Je Yanga SC leo wamezindua Jezi au ‘ Reflectors ‘ za Mafundi Ujenzi, Wafanyakazi wa Bandari au Watoza Ushuru wa Kupaki Magari?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mlioziona Jezi mpya za Yanga SC walizozizindua leo pale Serena Hotel karibuni ili muweze kutupa utofauti wa hizo Jezi na zile ‘ Reflectors ‘ ambazo mara nyingi huwa tunaziona zikitumiwa mno na Mafundi Ujenzi, Wafanyakazi wa Bandari na wale Watoza Ushuru wa Kupakia ( Maegesho ) wa Magari wa NPS.

Ila kuna Timu moja ( nimeisahau Jina lake kwa bahati mbaya ila nikiikumbuka nitaitaja hapa ) ambayo imezindua Jezi zake jana tu na tayari hata ‘ Wataalam ‘ wa Masoko na Biashara wa Vilabu vikubwa duniani kama vya Liverpool, PSG na Barcelona wamezisifia mno kiasi kwamba sasa wapo mbioni kuomba Michezo ya Kirafiki na hiyo Klabu kwani wamesema inaendeshwa Kisomi sana.

IGA UFE THIS IS NEXT LEVEL
 
"Mbona mnateseka?!!" Alisikika mlevi mmoja akiuliza.

Tunateseka kwasababu idadi ya ' Reflectors ' zinaongezeka nchini Tanzania na zinatuchanganya hivyo Mamlaka husika zianze Kuchukua hatua.
 
Ungeweka na kapichaa ndugu
 
Wewe Kuna kamanda huko kakutaja kuwa umepotea Sana kajitambulishe kwanza ndio urudi huku kwenye uzi wako.
 
Ungeweka na kapichaa ndugu

Bahati mbaya Mtandao wa JamiiForums huwa haukubali ' Reflectors ' kutumika hapa kwani zinaweza zikapofua Macho ya Watumiaji ( Members ) wake waliotukuka / tuliotukuka.
 
Wewe Kuna kamanda huko kakutaja kuwa umepotea Sana kajitambulishe kwanza ndio urudi huku kwenye uzi wako.

Nimeshawajibu wote ambao wameuliza nilipotelea wapi labda ulibakia ' Popoma ' Wewe tu Kujua.
 
Zile jezi zinafaa kuvaliwa na Team Membe mwakani kwenye kuchagua mgombea urais ndani ya CCM
 
Walianza wabrudishaji wakazindua then baba lao kamalizia shoo ya uzind
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…