Je Yanga ni sikio la kufa?

Je Yanga ni sikio la kufa?

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
Muda mwingine unaweza kukubali kuwa Yanga ni sikio la kufa iwapo km suala la Fei Toto litawabwaga chini. Je Yanga hawakupata somo kupitia kwa Morison?

Ni kweli Yanga Wana wanasheria tena mahili, lakini sio kila nwanasheiria ni mjuzi wa sheria zote na Duniani kote hakuna mtu anasomea sheria kwa Kila jambo. Sheria ni sawa na udaktari, Kila mtu anasomea anachokilenga (specialisation).

Haya msikie huyu msomi:

Wakili na mwana michezo mzoefu nchini, Aloyce Komba ametoa ufafanuzi juu ya dili la Fei Toto kutua Azam akisema:
.
“Yanga wamefanya uzembe wenyewe na wasije wakathubutu kukimbilia Fifa kama walivyofanya kwa Bernard Morrison itakula kwao. Waangalie vizuri mkataba wa mchezaji unaeleza nini, watapoteza muda zaidi.”
.
“Ninachokiona Yanga walimpa mkataba Fei ambao hauna faida kwao. Unawekaje kiasi hicho cha pesa kuvunja mkataba wake wakati unaona kabisa kiwango cha mchezaji kilivyo. mchezaji hawezi kuacha pesa hasa kama mkataba wake unaruhusu kuununua ama kuuvunja.”
.
“Sioni kama Azam wamekosea na ni timu ambayo inazingatia sana masuala ya kisheria katika kuvunja mikataba ya wachezaji wao ama wanaposajili mchezaji. Azam siyo wajinga kiasi hicho wakurupuke tu kumsajili Fei Toto pasipo kuzingatia taratibu za kimkataba.
.
“Wanachotakiwa kukifanya Yanga ni kuulezea umma ama wanachama na mashabiki juu ya hilo, lakini mengine ni kuleta siasa tu kwenye mpira.”
 
Back
Top Bottom