza vipigo vikubwa na kutamba kwamba mashabiki wao washangilie angalau kuanzia bao la tatu na kuendelea.
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC ambao msimu uliopita Wana-Kino boys walipigwa jumla ya bao 8 kwenye mechi mbili, (5-0 na 3-0) hali ilirudi baada ya msemaji wao Ally Kamwe alibuka na tuhuma kwa Azam Tv akidai kuwa Wanapaswa kutafakari kuhusu utoaji wa habari zao, akionyesha tofauti katika mahojiano ya makocha wawili. Katika video ya kwanza, mwandishi anamuhoji kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, ambaye anatoa maelezo kuhusu ushindi wa timu yake. Hata hivyo, mwandishi aliendelea kuuliza kuhusu goli moja, bila kuzingatia umuhimu wa pointi tatu.
Katika video ya pili, mwandishi wa maswali hayupo na anajikita tu katika majibu mazuri ya kocha wa "Panya Road" ambaye pia ameshinda. Kamwe alidai kuwa kuna ajenda inayofanywa ili kuonyesha kwamba ushindi wa Yanga ni dhambi, na anashangazwa na jinsi Azam TV inavyoshiriki katika ajenda hiyo. Alisisitiza kuwa mashabiki wanapaswa kuwalinda wachezaji na makocha wa Yanga katika wakati huu mgumu wa ushindani.
Hali hiyo ilimuibua Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally na kutoa kejeli kwa Watani zao kwa kuandika: Sasa hivi Azam Tv kabla hawajafanya Interview na Mwalimu wa Nyuma Mwiko wanatakiwa kupeleka Maswali kwa viongozi wa Nyuma Mwiko wakiyapenda ndio anaulizwa
Hivyo hivyo kwa idara ya Digitali ya Azam Tv kabla hawajaandika Caption wanatakiwa waitume kwa viongozi Nyuma Mwiko wakifurahishwa nayo ndio ipostiweeee
Je, Yanga ameshuka kiwango na sasa anatafuta visingizio au ndio Propaganda za soka la Tanzania?